Andrew Chenge asingeshindwa jibu(wages vs salary)

Kuna siku moja Chenge alikuwa anampa nondo Lissu ndo nilipokubali jamaa anajua sana sheria sema tu ana rekodi zake za kujihusisha kwenye madili. Kimaadili anatia shaka ila kwa ujuzi na utaalam wa sheria Chenge hana mpinzani nchi hii
Kuna mtu mmoja aliwahi kusema kwamba kama Chenge angetumia elimu yake kuiba basi angeiba zaidi ya hicho ambacho aliiba tena kwa kutumia mianya ya sheria!
 
Hili ni swala la kiufundi. Katika sheria, maneno wage na salary yanaweza kubeba maana tofauti na ile ya common usage. Kwa sababu hiyo, ni lazima usome definitions za haya maneno kwa mujibu wa sheria husika; sio common-usage meanings.
 
Kwa Jambo hot lilioibuaa mjadala nchi mzima ,Kwa mtu makini angesoma Kwa undani masuala yote yanayohusu Jambo hilo (mafao na kikokoteo)
 
Huyo mwanasheria alishajua kesho yake kuna kibao kitakachojadili suala la mafao so km part of his homework angepitia pitia makabrasha kujiwekea sawa. Kwa ufupi ni kuwa jamaa kachemka and he is not one of the best lawyers wa nchi hii
 
Kweli kabisa
 
Kiufupi inaonekana siyo mtu anayependa kuangaisha ubongo Kwa kujisomea
 
Kuna mtu mmoja aliwahi kusema kwamba kama Chenge angetumia elimu yake kuiba basi angeiba zaidi ya hicho ambacho aliiba tena kwa kutumia mianya ya sheria!
Zimwi likujualo halikuli hukakwisha
 
Huyu Mwanasheria Mkuu alidhalilisha kada yake kwa kushindwa kujibu lile swali. Kuna wakati mchangiaji mmoja (nafikiri board member) aligusia na kusema kuna contradiction kati ya Salary na wage kwenye sheria ya NSSF na PSSSF hivyo smart lawyer alitakiwa pale pale apitie hizo sheria asome interpretation yake ili awe aware maana hata mm nilitegemea kuwa Mr. President akianza kuongea lazima angeuliza ili kupata clear definition. Sasa yule jamaa akaamua kulala usingizi aliposhituliwa akakimbia swali. Poor Ag.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fisadi na mwizi hawezi kuwa bora kwa uwezo wa kujibu maswali!!
 
Huyu Mwanasheria Mkuu alidhalilisha kada yake kwa kushindwa kujibu lile swali. Kuna wakati mchangiaji mmoja (nafikiri board member) aligusia na kusema kuna contradiction kati ya Salary na wage kwenye sheria ya NSSF na PSSSF hivyo smart lawyer alitakiwa pale pale apitie hizo sheria asome interpretation yake ili awe aware maana hata mm nilitegemea kuwa Mr. President akianza kuongea lazima angeuliza ili kupata clear definition. Sasa yule jamaa akaamua kulala usingizi aliposhituliwa akakimbia swali. Poor Ag.

Sent using Jamii Forums mobile app
Alishindwa kujiongeza
 
salary ni malipo ya mshahara. mshahara ni malipo kwa mfanyakazi anayopokea kila mwezi kutoka kwa mwajiri wake mpaka pale mkataba utakapofikia ukomo.
wages ni malipo ya ujira kwa wafanyakazi aina ya vibarua wanaolipwa kwa siku au kwa masaa.

utofauti ndio huo.
 
Andrew Chenge maarufu kama joka la makengeza, mwanasheria hodari graduate from Harvard namkubali sana Kwa kutoa majibu ya hapo kwa papo Kwa masuala yanayohusu Sheria.

Nilishuhudia mwanasheria wa serikali jana kwenye Kikao kuhusu mafao ikulu,akishindwa kufafanua tofauti ya wages na salary.

Wengine mtaweza kutetea ya kwamba siyo lazima ajue kila kitu ,binafsi sikubaliani na kushindwa kwake kufafanua tofauti iliyojificha baina ya wages na salary pale alipoombwa kufanya hivyo na rais. Sababu mkubwa ni kutopenda kujisomea Sheria na kanuni mbalimbali,tena Kwa Jambo ambalo lipo hot miezi ya hivi karibuni ,suala kama la mafao na kikokoteo .

Kamwe joka la Makengeza hasingeshindwa kutoa ufafanuzi wa papo Kwa hapo iwapo ingetokea tokea fursa ya yeye kufanya hivyo (historia inamlinda Kwa hili kwani amefanya hivyo mara nyingi).
Wewe ungetofautishaje basi,badala ya kulaumu ungekuja na jibu,kifupi Kiswahili ni tofauti na Kiingereza,kiswahili hakina neno la moja kwa moja kuhusiana na kitu kimoja,ni tofauti na kiingereza ambacho kwa mfano ukisema I love or I like yanakuwa na maana tofauti lakini kwa Kiswahili inakuwa taabu kuelezea utofauti,vivyo hivyo Kiingereza kina neno lake moja kuhusiana na kila jambo ambapo ni tofauti na kiswahili ,kwa hiyo basi unapokuja kutofautisha wage na salary kwa kiswahili kunakuwa hakuna neno la kutofautisha hayo mawili ,ingawa tunaweza kusema wage ni malipo kwa mtu ambaye hajaajiriwa au ni mwaajiriwa wa muda(kibarua)anaweza kulipwa kwa siku au wiki au hata mwezi lakini salalry ni malipo kwa mtu aliyeko kwenye ajira na anayelipwa kwa mwezi na ana haki ya stahiki zote kutoka kwa mwajiri wake.
 
Pole sana
 
Back
Top Bottom