Andiko lisemalo " Kila nafsi itaonja mauti" ni swali na sio jawabu. Wachina wameanza kujibu. Babu zetu walikaribia kabisa kupata jawabu

Kama kungekuwa na batani ya kukupa thousand likes ningefanya hivyo
 
Kama umesimuliwa umelishwa matango pori, kama umesoma habari mwenyewe basi ulipaswa utafute mtu mjadili ina maana gani maana upeo wako unarukia hitimisho. Iko hivi kupitia AI wataweza kufeed info za marehemu kwenye Robot kwa maelezo ya ndugu wa marehemu, then Robot ata act kama alivyokuwa marehemu na sio kwenda ku absorb nafsi ya marehemu.
Acha uongo wewe.
Kinachofanyika unawekewa chip kwenye ubongo inayochukua taarifa zako zote ukifa taarifa zako zinakuwa uploaded kwenye cloud computing server ambavyo wanadai your consciousness inakuwa inaexist kwenye cloud kwahiyo unakuwa hujafa
 
Acha uongo wewe.
Kinachofanyika unawekewa chip kwenye ubongo inayochukua taarifa zako zote ukifa taarifa zako zinakuwa uploaded kwenye cloud computing server ambavyo wanadai your consciousness inakuwa inaexist kwenye cloud kwahiyo unakuwa hujafa
Kwa hiyo hapo unakuwa umekufa au upo hai?
 
Unahitaji vitu vitatu Ili uishi milele (1)kuzuia kuzeeka (2) nguvu(sio hospitalini) ya kuondoa majeraha ya aina yoyote. Yaani kuurudisha mwili kama awali kama vile hujatokewa na chochote (2)nguvu ya kuzuia roho isichomoke

Mwanadamu bado sana kuzuia kifo.
 
Utapeli wao nini?

Au ndio una prove yale niliyo yaandika awali kwamba watu wa dini wana judge from the conclusion instead of towards the conclusion?
In simple ligic mwili unazeeka. Seli za nwili zinazeeka. Ni kudanganyana kudhani hayo yatatokea katika mwili huu wa nyama. Labda kwa marobot kama kwa hao wachina.

Pia umegusia suala la polupation, kwamba itafahamika. Hapo umecheza patapotea. Kwamba itafahamika wakati ukifika? Kwa nini hao wanasayansi wasiplan ahead? Kwamba kwa suala la population itakuwa hivi na vile. Tofauti na hapo ni kama haya ya bwawa la Nyerere tu. Au watu watapewa midawa kuzuia uzazi na ni wateule tu wangeweza kuishi (kama kweli hiyo alinacha ingefanya kazi)

So, ni lazima pawepo na uhamaji toka hali moja kwenda nyingine.
 
Haya bana anyways sisi tunaamini suala la kutafuta na hatimaye kupata teknolojia ya kuishi milele Mungu ameliweka mikononi mwetu wanadamu na kwamba sisi ndio tunao paswa kutegua hicho kitendawili..



Unadhani kipi kitakuwa more interesting kwetu.

A. Kugundua dawa/teknolojia ya kuishi milele tukiwa bado tupo hapa hapa duniani au


B. Mungu kutoa hiyo teknolojia baada ya kifo? Tukiwa nje ya dunia?
Katika kusoma kwangu quraan kuna vitu nimeng'amua, yote yamekuwa sababu yeye kataka yawe(ni elimu hiyo kairuhusu kwetu)
Na sema hivi kwa sababu gani
Kuna aya nimeisahau, inaongelea kuhusu elimu ya roho.
Anamwambia mtume wanakuuliza kuhusu roho, waambie ni jambo ambalo elimu yake ipo kwa mwenyewe muumbaji(kama sijakosea) hapo inaonesha ni kiasi gani hatuwezi jua sababu elimu hiyo katunyima,

Pia katika kisa cha kuumbwa adam, baada ya malaika kuleta bong'o bong'o nyingi kuhusu kuumbwa kwetu sisi, mungu kuwauliza mnajua zaidi yangu etc(nafupisha) mungu alipomaliza kumuumba mwanadamu akampa na elimu ya vitu vyote vya duniani, akawaita malaika kisha akawauliza majina na kazi zake, malaika wakawa hawana elimu hiyo, wakimwambia mungu wewe ndio mjuzi zaidi, kisha mungu akamuuliza bwana adam akawa anajibu, hi inaonesha elimu ni mpaka tupewe(tuko limited)

Jambo la 3 ni kisa cha malaika wawili wale walioleta uchawi haruta na maruta, maana yake ni elimu ambayo hapo kabla haikuwepo, na wakati wanafundisha watu wanawaambia haya ni katika makosa hivyo watu wajilinde wasifanye hayo mambo, ni moja katika mitihani kwetu sisi binadamu.

Jibu la B nalikubali kiasi, japo naamini hii elimu hatotupa ila ataitumia mwenyewe kuturudishia uhai kwenye kiama kisha kutuacha tuishi milele na milele bila maradhi wala kuzeeka.
 
