Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,347
- 26,153
Ukweli lazima usemwe. Kila chama cha siasa kina sera, itikadi na Imani yake. Wanachama hujiunga kwa kuvutiwa na kuwa tayari kufuata mambo hayo. Kuhama chama ni kutotaka tena kufuata mambo hayo. Kisiasa, kibinaadamu na kijamii, kuhama chama ni haki ya kila mwanachama na mwananchi wa nchi hii. Lakini, kuhama chama hakupaswi kutanguliwa na 'vishekesho vya kisiasa'.
Kitendo cha Mbunge wa Moshi Vijijini, Mhe Komu kutangaza kuwa atahama CHADEMA na kujiunga na NCCR-Mageuzi baada ya Bunge kuvunjwa ni kichekesho cha wazi cha kisiasa kinachoonyeshwa na mwanasiasa huyo nguli wa siasa za kiupinzani na kimapinduzi nchini. Iko wazi kuwa ameshaamua kuhama CHADEMA. Hana tena chochote na cha namna yoyote na CHADEMA. Hana hata cha kungoja.
Kichekesho cha Komu kina sura mbili. Moja, anataka ajadiliwe na afukuzwe CHADEMA. Ni kwakuwa ameshaamua kukihama chama hicho lakini bado 'anang'ang'ania' kuwemo. Atafaidikaje? Mbili, Komu ataendeleaje kuwa Mbunge wa chama ambacho tayari ameshatangaza kukitoka na haamini chochote tena cha chama hicho? Mbunge Komu aache kuendelea kutuchekesha wafuatiliaji wa siasa hapa nchini.
Uamuzi utakuwa umesoma ramani nzima yakiwemo ya mafao yake ya kibunge. Kama hakufanya hivyo na ana hofu ya kuyapoteza, atakuwa hajaamua vyema.