Ananitega

Mwenzenu nimeo na nimebahatika kupata watoto 4. Nina kakazi kangu, kwa ujumla hap uswahilini mie natesa. Jirani yetu kuna dada flani tena shoga wa wife ameniganda ile mbaya. Kwa ujumla yuko njema. Hapa nilipo sielewi nifanyeje na tangu nioe sijawahi uza timu nje. Naombeni ushauri.
we Lutala vipi? wataka kusema huyo jirani anamzidi mkeo?
hebu tulia na mkeo bana, achana na hayo mawazo ya kishetani eboh!
huelewi ufanyeje?!!!! piga magoti mwombe Mungu akuepushe na hilo pepo la usaliti katika ndoa, pia acha mazoea na huyo dada coz nahisi unamchekeachekea ndo maana kakuganda.
Mheshimu mkeo Lutala.
 
Achana na huyo hana lolote anataka kukuchuna tu shauri yako..kwani haoni wanaume wengine mpaka akugande wewe?
 
wanaume huwa mnashangaza kwa kweli..................hivi kweli huwezi kumwambia mwanamke NO akakuelewa? au ndio unakuwa ushataka tu kutekenyana na shoga wa mkeo unatafuta sababu tu?
 
Mwenzenu nimeo na nimebahatika kupata watoto 4. Nina kakazi kangu, kwa ujumla hap uswahilini mie natesa. Jirani yetu kuna dada flani tena shoga wa wife ameniganda ile mbaya. Kwa ujumla yuko njema. Hapa nilipo sielewi nifanyeje na tangu nioe sijawahi uza timu nje. Naombeni ushauri.
hapana mkuu hapo miye nimegoma labda ulete hoja nyingine kabisa
sema hapo umejitega wewe mwenyewe kwa tamaa tu za kimaumbile, kwani huyo dada
anatumia mtego wa kitu gani ambacho mkeo hana?

akili yako tu ndiyo imezidiwa na tamaa za mwili wako, na uroho wa uzinifu wala hakuna jipya hapo
usisingizie kutegwa nyie wote na huyo dada mmewakiana tamaa tu, wala hakuna jipya

kama umeoa na unaishi na mkeo na mna mtoto, hayo mambao ya nini? kama ulivamia tu ndoa bila kujua misingi na miiko ya ndoa umeumia, tambua kuwa mtu kutoka nje ya ndoa ni kujitenda dhambi yeye mwenyewe, mkewe na kiisha Mungu, malizeni ujinga wenu huko nje na mkiisha ingia katika ndoa muwe watulivu na wastahimilifu huku mkishindana na tamaa za miili yenu
 
na ukimwi je??usikute anataka kukusakizia we haya!!!tena shoga wa mkeo huyo ana lake jambo,je MKEO AKITEMBEA NA RAFIKIYO UTAFURAHI WEWE,MAANA MUOSHA HUOSHWA,MUOGOPE MUNGU ,
 
Tena inavyoonekana hana huruma huyo dada hafai kabisa,maisha yenyewe haya,na watoto unao 4,bado huyo mwanamke haoni huruma,mimi namwita muuaji kabisa au mbomoaji,hafurahii unavyoishi na familia yako,utakuja kutuambia hapa.
 
Mwenzenu nimeo na nimebahatika kupata watoto 4. Nina kakazi kangu, kwa ujumla hap uswahilini mie natesa. Jirani yetu kuna dada flani tena shoga wa wife ameniganda ile mbaya. Kwa ujumla yuko njema. Hapa nilipo sielewi nifanyeje na tangu nioe sijawahi uza timu nje. Naombeni ushauri.

acha kututega bana,...
ushauriwe 'kujilipua' halafu ndoa yako ikiyumba uje utulaumu?

Jibu unalo.
Achana nae huyo, huenda yeye na Mkeo wanakutega vile vile.
 
Kama jamaa ana soluhisho kuwa kaamua kumlipua kwanini alikuja kuomba ushauri hiki ni kichefu kichefu na utakuja juta kwa uwamuzi huu na mtaa utauhama wandugu ngono sio chakula kuwa ukiacha kufanya utakufa njaa mheshimu mkeo na amini kuwa mkeo ndio mwanamke mzuuri kuliko wote duniani kwani ni wewe ndio uliamu kuishi naye
mpe heshima yake anayostahili kwani kukubali kujitoa kuishi na wewe ni tunu ambayo inatakiwa uienzi mthamini na jali thamani ya mkeo

Sikuvutiwa kuchangia mada hii lkn imebidi tu kuchangia kitendo cha kumuona huyu mwanamke ni mzuri kuliko mkeo hili ni kosa na inaonyesha jinsi gani usivyotulia i mean utuilivu ziro better usingeileta mada hii humtendei mkeo uungwana hakuna aliyekulizamisha umuoe yeye ni wewe mwenyewe. Kumbuka ukisambaratisha familia yako kwa kwenda nje ya ndoa unakaribisha mateso hasa ikitokea mkiachana nyumba yako itakuwa haina thamanii na amani tena kwani hautopata mwanamke ambaye ataweza kuwalea watoto wako kama mama yao. usijeshangaa hata hiyo kazi yako ikayumba kumbuka labda uliipata hiyo kazi kwa sababu ya mkeo. na kuna laana itakupata kama mkeo atakuwa kwenye manung'uniko au ikitokea mmeachana. Na ndio maana kabla ya kulala ni vizuri msameheani kama mmekoseana hii hudumisha upendo.

Samahani kwa kutumia lugha kali lkn hii yote ni kwa sababu ya uchungu nilionao kama Mwanaume ninayejali

Kumbuka Tofauti kati ya mbwa na BInadamu ni kuwa binadamu unaweza kufikiri na kujua baya na zuri tujiepushe kufanya mabaya yatakayoudhi mpenzi wako mfanye mpenzi wako kuwa bestfriend wako ungeeni kirafiki zaidi mnapokuwa na matatizo au na furaha. wanawake hawahitaji mambo makubwa sana zaidi ya faraja na kujisikia amani akiwa na wewe kama sisi tunavyojisikia tukiwa nao. Kumbuka usithubutu kumchukizamkeo kwani maisha yako yako mikononi mwake mtu anayeweza kukuandalia chakula ni hatari mno katika maisha yako kwani anaweza kukuua wakati wowote ule lakini hili hatulifikirii wewe kila siku unampiga tu na kufanya ajisikie vibaya lakini ashukuruwe mungu kwa kuwafanya wanawake kuwa na moyo mzuri wa mapenzi kwa waume zao.

Mthamini mkeo kama ambavyo anakuthamini wewe.
 
Piga kitu mzee heshima mbele, ila usisahau familia maana mmmh............................................
 
isije ikawa katumwa na mkeo:eek2:,vinginevyo dumisa mila on your own risk tena kuweka heshima fumua ndogo vibaya vibaya mbele mwambie mkeo anatosha,kisha baada ya hapo funga vioo kabisa tena weka na tinted kabisa lakini ukinogewa shauri yako.:A S-danger:
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom