Anawaonea huruma CHADEMA lakini.....

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
4,080
5,045
Nimesoma mahali andiko la Jasusi Chahali kuhusu Mbowe kuwa mahabusu kwa siku tisini.

Katika andiko lake hilo amesikitishwa na kitendo hicho lakini kama nimemsoma vizuri mwishowe amewaangushia jumba bovu Chadema.Amewalaumu Chadema kumkumbatia Kigogo wakati wakijua fika Kigogo alikuwa mwizi anayetafutwa.Pili ameonyesha kuwa Chadema kuwashabikia wanaharakati wanaondesha mijadala mingine kuhusu Katiba mpya,na kwa uelewa wangu ni kama anawasikitikia Chadema kuingizwa chaka tena!!

Yote aliyoyaandika yanaweza kuwa kweli lakini hebu tuchukue nafasi ya Chadema katika hayo yaliyozungumzwa na tuyatizame kwa jicho la tatu.Kama ilivyo kwa binadamu wote ni vigumu kujua anachowaza mtu na mara nyingi tunaaminiana au kutuhumiana bila hata ushahidi wa kina.Kwa Chama cha siasa kuweza kuwajua wabaya na wazuri ni kudra ya Mungu tu.Jambo hili linawafanya mara nyingi wawe suscipious ambayo inawasaidia kutokupanga jambo lolote ovu (Hamuaminiani).Hii ni safety mechanism ambayo kwa mtizamo wangu imewasaidia sana Chadema mpaka kufika hapa walipo leo.Wangepanga kitu chochote fishy si ajabu wangeshapotea wengi!!Lakini jambo hili athari ingine kubwa hasa ikiwa Chadema wataendelea kuonewa ni kusababisha watu kupanga mambo kama individual na madhara yake ni kutokea watu kama kina Hamza.

Tukija kwa wanaharakati hata mie binafsi siwaamini sana,kuna mmoja maarufu hajapata msukosuko hata mmoja pamoja na harakati zake,kuna mwenyekiti wa Chadema wa wilaya moja ambaye kwa maandishi yake ungetegemea apate msukosuko lakini wapi.

Utamwamini nani kwani hata Bwana Chahali,mkosoaji mkubwa wa serikali aliwahi kukiri kudhulumiwa pesa na Kinana (Je alimfanyia Kinana,(Katibu Mkuu wa CCM) kazi gani,ajuaye ni Mwenyezi Mungu.

Chadema imeondokewa na makatibu wakuu wawili (watendaji wakuu wa Chama na waendeshaji wa shughuli za kila siku za chama),hawa si watu wadogo.Ni kipi walikisema walipokwenda huko ni kipi walikitoa kwa hiari na ni kipi walilazimishwa au kulaghaiwa, hakuna ajuaye ila Mwenyezi Mungu na katika hatua hiyo HAKUNA WA KUMUAMINI ni kumuachia MUNGU TU!!
 
CDM ni chama kikubwa sana kuliko CCM. na ndiyo maana CCM wanahaha kila kona kuminya demokrasia nchini...CDM inasonga mbele.

Ogopa sana chama kinachojiongoza kwa nguvu za wanachama.

Mwendazake na madogo walifanya hila, na sasa wamegeukiana wao kwa wao..hakuna wa kuua CDM labda muumba tu kama ataamua na iwe hivyo..ila kwa binadamu anayehema nasema HAKUNA, Sabaya kajaribu kaishia kunyea debe, Wakataka kummua Lissu leo ni mzima anahema.


Kwa mamlaka ya roho mtakatifu nasema hivi Free Mh. MBOWE si gaidi, naruhusu sasa nguvu za MUNGU zifanye kazi yake.
 
Chadema haihitaji support ya yeyote ili iwe ilipo, ile ni super brand; ni wapuuzi tu ndio huwa wanaidandia kutafuta umaarufu.
 
Huyo kigogo na Chadema mbona ngoma haipandi huu mwezi wa pili sasa baada ya Kigogo kusuggest Chadema iunde jeshi na Lissu kuyaita mawazo yake ni ya kijinga?
Chadema haujawahi kuwa mashabiki wa Kigogo bali ni Kigogo ndie aliyejifanya shabiki wa Chadema. Chadema watatumia platform yeyote ambayo wataona inafikisha ujumbe wake kwa wengi. Sasa hivi wafuasi wao wako kwa Maria ingawa yeye na Fatma si wanachama wao. Hii ni kwa sababu wakina Maria wanaongea ukweli wao bila uoga na hawasiti kutetea haki ya Chadema kufanya siasa bila kubughudhiwa.

