Anayopitia mdogo wangu wa kike siyo sawa na umri wake, inaniumiza sana...

aise

JF-Expert Member
May 16, 2018
2,538
2,000
Ni mdogo wangu wa kike, anayoyapitia yananiumiza mimi kama kaka yake. Najiona mwenye hatia ndani ya nafsi.

Wazazi wetu walifariki na kutuacha tukiwa wawili, tukiwa wadogo.

Mimi kama kaka niliingia mtaani na nikaishi mtaani kama chokolaa, nilishuhudia na kujionea ni namna gani wanadamu walivyo watu wa hovyo.

Kunyanyaswa, kuonekana mbwa mbele za watu ilikuwa kawaida kwangu mpaka nikaizoea hiyo hali.

Nimeishi kama mtoto wa mtaani mpaka nimekuwa kijana. Nimeyaona mengi huko.

Nikirudi kwa mdogo wangu wa pekee, alipewa mimba akiwa na miaka chini ya 16, mimi binafsi simlaumu kwa kupewa mimba, angejuaje hayo mambo kuwa yana madhara mbeleni? Alikuwa bado mdogo.

Kwakuwa mdogo wangu alikua hasomi, kupewa kwake mimba haikuwa jambo la kushangaza wala kushtua watu, ukizingatia hakuna mzazi wala mlezi aliyepo.

Alilea mimba na akajifungua katoto, kasichana, nikapewa nafasi ya kumchagulia jina, nikasema aitwe 'Furaha' .

Akapewa tena mimba, naamini ni katika kujaribu kujitafutia nahitaji yake na mwanae, alipewa mimba tena.

Afanyeje sasa? Msaada ninaoutoa kwake ni kama tone ndani ya bahari, si chochote, haisaidii. Na sasa naona magumu zaidi yamemfika.

Mara kadhaa hunipigia simu huku akilia na kusema maneno ambayo binafsi yananiumiza sana, ananiambia mpaka mambo ambayo kwakweli naamini hakupaswa kuniambia, lakini amwambie nani sasa? Mimi ndiye ndugu yake.

Anayopitia siyo sawa na umri wake, hii hali inaniumiza sana mimi kama kaka yake. Nazikumbuka sana nyakati nzuri tukiwa na wazazi wetu.

Mimi binafsi nimejifunza mengi katika kuishi, nimepata changamoto nyingi hata sasa nazikabili.

Ila changamoto anazopata mdogo wangu ni kubwa Mara dufu, ana watoto, hana mzazi wala mlezi, anawatunza vipi watoto?

Haya maisha ni hovyo.
 

Mac Bully 001

JF-Expert Member
Jun 26, 2012
6,548
2,000
Poleni sana kaka, duh, noma sana haya maisha ila wewe endelea kumpa push pahali unapopaweza dadako, hata iwe kimawazo pia. Mwe positive na naamini mambo yatawanyookea very soon, naamini hayo kwani Mungu yupo na haachi watu wake.
Wanawake kwa kweli wanapitia magumu maradufu kutushinda ndio maana wanapaswa heshima yaani hawa dada zetu, mama zetu, shangazi, hata jirani wa kike, wanapitia aisee. Ila mzee baba, kaa ngangari, na usimweke mbali dadako hata siku moja. Mungu awaonekanie kila siku.
Imenitachi sana yaani, dah!
 
Mar 22, 2015
39
95
Pole sana mkuu, ila ingependeza umchukue dada yako uishi naye kwa hali yoyote na wanae endelea kupambana mpaka Mungu atakapokuvusha kwenye huo mtihani.

Pole sana, ni changamoto unapitia itumie kama fursa kwa kupambana kwa hali na mali na hakika Mungu ni Mwema utavuka na mambo yataenda sawa.
 

Redpanther

JF-Expert Member
Feb 23, 2019
2,430
2,000
Kwahiyo mkuu, dada yako kupigwa mimba/kuzalishwa, kwako wewe kama mwanaume wa familia unaona ni sahihi!!! Most of them waswahili/wazazi/makaka hawako serious kwa mabinti zao.

Kingine unakuta binti anaishi na bwana kwa maana wachumba/wanaharusi watarajiwa, na hapo hapo wanaishi pamoja bila kufunga ndoa, washatiana mimba baada ya hapo wanapata mtoto/amebarikiwa mtoto 😱 huu ni upumbavu kabisa, na wazazi wanaangalia tu.
Kichwa chako kinashida, katika uliyoyaona sijaona tatizo lolote ila kichwa yako imejaa maji tu. Ni nani alikuambia mzazi/kaka unapaswa kuzuia hisia za dada yako kwa mtu anayemjali labda akiwa under 18 lakini binti anapokuwa Mkubwa tayari anakuwa anauwezo na haki ya kuamua nini kitokee au kipi achague.

Labda nikuulize! Kwa mfano dada yako ameamua kuishi na mpendwa wake wakaja kujitambulisha nyumbani na bahati nzuri wakapata Mtoto na maisha yao yako vizuri tu, wewe kaka utakuwa na nguvu ya kwenda nyumbani kwa dada yako kumzingua yeye na mumewe/mzazi mwenzie kisa tu hajafunga ndoa kanisani?

Utumwa wa Dini unakusumbua wewe!

Ushuri wangu kwa jamaa (Mtoa maada) akaze tu na pia anapaswa kuwa karibu na dada yake kadri awezavyo kwa maana wao ndio ndugu wanapaswa kushikana mkono na ikiwezekana dada atumie uzazi wa mpango kuepuka mimba zisizo tarajiwa.
 

trey007

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
750
1,000
We jamaa hicho kichwa chako kina mushkeli sehemu
Kwahiyo mkuu, dada yako kupigwa mimba/kuzalishwa, kwako wewe kama mwanaume wa familia unaona ni sahihi!!! Most of them waswahili/wazazi/makaka hawako serious kwa mabinti zao.

Kingine unakuta binti anaishi na bwana kwa maana wachumba/wanaharusi watarajiwa, na hapo hapo wanaishi pamoja bila kufunga ndoa, washatiana mimba baada ya hapo wanapata mtoto/amebarikiwa mtoto 😱 huu ni upumbavu kabisa, na wazazi wanaangalia tu.

🇦🇷🇦🇷🇦🇷🔥🔥
 

Kokolo

JF-Expert Member
Mar 20, 2008
1,210
2,000
Pole, kuwa naye karibu sana, mpe watumaini, mwambiye afanye biashara ndogondogo kuuza uji na mihogo, viazi, sambusa , auze chai , vitu vidogovidogo vya kupata elfu kumi kwa siku, weka mpesa tukusaidiye kiasi kidogo Cha kuanzia huyo Dada yako, poleni sana kwa kuondokewa na wazazi wote imagine na ndugu wa siku hizi hawana msaada sana, yaani hapo ni kama ndege asiye na mabawa pole sana mkuu ibox number yako tukusaidiye kianzio kiasi inauma sana.
 

That Gentleman

JF-Expert Member
Dec 16, 2016
1,699
2,000
Pole mkuu ila tambua kuwa changamoto tumeumbiwa wanadamu, jitahidi sana kuwa karibu na dada yako kwa kumfariji, kumpa elimu na ushauri wa mara kwa mara.

Wewe ndiyo baba yake + mama yake so kaza mkuu japo mambo ni magumu ila komaa tu.

Kila kitu ni mpito tu, hata hizi nyakati ngumu (shida) tulizonazo zitapita tu. Have a heart ♥
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom