Anaswa na Madawa ya Kulevya Uwanja wa Ndege Dar

Anaswa na Madawa ya Kulevya Uwanja wa Ndege Dar

hapa nadhani ni wakati muafaka wa kuwajua mapapa wa hii biashara.
 
sidhani kama huyu dada wa kongowe ndiye anaweza kusababisha cheni yote ya wauza unga ipatikane kwa kuwa sio yeye wa kwanza.hata hivyo nahisi kuna mtu kawachomea ushauri waanze na uwanja wa ndege kwa mtu wa kwanza kuhisi au kujua kuwa kuna shehena ya madawa.
 
Bandugu, hivi Tanzania tunalima haya madudu? mbona wapopo, wapakistani n.k wanakuja sana huku na sasa wachina pia? Je, kuna meli na motherboat ambazo ndo zinaingia haya madudu kwa wingi? je, Tanzania imegeuka kuwa 'hub' kuu ya kusafirisha haya madudu? tumeipiku Guinea Bissau katika hili?
 
Kazi hii inahaririwa kitaaluma sana na vinara wa biashara hii cyo hawafahamiki
Ila mtandao wake anahitajika mtu kauzu kuufumua kama makufuli o zito kama angekuwa na meno! Maana huhitaji semina kujua kuwa wanaoandaa mpango high secret service!
 
Mkuu unazungumza kama vile wauzaji wa madawa ya kulevya hawajulikani, Kwa taarifa yako mtandao wote unajulikana kutoka kwa ma druglords mpaka kwa wauzaji reja reja. Kwa nini hawakamatwi hilo nakuachia uwaulize jeshi la polisi.

Labda nikuulize tu kidogo, hujawahi kukutana na mlevi wa unga au teja, basi wale tu wanatosha kukufahamisha unga unauzwa wapi, follow the river to find the sea.

Hili ni swali zuri sana. Kama ulikuwa unafuatilia sakata la Kapuya na ubakaji wa mwanafunzi, Kapuya alitamka/aliandika kwenye SMS wazi wazi kwamba watoto wao wanauza madawa na hakuna wakuwakamata. Sasa kama wanaofanya hizo biashara ni watoto wa "ruling class" kina Kinjekitile na Riz1, unategemea nani hawakamate hao. Atakayethubutu, atakuwa hajipendi.

Tiba
 
aisee, mwanamke!! kashusha dawa 63!!!! hivi anameza na nini, maji juice au kavu kavu? wanawake sisi kumbe wengine ni hatari sana jamani, yaani huyo alikuwa tayari kwa lolote hata kufa, ni vema mtandao wake wote ukajulikana na kutajwa kwa watanzania ili hata majirani huko kongowe na kwingineko wawajue na kuwa mbali nao
 
Kwa nini wasingemuacha akakamatiwe China ili ashitakiwe kwa sheria za huko? Kwa kukamatwa Dar, hakuna kesi hapo, watasema sio madawa ya kulevya bali ni malighafi ya kutengenezea madawa ya kulevya!
 
Sema hizo kete anazitolea juu ya gazeti lililotandikwa kwenye ofisi za uwanja wa ndege! Akizitolea chooni watazipata je?
 
Ni vigumu sana dawa za kulevya na ujangili kuisha kwani wahalifu mara wanapokamatwa hufichwa mbele ya jamii sura zao, majina yao! hiki ni kikwazo kikubwa sana kwani jamii ingejua naamini wapo wasamalia wema ambao wangetoa ushirikiano kusaidia kuharakisha juhudi za utokomezaji wa shughuli zote hizi haram.
 
Kwa nini wasingemuacha akakamatiwe China ili ashitakiwe kwa sheria za huko? Kwa kukamatwa Dar, hakuna kesi hapo, watasema sio madawa ya kulevya bali ni malighafi ya kutengenezea madawa ya kulevya!

Na malighafi hiyo mbebaji ana maamuzi ya kuchagua anayabebea wapi..tumboni au kwenye kikapu!

Kwa kweli nchi yetu 'haijatamani' bado kupambana na haya maunga...
 
Tatizo wahusika wanajulikana ila hakuna wa kuwakamata. Kazi kudili na vifaranga tu!
 
hakika hiz habari kuhusu madawa ya kulevya ingekua nguo yangu ningemvalisha mnyama asie na utashi coz kama viongoz wa nchi wako sirous haya yanaishia wap?
 
Kwa hali ilipofikia tanzania,kupambana na madawa ya kulevya ni sawa na kupambana usikione kivuli chako.
 
Nyonga kabisa wanatia aibu taifa kila leo. Tena wavuliwe nguo wakati wachina wanawanyonga na iwe hadharani na irushwe TBC labda mapunda yatapata adabu. I wish angedakwa huko afu iwe hivi.
 
tamaa za mabenzi na mavogue ndizo zimetufikisha hapa huyu angenyongwa tu.
 
Huu sasa ni ujinga..Napendekeza sheria ya kunyonga ..kwa hii mijitu inayotaka utajiri wa haraka.
 
CCM wangependa tuijadili CDM na kusambaratika kwake na si hoja muhimu kama hizi kwasababu baadhi ya viongozi ni wahusika wakuu.
 
Back
Top Bottom