Andrew Chenge asingeshindwa jibu(wages vs salary)

Andrew Chenge asingeshindwa jibu(wages vs salary)

Lazima upate kuipitia sheria kama kinachosemwa ni sawa kunauwezekano mjumbe ametafasiri tofauti hivyo inahitajika na wewe ujiridhishe kwanza kabla ya kujibu kisiasa
Adi apo umethibitisha uyo mwamasheria ni mvivu wa kusoma na kufatilia mambo muhimu.
 
Hivi wahitimu wa Havard hawana maadili kumbe? ndivyo wanafundishwa kuwa majizi kumbe!
Kuwa jizi ni tabia ya mtu kuanzia kwenye malezi, ukiona watoto umewapa andazi, alafu mmoja anang'ang'ania pande lake liwe kubwa, jua kabisa asipodhibitiwa atakuja kuwa tishio ata ofisini
 
Asante kwa kunisahihisha hiyo lugha ya kitumwa siijui sana mkuu. Kama ulifuatilia ule mkutano kuna mjumbe alitoa changamoto kuwa kuna sheria ya mfuko mmoja inatamka wages na inafanya calculation ya makato kutoka kwenye mshahara wa mfanyakazi baada ya ku include na allowances hivyo mchango unakuwa mkubwa ukilinganisha na sheria inayotamka salary ambapo makato yanatoka kwenye gross/basic salary hivyo ha include allowances. Kwa maoni yangu hii ilihitaji kusoma hizo sheria mbili ili kujibu kisheria zaidi na wala si kisiasa.
acha kutetea upepo
 
Ujanja sio kujua kila kitu off the head; ni pamoja na ujasiri wa mbele ya rais kusema sina hakika; HUYU NI MJANJA NA MWELEVU
 
Sijawahi kuwaamini ccm
Andrew Chenge maarufu kama joka la makengeza, mwanasheria hodari graduate from Harvard namkubali sana Kwa kutoa majibu ya hapo kwa papo Kwa masala yanayohusu Sheria.

Nilishuhudia mwanasheria wa serikali jana kwenye Kikao kuhusu mafao ikulu,akishindwa kufafanua tofauti ya wages na salary.

Wengine mtaweza kutetea ya kwamba siyo lazima ajue kila kitu ,binafsi sikubaliani na kushindwa kwake kufafanua tofauti iliyojificha baina ya wages na salary pale alipoombwa kufanya hivyo na rais. Sababu mkubwa ni kutopenda kujisomea Sheria na kanuni mbalimbali,tena Kwa Jambo siyo kama hili la mafao.

Kamwe joka la Makengeza hasingeshindwa kutoa ufafanuzi wa papo Kwa hapo iwapo ingetokea tokea fursa ya yeye kufanya hivyo (historia inamlinda Kwa hili kwani amefanya hivyo mara nyingi).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona yeye mwenyewe ana PhD lakinu kiingereza hawezi ongea na hatumshangai...
 
Hivi Chenge ni mhitimu wa Harvard kweli?
Unauliza jibu Ngosha, ndo maana na kuiba kote ila hakuna sehemu yenye ushahidi wa kumpeleka mahakamani. Ana akili kabla hajafanya jambo anahakikisha kishaona yajayo na haachi alama.
 
Kuna siku moja Chenge alikuwa anampa nondo Lissu ndo nilipokubali jamaa anajua sana sheria sema tu ana rekodi zake za kujihusisha kwenye madili. Kimaadili anatia shaka ila kwa ujuzi na utaalam wa sheria Chenge hana mpinzani nchi hii
Makinda alikuwa anamtumia Lissu kwa reference, kisha Andrew anakuja kutoa hitimisho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila mwanasheria bora alikuwa honest kuliko angejifanya anajua kumbe hujui. Kama kwenye medicine motto ni bora kusema hujui sio kosa as utajifunza, kosa fatal ni pale hujui halafu wajifanya unajua na ukakosea
 
Salary yangu ni Tsh 500,000/=
kwa mwezi
hii ndio basic yangu ninayokatwa Kodi, nhif, bima, nk
Kwa mwenzi.
Lakini
Wage yangu ni Tsh 700,000/
Kwa mwezi, kwani hapa nimeongezewa Allowance kama Usafiri Tsh 100,000/=na
Lesheni Tsh 100,000/=

Hivyo kuna mifuko ilikuwa inakata asilimia 10 toka kwenye Salary tu na kuhifadhi.
Na kuna mifuko mingine ilikuwa inakata asilimia 10 toka kwenye Wage yaani ile iliyo ongezewa na marupurupo.

Ndio ukabidi kuwe na uwiano mmoja wa makato, yaani makato yafanyike toka kwenye ama Salary au Wage kwa watumishi wote
Masahihisho yapo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilitakiwa ajue ,sababu ni wajibu wake alafu inshu ya mafao ilikuwa very hot,angejiongeza kujiupdate kuhusu mambo mbambali kuhusu iyo Sheria
Hapo ndipo tatizo lilipoanzia,pengine AG sio mpenzi wa kusomasoma kitu ambacho ni hatari sana kwa mwanasheria.
 
Back
Top Bottom