Kufa utakufa hata utunge din yako, utakufa hata ulete mada zenye logic mia , utakufa hata uwe nan hakuna atakaye ishi kama jiwe. Hakuna cha mzungu wala mnyarugusub kifo hakikwepeki achen kudanganyana kama farao kifo ni kufatu basi hakuna kifo kuish

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi wafuasi wa dini za kiafrika tuna amini kwamba Mwenyezi Mungu (Chanzo cha vitu vyote ) alituumba wana wa dunia na kutuweka kwenye sayari ya dunia ili tuweze kujibu maswali mbalimbali ambayo yeye Mwenyezi Mungu ametuuliza.

Moja kati ya swali ambalo Mungu ametuuliza ni " Tutafanya nini ili kuhakikisha mwanadamu anaishi milele duniani/ kuondoa kifo?"

Kwa bahati mbaya sana waasisi wa dini mbili maarufu duniani; ukristo na uislamu pamoja na shina lao ( Judaism) wameshindwa kupata jawabu la swali hili ndio maana katika vitabu vyao wameliandika swali hili kana kwamba ndio " Jawabu"

Wanadai ya kwamba " Kila nafsi itaonja mauti"

Kwa sisi waamini wa dini za kiafrika pamoja na dini zote zenye mlengo wa kufanana na dini za kiafrika, tumegoma kuweka full stop baada ya sentensi " Kila nafsi itaonja mauti". Badala yake tumeweka alama ya koma (,) kisha tumeongeza sentensi nyingine kwamba, " mpaka hapo teknolojia ya kuondoa mauti duniani itakapo patikana". Kwetu sisi andiko hili lilipaswa kuwa " Je kila nafsi itaonja mauti"?

Tofauti kati ya dini za kiibrahimia / Abrahamic religions ( ukristo, uislamu na uyahudi) na sayansi ni kwamba dini za ki ibrahimia huwa zina address majibu ya maswali kuanzia kwenye hitimisho ( They address issues from the conclusion) wakati sayansi huwa in address issues kuelekea kwenye conclusion ( Science addresses issues towards the conclusion)

Mfano :
i. Dini: mtu akifa anaenda motoni au peponi( watu wa dini tayari wanalo hitimisho. Tayari wanajua mtu akifa atakwenda wapi)

ii. Mtu akifa anaenda wapi ? ( wanasayansi bado wanafanya tafiti kujua mtu akifa anaenda wapi na siku wakipata majibu basi yatakuwa ndio majibu sahihi zaidi kushinda majibu ya watu wa dini)

Mfano wa pili ;

i. Kila nafsi itaonja mauti ( tayari watu wa dini wamesha conclude. Japo ukiwauliza why ?. Au kwanini isiwe kinyume chake? Hawana majibu yanayo make sense)

ii. Wanasayansi ( Je ni kweli kila nafsi itaonja mauti? ) Ndio maana wapo wanatafuta jibu la swali hili.

Kwa bahati nzuri sana mababu zetu wa kiafrika walikuwa hatua chache sana kugundua teknolojia ya kuondosha kifo duniani.

Isinge kuwa watu wa dini hizi mbili uislamu na ukristo kuja kuwavuruga baadhi ya mababu zetu kwa kuwaambia mambo kama kila nafsi itaonja mauti basi sasa hivi huenda duniani tayari teknolojia hiyo ingeisha anza kutumika.

Na hii ni kwa sababu indication zote kwenye nature zina onyesha kwamba uwezekano wa uwepo wa raw materials kwenye ardhi ya dunia ambazo zina support human immortality technology ( wanadamu kuishi milele na kutokufa kabisa ) ni mkubwa sana.

Nilisha andika makala kuhusu mambo yanayo indicate uwezekano wa kuwepo kwa raw materials zinazo support uwezekano wa teknolojia ya kuishi milele duniani. Babu zetu walikuwa wamesha anza kuitumia teknolojia hiyo kama vile kutumia baadhi ya miti inayo fanya mtu asife mpaka yafanyike mambo fulani fulani. Baadhi ya miti hiyo ni pamoja na ule unaojulikana huko usukumani kama lufakale.

Vitu vingine ni kama uwepo wa miti ambayo baadhi ya wanyama na wadudu huitumia kuwafufua wenzao pindi wanapo kufa mfano nyoka wakiwa wanapigana mmoja wapo akafa basi yule.alie hai huenda kuchuma majani ya mti huo na kumtemea mwenzake mdomoni ambae hufufuka hapo hapo.

Uwepo wa teknolojia ya kumkopesha mfu uhai hasahasa mtu alie fia ugenini ili kupunguza gharama za usafiri. Kwa mfano mmetoka Kigoma.mmeenda Lindi baada ya kufika Lindi (let's say kilingeni kwa mganga), mwenzenu akafariki basi ipo miti ambayo huyu maiti analishwa anarudiwa na Uhai kisha ndugu zake mnaambiwa safirini nae hadi Kigoma but akishafika nyumbani kwao atatokwa na huo uhai wa mkopo na kurejea katika umauti wake.

