Uislamu uheshimiwe kuanzia ndani, kabla ya kuheshimiwa na wengine

Diwani

JF-Expert Member
Oct 25, 2014
2,672
2,697
Amani iwe nanyi Ndugu zangu Waamini wa dini ya Kiislamu.

Pokeeni Salamu kutoka kwa Ndugu wa Imani ya Mungu mmoja kwa muongozo wa Injili Takatifu na Mjumbe wake Yesu Kristo.

Mimi ni shuhuda wa wazi wa Imani yenu kwa sababu, Uungwana wenu umenipa fursa ya kuijua imani yenu Takatifu na kujifunza misingi ya mafunzo baadhi ya Utu na Udugu kama yalivyoteremshwa kutoka kwa Muumba kwa kinywa cha Mtume Mohammad (SAW), Mjumbe mtiifu wa Mwenyezi Mungu na kunakiliwa katika Quran Tukufu.

Kwa mujibu wa tovuti ya Pew Research Center Uislamu ndio itakuwa dini yenye Waumini wengi zaidi duniani ifikapo Mwaka 2060. Hii ni kutokana na sababu kama

  • Ndoa za mitala: ni ndoa zinazohusisha Mume mwenye Mke zaidi ya mmoja. Ndoa hizi zinachangia ongezeko la watu kwa sababu ya kuzaliana kwa kasi kati ya Waumini wa dini hii. Hivyo, inakadiriwa, mpaka ifikapo mwaka 2050 kutakuwa na kundi kubwa la Waumini kwenye Familia za Kiislamu.
  • Kuanguka kwa Imani ya Kikristo eneo la Ulaya na Amerika: imani ya Kikristo ni kati ya imani zinazopitia changamoto kubwa duniani kwa maeneo haya mawili. Kwa sababu, ipo katika eneo lenye ukuaji wa Falsafa za Kiliberali zinazochagiza kufa kwa imani ya Mungu mmoja, yaani Atheism. Eneo la Ulaya ndilo lililoathirika zaidi na mifumo hii, kiasi cha dini ya Kikristo kupoteza mvuto na ushawishi.
  • Kubadili imani kwa Waumini wengi wa Kikristo na Wasio na dini katika eneo la Ulaya na Amerika: jambo lililosababishwa na kupotea kwa mvuto wa dini ya Kikristo inayoshambuliwa na ajenda kam Ushoga, Uliberali, Ushetani (Satanism) na Ufemini. Hivyo, watu wengi wa maeneo hayo kutafuta imani mpya ya kuendelea kumuenzi na kudumisha imani ya Mungu mmoja.
  • Uhamiaji wa wakazi wengi wa eneo la Uarabuni, lenye idadi kubwa ya Waislamu katika maeneo mengineyo duniani ikiwamo Ulaya.

Mambo haya na mengineyo ambayo hayajaainishwa yataifanya Imani ya dini ya Kiislamu kuwa imani yenye nguvu na Ushawishi kutokana na idadi ya Wafuasi wake. Hivyo kuondoa Utawala wa muda mrefu wa imani ya Kikristo uliodumu kwa muda mrefu, na kuingia ukurasa mpya wa uso wa dunia katika imani.

Je, dini kama Taasisi imejiandaaje?
Kwanza naomba tutofautishe, Imani na Dini. Dini ni njia ya kufika kwenye imani, dini ni Taasisi pia ya kusimamia na kudumisha Imani Fulani. Hivyo, inapaswa kuwa na misingi ya Kiimani na Misingi ya Kiutawala.

Ikiwa Uislamu itakuwa dini yenye Ushawishi mkubwa kuliko zote, hivyo, jukumu la kuilinda amani ya dunia, litakuwa juu yake. Kama dini isisitizavyo. Hii haitamaanisha kuwa, hakutakuwa na dini nyinginezo. Je, suala la Elimu dunia litabaki kuwa si kipaumbele kama mnavyonadi leo hii? Madai ya kuwa Quran imefunza kila kitu, yanathibitisha.

Kwa sababu, kwa namna yoyote niwatazamavyo viongozi wa dini ya Kiislamu hapa nchini, naona Uislamu umekomaa kiimani, ila si Kitaasisi, yaani ni kama Kondoo waliokosa mchungaji. Mniwie radhi ndugu zangu Waprotestanti, hivyo ndivyo hata ninyi mlivyo. Hakuna Utawala wa Kitaasisi, bali wa Utashi wa mtu mmoja, yaani Mchungaji wa kila kanisa, kwa mapenzi yake na namna atakavyojisikia.

Sioni nguvu wala Ushawishi wa BASATA, ila ni matarajio yangu kuwa, itakuwepo siku za usoni. Kwa ukuu na nguvu ya dini ya Kiislamu, msikubali ikatwezwa si tu na wale wasio Waislamu, bali hata wale viongozi wenu, wenye Mamlaka juu ya dini yenu.

Nimewiwa kuandika hivi kwa sababu ya toni (tone) ya chuki inayohubiriwa na baadhi ya viongozi wenu, Je, hakuna Kiongozi mmoja wa kutoa msimamo wa wote? (Rejea sakata la bandari) ni hii dini inayochukua nafasi ya Imani ya Mungu mmoja duniani?

Kama ndivyo, naamini kuna mabadiliko mengi yatafanyika, ikiwamo kulazimu elimu ya dunia kuwa sehemu ya Utaratibu wa Imani. Kwa lengo la kukuza dini kama Taasisi, si tu dini kama Imani.

Kwa sababu, Uislamu ni Mmoja. Msiache dini igawanyika sana kama dini yetu ya Kikristo, kiasi cha kuwafanya kondoo kuhubiriwa yasiyo mafundisho ya Imani yetu. Hili litawezekana ila si kwa Utashi mdogo wa wengi wa viongozi wenu.

Asalaam Aley’kum.

Diwani

Projected 1.jpg
Projected 3.jpg
Projected 2.jpg
 
Naona uzi Umepoa!

"we Must respect the other fellows religion,but only in the Sense and to the extent that we respect his theory that his wife is beautiful and his children smart"...



Man is and always has been a Maker of god's.
 
Back
Top Bottom