Anaswa na Madawa ya Kulevya Uwanja wa Ndege Dar

Na mchina akamatwa uwanja wa ndege akiwa na shanga 58 zilizotengenezwa kwa pembe za ndovu apo ngoma droo
 
Invisible hapo ni kama kumpigia mbuzi gitaa maana huo mtandao hutausikia wala taarifa za alikotoa mzigo
kamanda nzowa ataizima kimya kimya na wala huo upelelezi hautasema mzigo ni wa nani wala ulitoka wapi na wapi madawa hayo yaliingilia
Halafu hawapati fundisho hawa watu ni kama kuna mtu anawahakikishia usalama wao kuwa nyie nendeni tuu hakuna shida

Swali ni wapi yanakopelekwa hayo madawa aliyoyanya huyo mwanamke.. nina wasiwasi kuwa yatarudishwa kwa mwenye mzigo halafu punda mwingine atamezeshwa hizi kete..aisee ni zaidi ya kichefuchefu na majanga
 
Hawakomi??yaani ndio kwanza wanazid kuongezeka??

Nakubaliana na wew Invisible,,huy punda abanwe aseme ukweli,,,tumechoka haswaa
 
Inavyoonyesha sasa hivi Tanzania ni supplier mkubwa wa madawa ya kulevya tofauti na zamani watu walikuwa wakikamatwa wanaingiza ila siku hizi wanakamatwa wakiyatoa

Swali

Je nani ameingiza mzigo wa ku supply duniani? Ameingiza kwa makontena au kwa shehena ya aina gani? Kuna utata mkubwa sana juu ya mzigo uliopo nchini
 
Baada ya kukamatwa story itakuwa uchunguz haujakamilika na miaka 5 badae mahakama yashindwa kumtia hatiani kwa kuwa ushahidi haujitoshelezi
 
Duuuu, haya mambo yamekuwa kawaida sasa ila jipya ni hilo la kudakwa Uwanja wa ndege wa Kambarage...

Na itaendelea kuwa kawaida kama serikali haitawatafuta wanaowadhamini na huwatumakwa hili lishatuaharibia kimataifa na huenda rais anapoenda nchi za watu wanampekua mara dufu
 
Aki i swear,drus lords ni "friimasoni"
Mbona wao hawajulikani,na wanaojuilikana hawakamatwi,???
 
[Mbona hili ni moja ya matatizo mengi tu yanayoisambaratisha nchi yetu. Na bahati mbaya sana hata viongozi tunaowategemea kutuongoza wameziba masikio na nta na macho yamejaa ukungu. Ni hawahawa wanafikia kuruhusu operstion za kikatili dhidi ya rai wema ili tu either kuwanyamazisha or kuonyesha kuwa upande fulani unahusika. ulimboka, kibanda na sasa huko temeke. ni ujinga. inakuwa kama vile sote ni wajinga na hatuwezi kupambanua mambo. niwakumbushe tu, jaribio la mapinduzi miaka ya 80 lilikuwa ni kutokana na ukweli kuwa Nyerere na serikali yake walishskuwa viziwi wa ukweli. Hali hii tayari tumeshaifikia. siku tukiona vifaru baarabarani or jamaa wa lugalo wako barabarani tusishangae kwa sababu nao ni binadamu pia. Tujiandae.]
 
Invisible unataka wahusika wote wa madawa ya kulevya wakamatwe, Tanzania si itabaki bila ya viongozi wa serikali
 
Wanngemuacha afu wawatonye wachina wamkamatie kwao...hapa mbona huyu ni raia huru tayari....
 
Uzuri wa hii nchi hizi kesi hupotea kama upepo tu na madawa anapewa punda mwingine anasafirisha hutakaa usikie yameenda wapi after hapo.
 
Hivi hawa ma-punda sijui wabebaji wanakuwaga wametolewa akili kwanza au ni nini? Sielewi na makelele yoooote ya huyu kakamatwa China sijui na yule wapi bado watu wanadiriki kutumika katika hii biashara?!!!!:confused2:..Hii ni zaidi ya Ze KOMEDI!
 
na akisha kunya hizo kete zinapelekwa wapi?.miaka kadhaa huko nyuma niliwahai kusikia uteketezwaji wa siraha haramu,ila miaka ya sasa sijawai kusikia uteketezwaji wa dawa za kulevya.
 
Mkuu Invisible huu mtandao tuachane nao tu, maji yamezidi unga. Pamoja na ushaidi wote huo, amini amna kesi hapo.

No seriousness katika hili jambo, kama mateja wanazurura kutwa wamelewa madawa ya kulevya, If there were any seriousness wangewakamata tu hao kwa kuanzia na wawaambie nani amewapa hayo madawa. So sad to Tz my Country, ila confused about the future of this country anyway. Mungu aingilie kati tu.
 
Hivi hawa ma-punda sijui wabebaji wanakuwaga wametolewa akili kwanza au ni nini? Sielewi na makelele yoooote ya huyu kakamatwa China sijui na yule wapi bado watu wanadiriki kutumika katika hii biashara?!!!!:confused2:..Hii ni zaidi ya Ze KOMEDI!

mnawakamata wa nini hakuna cha kuwafanya hapo, waache waende china na Hongkong wakasweke ndani, huko wako serious na huu mchezo. hii itasaidia kutokomeza ila mapambano TZ kwa dawa za kulevya kila siku ZE Comedy mpya
 
Tumuombe Mwakiembe,binti ahojiwe na video iwekwe hapa Jf ili na sisi tuwajue dealers.
 
Back
Top Bottom