Kuna miti hutumiwa na waganga makaburini anachapa kwenye kaburi linapasuka marehemu anatoka anazungumza nae.

Kuna dawa ikifukizwa kaburini usiku saa tisa wale.marehemu wote kwenye hilo kaburi wanatoka kwenye makaburi yao wanakuja kusikiliza umewaitia jambo gani.

Ipo miti ambayo mtu alie uwawa na watu hupakwa hufukiziwa kisha mtu huyo hurejewa na uhai na kisha kuulizwa nani alie muua pamoja na maswali mengine then mahojiano yakikamilika mtu huyo hurejewa na umauti.

Hayo ni baadhi ya maarifa waliyo kuwa nayo babu zetu.

Babu zetu hawakutikiswa kabisa na kifo. Katika kitu ambacho usingeweza kuwatisha nacho babu zetu basi ni kifo kwa sababu wao walikuwa wamesha fikia hatua ya kujua kwamba mwanadamu hafi anaishi milele. Ndio maana waliendelea kuwasiliana na mababu zao walio " kufa" kana kwamba bado wapo hai.

Mambo haya nimeyazungumza mara nyingi sana hapa jf.

Wenzetu ngozi nyeupe wanapambana kutafuta jawabu la swali hili ambalo Mungu ametuuliza.

Wiki kadhaa zilizo pita wachina walikuja na tangazo la uwepo ya AI Robbotic machine ambazo zinapelekwa kaburini mahali ulipo hifadhiwa mwili wa ndugu yako marehemu zina absorb his/ her consciousness ( personality) and then marehemu wenu anarudi.kuishi nanyi kupitia robbot huyo. So kila kitu kinakuwa cha ndugu yenu kasoro mwili wake tu ndio unakuwa wa huyo robbot.

Kuna teknolojia ya cloning.

Kuna kampuni huko Marekani ambao wana pambano kutafuta teknolojia ya kuishi milele. Mamilioni ya watu wanalipa mamilioni ya shilingi kwenye kampuni hiyo wakifa miili yao ihifadhiwe sehemu maalumu ili teknolojia ya kuishi milele itakapo patikana basi watu hao warejeshwe duniani kupitia miili yao.

Ama kweli tukipata jawabu la swali hili basi tutakuwa tumemfurahisha sana Mungu kwa sababu atasema hakika " these creatures are my true creatures"

Kuna wakati huwaga nina amini huenda Yesu alikuwa Time Traveller from the future alie kuja kutupa moyo wanadamu wa kizazi hiki kwamba in the future teknolojia.ya kuishi milele.itapatikana duniani na ikipatikana basi mfumo huu wa maisha ya sasa utakuwa replaced na mbingu mpya (mfumo mpya)

Kizazi cha watu watakao ishi miaka.kati ya 500 basi 1000 ijayo watawashangaa sana watu wa kizazi hiki kwamba ilikuwaje wakashindwa kugundua teknolojia ya kuishi milele mapema..

Kilaza atakuja na hoja " binadamu lazima wafe ili wengine wazaliwe kwa sababu ya kubalance ecosystem blah blah blah" Kama hiyo ndio hoja mbona Mungu alitaka.awali Adam na Hawa waishi duniani milele? Ingekuwaje?

Tukifikia hatua ya kugundua teknolojia ya kuishi milele then ishu ya population haiwezi kuwa tatizo kwetu kwa sababu tutakuwa na means za kudeal nayo.
Hakuna andiko la kila nafsi itaonja mauti kwenye Biblia. Halipo!


YESU NI BWANA NA MWOKOZI
 
Kwanini usiseme Cell?
Unahitaji vitu vitatu Ili uishi milele (1)kuzuia kuzeeka (2) nguvu(sio hospitalini) ya kuondoa majeraha ya aina yoyote. Yaani kuurudisha mwili kama awali kama vile hujatokewa na chochote (2)nguvu ya kuzuia roho isichomoke

Mwanadamu bado sana kuzuia kifo.
 
كُلُّ نَفْسٍۢ ذَآئِقَةُ ٱلْمَوْتِ ۗ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۖ فَمَن زُحْزِحَ عَنِ ٱلنَّارِ وَأُدْخِلَ ٱلْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ ۗ وَمَا ٱلْحَيَوٰةُ ٱلدُّنْيَآ إِلَّا مَتَـٰعُ ٱلْغُرُورِ


"Kila nafsi itaonja mauti, na bila
shaka mtapewa ujira wenu sawasawa
siku ya Kiyama. Na aliyewekwa mbali
na Moto na kuingizwa Peponi, basi
amefaulu; na maisha ya dunia hii si kitu
ila ni starehe idanganyayo."

3:185 Qur'an
Tazama BUMUNDA hili
 
Back
Top Bottom