Anayeangalia mechi ya Simba vs Tembo(FA) inaonyesha mpira wa back pass upo kwenye damu ya wachezaji wa Kitanzania kabisa

THE FIRST BORN

JF-Expert Member
Apr 24, 2019
1,727
3,286
Wasalam wanajukwaaa.

Nipo naangalia hii Match ya Simba na Tembo ya FA Aisee inakera badooo sana, Yani zile beki zinachokifanya ndio kile tumetoka kukiona kwenye Team ya Taifa. Japo sio wote walikua Team ya Taifa ila hiki ni kielelezo kua Kumbe wachezaji wa Kitanzania swala la kuchezea Mpira Nyuma Lipo Damuni.

Nasema kama mtu ananipinga hapa angalia Mpira akishika Mchezaji wa kigeni kama Kanoute,Luis Miq,Saido wote hawa wana force wanafanya Turns za kwenda Mbele sio za kurudisha Mpira nyuma.

Ukibisha Nenda kibanda umiza saiv angalia hii game kama huna Azam kwako.

Nasema utachukia sana Mtu anapokea mpura Nyuma hata hajakabwa anarudisha kwa golikipa mara wanagongeana wao tu wakat kule mbele Fowards hajapata Mpirà.

Ili SOKA La Bongo Li badilike linatakiwa Lianzie kwa vilabu vyetu Maana sisi wachezaji wetu Asilimia 90 wanatoka Ligi ya Ndani sio kama Mataifa Mengine ambayo Team zao za Taifa zinaundwa na wachezaji wanaocheza Nje ýa Nchi hususan ulaya ambako Mpira wa back Pass ni Criminal offense kabisa.

Kwa soka hili la back pass hata tulete Pep Team ya Taifa haitotoboa Maana mchezaji kafundishwa kuchezea mpira Nyuma..Labda wachezaji wa Team ya Taifa wote watokee vilabu vya Mataifa ya Nje ya africa.
 
Subiri walau AFCON iishe mkuu...

Yanini haya Sasa...

Achana nayo
Hili soka linakera sana kaka..unaangalia coz sisi tunapenda Mpira kama hakuna Match nipo Radhi niangalie hata Marudio.

Saiv ipo hii game naangalia ila inaumiza lakn ukiwa unaumia unagundua kumbe lile tatizo tulilokua tunalilalamikia Team ya Taifa Afcon linatengenezwa huku.
 
Watoto Wana mjini Wana kamsemo...

Kama inauma Vaa nenda
 
Wasalam wanajukwaaa.

Nipo naangalia hii Match ya Simba na Tembo ya FA Aisee inakera badooo sana, Yani zile beki zinachokifanya ndio kile tumetoka kukiona kwenye Team ya Taifa...
Kwenye kikosi cha Simba kilichoanza leo, wamecheza wabongo tupu? Au wabongo pekee waliopangwa ndio wanaocheza back pass?
 
Hili soka linakera sana kaka..unaangalia coz sisi tunapenda Mpira kama hakuna Match nipo Radhi niangalie hata Marudio.

Saiv ipo hii game naangalia ila inaumiza lakn ukiwa unaumia unagundua kumbe lile tatizo tulilokua tunalilalamikia Team ya Taifa Afcon linatengenezwa huku.
Kuna siku Shabalala alirudisha pasi nyuma wakati kuna wachezaji mbele yake,Benchika alikuwa karibu pale kwenye mstari akamgombeza shabalala kwa kujionyooshea kidole kichwani kwamba ( huna akili), back pass simba inakera sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuuu zina kera Mnoo yani unajiuliza kwanini usimpe mtu Mali akatembea nayo.

Kama unafatilia games za Mali wale watu wanapiga boli ujue wanapeana pasi hata katikati ya watu halaf mtu ana vunga kama anarudi nyuma then anapiga turns anapiga pasi ya mbele.

Hili swala la back pass kwa Team zetu linatengenezwa mbali mno yani mtu anatengenezewa Mind set kua usimpe mtu mpira akiwa kasogelewa na Mpinzani. Wanafanya hivo huko mazoezin.

Ndio maana unaona mtu yupo katikati ya wachezaji pinzan na hajakabwa kivile hapew mpira anapewa alie nyuma coz hajazungukwa na wachezaji wa Team pinzan.

Na hili Kocha wa Simba anatakiwa alipige Vuta sana hata Team zote kwa ujmla.
 
Back pass, kuupozesha mchezo na kuridhika ndio ugonjwa sugu wa Simba hata aje kocha gani. Labda makocha wawe wanatembea na fimbo itasaidia. Simba wakishafunga goli mbili tu hata kama timu ya kupiga goli kumi basi jua biashara imeishia hapo. Tegemea KUONA back pass nyingi, watu kutembea na mpira na wachezaji kupigiana pasi fupi fupi wakiwa karibu.

Kwa mfano kwenye mechi ya jana wakati kapombe anapiga pasi nyingi kwenda mbele na kuachi mpira haraka kila anapoupata kiungo mwenzie Kanoute anakaaa na mpira zaidi ya sekunde 30 na kuipozesha timu isiende mbele kwa haraka tena wakati mwingine anageukia nyuma kabisa wakati yeye ni kiungo wa ushambuliaji.
 
Wachezaji waliokuwa wanapeleka mpira mbele Kama Peter Banda, Sackho walikuwa ama kuachwa, timu imeshavuka mstari wa kati halafu inapigiwa back pass. Ndio maana pamoja na mafanikio ya klabu za Tanzania wachezaji wanaochukuliwa ni WA kutoka nje.
 
Back
Top Bottom