Samahani
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 222
- 335
Wadau wa jukwaa, naomba kuliweka hili mbele yenu, huenda roho yangu ikapoa.
Uwezo wa maisha bado haujanipa kibali cha kujenga nyumba yangu, na hivyo naishi katika nyumba ya kupanga yenye vyumba viwili vya kulala. Kwa bahati mbaya, Mke wangu wa ndoa ambaye tumejaliwa naye mtoto mmoja tu sio mwajiriwa, hivyo yupo nyumbani akipambana na majukumu ya nyumbani pamoja na bishara ndogo ndogo ambazo kwakweli ni muhimu sana kwa ustawi wa familia yetu.
Lakini ajabu ni kuwa, mama huyu "Anataka muda wote awe na msaidizi wa kazi za ndani, yani housegirl, lakini hawezi kukaa naye hata kwa miezi miwili!!!". Pamoja na mimi mwenyewe kupendelea walau kuishi na ndugu ili kuwasaidia pia kimaisha, iwe ni wa kwangu au wa kwake, mara zote hataki, na anasisitiza kuwa anahitaji "House Girl"
Mara kadhaa nimeshamruhusu kwa shingo upande, lakini ajabu ni kuwa, hakai na wadada wa kazi kwa zaidi ya miezi miwili. Nashindwa kuelewa hasa tatizo ni nini, lakini kila baada ya mwezi mmoja na nusu au miwili, wadada hawa huamua kuondoka, na wapo ambao huniaga kuwa wanakwenda kusalimia kisha hawarudi, huku wengine wakaiamua kutoroka usiku wa manane au alfajiri sana!!
Mosi, Nashindwa kuelewa ni kwanini hasa mama watoto anahitaji kuwa na dada wa kazi ilhali nyumba yetu ni ndogo, yenye majukumu yanayoweza kusimamiwa na yeye peke yake na mimi kumsaidia pia kwa kuwa kila nitokapo kazini nina jukumu la kuungana naye kumalizia baadhi ya kazi za nyumbani.
Pili, ni hii adha ya wasichana wa kazi kuondoka mapema wakati ndio kwanza tunaanza kuwazoea. Mbaya zaidi, ni mara zote nalazimika kuwapigia ndugu wa mikoani wanisaidie kupata wafanyakazi. Hili la kupata adha ya kuwapigia ndugu, jamaa na marafiki zangu kila mwezi linanikwaza mno, na kwakweli nimeshakata shauri kuwa, SITAHANGAIKA TENA!!
Nisaidieni niwe na amani tena!!