Amandla...
 
Na hawa mashangazi wawili pamoja na kweli wao si wafuasi wa chama chochote cha siasa nchini lakini baadhi ya Watanzania wanadhani ni wanachama wa Chadema kwa misimamo yao kuhusu demokrasia ya kweli nchini, upatikanaji wa katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi ili chaguzi zetu ziwe huru na za haki.

Chadema haujawahi kuwa mashabiki wa Kigogo bali ni Kigogo ndie aliyejifanya shabiki wa Chadema. Chadema watatumia platform yeyote ambayo wataona inafikisha ujumbe wake kwa wengi. Sasa hivi wafuasi wao wako kwa Maria ingawa yeye na Fatma si wanachama wao. Hii ni kwa sababu wakina Maria wanaongea ukweli wao bila uoga na hawasiti kutetea haki ya Chadema kufanya siasa bila kubughudhiwa.

Amandla...
 
Na hawa mashangazi wawili pamoja na kweli wao si wafuasi wa chama chochote cha siasa nchini lakini baadhi ya Watanzania wanadhani ni wanachama wa Chadema kwa misimamo yao kuhusu demokrasia ya kweli nchini, upatikanaji wa katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi ili chaguzi zetu ziwe huru na za haki.
Mtu yeyote akiwa na mawazo huru anahesabiwa kuwa ni mfuasi wa Chadema. Hawaoni kuwa kwa mtazamo huo wana jenga hoja kuwa huwezi kuwa na mawazo huru na ukawa mfuasi wa CCM.

Wale mashangazi walitofautiana mwanzo wa awamu hii lakini hawakublokiana. Wakati wote waliendelea na urafiki wao na kuheshimoana. Sasa wako page mmoja baada ya mmoja kutambua kuwa alikosea kwa kushangilia mapema.

Amandla...
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Majengo 90% yalijengwa na watanzania wote enzi za chama kushika hatamu. Nitajie uwanja wowote wa maana ccm iliojenga baada ya mfumo wa vyama vingi. Katazame majengo ya ccm iliyorithi toka mfumo wa chama kimoja yana hali gani. Mengi ndio majengo chakavu na yaliyochoka kuliko yote. Bisha tuweke mfano halisi.
Sasa kinachofanya chadema kisiwe na jengo la maana la ofisi ni kitu gani?
 
Mwanaharakati maarufu ambaye hajawahi kutiwa msukosuko ni nani? Godlisten Malisa ama? Kama ni yeye ni sawa. Huwa anajenga hoja nzuri katika maandiko yake na si rahisi kumkuta akiporomosha matusi. Malisa pia ana ukaribu sana na viongozi wengi wa serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. Na anaendesha kampeni nyingi zinazofanikiwa sana katika kusaidia watu mbalimbali wenye shida katika jamii.

Malisa mimi namuona kama ni hazina kubwa ya Chadema na taifa kwa ujumla labda aje apoteze mwelekeo huko mbele ya safari. Anazijua harakati. Ni msomi. Ana uwezo wa kutoa hoja - tena katika mawanda na muktadha sahihi.
 
Huyo kigogo na Chadema mbona ngoma haipandi huu mwezi wa pili sasa baada ya Kigogo kusuggest Chadema iunde jeshi na Lissu kuyaita mawazo yake ni ya kijinga.
Toka hiyo siku nilitokea kumdharau sana nikaacha kumfutilia
 
Kwanza Chahali ni mwanaccm ambaye hajawahi kuchukia ubaya wa ccm , yeye alimchukia Magufuli tu , halafu Chadema haijawahi kumshobokea Kigogo au Mange , bali watu hao wao ndio walioishobokea Chadema ili wajipatie wafuasi , ikumbukwe kwamba Chadema mara zote haijawahi kumshobokea mtu bali inamheshimu yeyote anayeipiga Spana ccm .

Kwa mfano leo huwezi kuilaumu Chadema kwa kumuunga mkono Halima Mdee wakati ule , maana aliipinga ccm kiukweli hasa , lakini baada ya Mdee kuingia ccm Chadema ikimpinga utailaumu ?
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom