Anayopitia mdogo wangu wa kike siyo sawa na umri wake, inaniumiza sana...

Poleni sana kaka, duh, noma sana haya maisha ila wewe endelea kumpa push pahali unapopaweza dadako, hata iwe kimawazo pia. Mwe positive na naamini mambo yatawanyookea very soon, naamini hayo kwani Mungu yupo na haachi watu wake.
Wanawake kwa kweli wanapitia magumu maradufu kutushinda ndio maana wanapaswa heshima yaani hawa dada zetu, mama zetu, shangazi, hata jirani wa kike, wanapitia aisee. Ila mzee baba, kaa ngangari, na usimweke mbali dadako hata siku moja. Mungu awaonekanie kila siku.
Imenitachi sana yaani, dah!
Bora wewe umegundua wanawake tunapitia magumu mara dufu yenu! Kwahilo tu Mungu akubariki!niliwahi sema uzi mmoja marufuku kbs kumcheka single parent wanapitia mengi sana nikavamiwa na malaika wa jf!
 
aise acha nami nikulalamikie kidg...! Unakumbuka nilikuunganishia kazi Mwanza mwaka juzi eh? Nikampa jamaa namba zako tunakupgia hupokei..! Binafsi nilishangaa na jamaa mie nilikua namjua ana roho ya huruma mno mno...kwanza suala la mshahara hata ungeshangaa hela anayokupa ungemsaidia sana sister ako..! Kwanza hakua na kazi alikua anTaka kijana tu wa kulinda jumba lake akiwa kazini..so ww ungepata fursa tena na tena za kufanya chichote as side hustle..anywys tuyaache haya

Namba 2 pole sana son....! Wewe ndo baba kwa hao wajomba! Mpe moyo dada kila uwezapo...
3.nitumie namba yake pm ila utamuambia wewe unitambulishe!

pole sana aisee!
 
Ni mdogo wangu wa kike, anayoyapitia yananiumiza mimi kama kaka yake. Najiona mwenye hatia ndani ya nafsi.

Wazazi wetu walifariki na kutuacha tukiwa wawili, tukiwa wadogo.

Mimi kama kaka niliingia mtaani na nikaishi mtaani kama chokolaa, nilishuhudia na kujionea ni namna gani wanadamu walivyo watu wa hovyo.

Kunyanyaswa, kuonekana mbwa mbele za watu ilikuwa kawaida kwangu mpaka nikaizoea hiyo hali.

Nimeishi kama mtoto wa mtaani mpaka nimekuwa kijana. Nimeyaona mengi huko.

Nikirudi kwa mdogo wangu wa pekee, alipewa mimba akiwa na miaka chini ya 16, mimi binafsi simlaumu kwa kupewa mimba, angejuaje hayo mambo kuwa yana madhara mbeleni? Alikuwa bado mdogo.

Kwakuwa mdogo wangu alikua hasomi, kupewa kwake mimba haikuwa jambo la kushangaza wala kushtua watu, ukizingatia hakuna mzazi wala mlezi aliyepo.

Alilea mimba na akajifungua katoto, kasichana, nikapewa nafasi ya kumchagulia jina, nikasema aitwe 'Furaha' .

Akapewa tena mimba, naamini ni katika kujaribu kujitafutia nahitaji yake na mwanae, alipewa mimba tena.

Afanyeje sasa? Msaada ninaoutoa kwake ni kama tone ndani ya bahari, si chochote, haisaidii. Na sasa naona magumu zaidi yamemfika.

Mara kadhaa hunipigia simu huku akilia na kusema maneno ambayo binafsi yananiumiza sana, ananiambia mpaka mambo ambayo kwakweli naamini hakupaswa kuniambia, lakini amwambie nani sasa? Mimi ndiye ndugu yake.

Anayopitia siyo sawa na umri wake, hii hali inaniumiza sana mimi kama kaka yake. Nazikumbuka sana nyakati nzuri tukiwa na wazazi wetu.

Mimi binafsi nimejifunza mengi katika kuishi, nimepata changamoto nyingi hata sasa nazikabili.

Ila changamoto anazopata mdogo wangu ni kubwa Mara dufu, ana watoto, hana mzazi wala mlezi, anawatunza vipi watoto?

