Anayefahamu kanisa zuri lenye sifa zifuatazo, anijulishe nijiunge tafadhali

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,397
Kusali ni muhimu, lakini baadhi ya tabia na sheria za baadhi ya makanisa yanachangia sana kuvunja moyo watu kuabudu.

Naomba mwenye kujua kanisa lolote lenye sifa zifuatazo ili nijiunge;
  1. Liwe ni kanisa la kikristu
  2. Liwe na mfumo wa kitaasisi (yaani management iwe kimfumo wa kitaasisi)
  3. Liwe linapatikana angalau kila wilaya/mkoa
  4. Misingi ya waumini wake iwe ni ile ya teamwork (umoja bila kubagua masikini au tajiri hususani wakati wa matatizo ya mmoja mmoja)
  5. Liwe ni kanisa lisilotegemea uwepo wa mchungaji/kiongozi mmoja
  6. Liwe ni kanisa lenye ratiba maalum ya kuzingatiwa (standards)
  7. Liwe ni kanisa linalojali malezi ya watoto kiroho
  8. Liwe ni kanisa la watu wenye akili timamu.
  9. Liwe ni kanisa lenye kupenda haki, usawa na uwazi
  10. Liwe ni kanisa linaloponya, kukuza na kujenga imani kwa waumini wachanga n.k
Yoyote anayefahamu kanisa lenye hizo sifa anifahamishe!! Natafuta kanisa la kujiunga!
 
Sidhani kama kuna kanisa la aina hii duniani hapa, makanisa mengi suala la haki sijui kuangalia haki za binadamu hakuna. Ndio maana wametulia kuhusu mgogoro kati ya Israel na Parestina
Huenda likawepo tusichonge ngoja wadau watupe maoni
 
Back
Top Bottom