Haya maisha ni hovyo.
Anayopitia siyo sawa na umri wake, hii hali inaniumiza sana mimi kama kaka yake. Nazikumbuka sana nyakati nzuri tukiwa na wazazi wetu.

Siku njema zijapopita usihuzunike bali ufurahi kwakuwa zilikuwako!
Mungu atampigania
 
Mchukue ukae nae karibu,maana mkiwa karibu hata wewe mwenyewe binafsi utapata utulivu na amani kuliko akiwa mbali na wewe halafu kila wakati unawaza ..leo kapatwa na nini huko, Unakosa utulivu cha msingi mchukue ukae nae karibu mkuu.
 
Sijui ni changamoto gani anazo zipitia lakn kwa maelezo yako binafs nimekuelewa na nakupa pole wewe na mdogo ako haya ndo maisha, ...cha msingi hakuna kukata tamaa kesho ya mwanadamu ni fungu kikubwa dua

Mungu awatie nguvu na akiri ya kuwayashinda majaribu...

Usisahau kuwaombea zaidi walio na matatizo makubwa kukuzidi na mungu atakuinua
 
Poleni sana mkuu. Omba msaada wowote hapa na tutachangia kadri ya uwezo for your sisy.

Watoto wa kike wanapitia magumu mno mno mno na changamoto nyingi kwa maisha ya sasa... hasa wanaotokea familia masikini.

Ukimkuta single mother out there usimkebehi wala kumdharau. Ni kumuombea na kumpa support kadri iwezekanavyo.

Wanapitia the hard way to survive this world of irresponsible fathers.

I know and am closely witnessing what I am talking here.

-Kaveli-
 
Jamii kubwa kwa sasa inakumbwa na tatizo la irresponsible fathers.

Family break-ups zimekuwa nyingi.

Pia, mabinti kuzalishwa na kutelekezwa imekuwa kama jadi.

-Kaveli-
 
Wanawake muda mwingine n wajinga sana.
Anapgwa mimba anatelekezwa,anahangaika nayo baada ya muda kidogo unaona kapgwa nyingine tena,huu ni upumbavu.

Kama umeamua kutumia uchi kutatua changamoto,basi tumia njia ztakazo zuia mimba.

Mimi wanawake wa hiv hata huwa siwahurumii hata kidogo
Kabisa mkuu, me mwenyewe ni ndugu yangu kazalishwa na jamaa na kiuhalisia familia ya yule jamaa haimtaki kutokana na Dini yake

Ila cha ajabu anaenda kulala kwa jamaa anarudi Asubuhi nyumbani

Inshort mkuu hawa watu wakati mwingine siyo akili zao watu wanakua washafanya yao yaani kuwapumbaza kichawi.
 
Poleni sana mkuu. Omba msaada wowote hapa na tutachangia kadri ya uwezo for your sisy.

Watoto wa kike wanapitia magumu mno mno mno na changamoto nyingi kwa maisha ya sasa... hasa wanaotokea familia masikini.

Ukimkuta single mother out there usimkebehi wala kumdharau. Ni kumuombea na kumpa support kadri iwezekanavyo.

Wanapitia the hard way to survive this world of irresponsible fathers.

I know and am closely witnessing what I am talking here.

-Kaveli-
THE WORLD OF IRRESPONSIBLE FATHER'S!!! Mungu wasaidie wakina Mama waliotelekezwa na wanaume!! Kwa kweli wanapitia magumu mengi!!
 
Yap
But trust me haikua rahisi mpaka nikamtoa moyoni nimepambana sana kusamehe
I know honey.

God bless your beautiful heart.

Mtekelezee majukumu yake kama Mzazi.

Na umuombe Mungu ukiwa baba na wewe huyu tushetani tusikushawishi na wewe.🤫🤫😃😃
 
I know honey.

God bless your beautiful heart.

Mtekelezee majukumu yake kama Mzazi.

Na umuombe Mungu ukiwa baba na wewe huyu tushetani tusikushawishi na wewe.🤫🤫😃😃
Thank you my dear
Nimejifunza sana
Mungu anisaidie nisipite njia hiyo watoto ntawaumiza wakati hawana hatia
It,s more like psychological torture and trauma
 
Back
Top Bottom