Anachokifanya Komu ni 'kichekesho cha kisiasa'

Anachokifanya Komu ni 'kichekesho cha kisiasa'

Nashindwa kujua Komu anatafuta nini, kwanza katikati ya CORONA na ambapo wanasiasa wote kama sio wengi sana 99.9% wanatangaza mshikamano kwa kipindi hiki, anakuja kuleta siasa za kugawana fito. Muda sio Mwafaka, pia anasema hajawa tayari kuahama hadi bunge livunjwa, kwanini hakusubiria bunge livunjwe aseme hayo? ANATAKA KUHAMISHA KUTOKA KUPAMBANA NA CORONA iwe KOMU KOMU KOMU ili iweje? Je anataka CDM imsaidie kubaki mwanachama kwa siku hizi mpaka bunge livunjwa ili CDM ifaidike na nini kama CHAMA?

Uamuzi:
Vile anataka afukuzwe ili apate kiki, CDM imfukuze haraka ili kuondoa dhana ya kwamba inaweka wabinge ili kula hela ya taifa bila maana yoyote, maana iwapo kuna maana kubakia muda huu basi angekaa kimya amalizie maana hiyo.

lakni lengo linguine ni kugombanisha CDM na NCCR, sasa ni wakati wa MBATIA na MBOWE kuonesha wamekomaa kisiasa na wako kuongoza nchi, Nadhani NCCR watoke kulaani anachokifanya KOMU, wakti mwingine iwapo mtu analengo la kuvuruga basi akataliwe kuwa chama hakiwezi kuwa naye maana amekwaza wanachama wa NCCR pia kujaribu kuonesha NCCR ni kichaka, Pia Chadema ifukuze tu mtu huyu kwa faida ya TAIFA
 
Wewe Yohana kwani ni miezi mingapi imebaki bunge livunjwe? Wakati mwingine kuna gharama kubwa tu unatakiwa kulipa kulinda heshima yako.
CDM wakiogopa kumtimua Komu eti kwa sababu ya ruzuku huko ni kujidhdlilisha kwa kiwango cha juu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Komu ameshaaga kuwa anaenda Nccr mageuzi na kinachombakiza bungeni ni wapiga kura wa Moshi vijijini siyo Chadema.

Maana yake ni kuwa Anthony Komu anawasubiri Chadema wakachukue kadi yao kama wanaihitaji.

Mbowe hawezi kumtimua mbunge hilo nakuhakikishia, alikuwepo Shibuda bhana alikuwa anainanga Chadema bungeni na yeye akiwa mbunge wake lakini hawakuthubutu kumtimua kwa sababu za kimapato!
 
Dawa nikumvua Uanachama hili akose ,posho za Ubunge.
Hata akivuliwa uanachama ataenda mahakamani kuweka injunction halafu spika ataendelea kumlinda hadi amalize muda wake. Mtindo huu haujaanza leo, kumbukeni ya Hamad Rashid alipofukuzwa CUF, spika alikataa kutambua uamuzi huo hadi bunge lile lilipomaliza muda wake.
 
Nampongeza Mh. Komu kwa kutumia haki yake ya kikatiba na pia ukomavu aliouonyesha kwa kusema hadharani bila unafiki juu ya msimamo wake wa kisiasa. Sipendi kusema lolote juu ya sababu alizotoa za kujiondoa Chadema ILA naomba niseme machache juu ya jimbo la Moshi Vijijini.

Kwa bahati nilibahatika kuwepo sehemu kadhaa za Jimbo husika kama miaka ±20 ambapo nilifurahishwa sana na mandhari niliyoyakuta huko. Kipindi hicho bado kahawa zilikuwapo kwa kiasi chake na kwa upande wa ndizi nazo hazikuwa haba kiasi cha kufanya mlo wa “Machalari” kwa kitimoto kuwa mlo wa “mtu wa kawaida”. Kipindi hicho safari za kutembelea maeneo kama Kolila, Tsuduni, Kimochi, Mdawi, Kameti, Sango, Shia, Mkonga, Mahero (mashambani) nk hazikuwa za shida sana kutokana na ubora wa wastani wa barabara (Changarawe) ijapokuwa bodaboda hazikuwepo kabisa. Kutokana na hali ya hewa ya baridi kipindi hicho ungaliweza kuzitembea sehemu kadhaa kwa gari au hata kwa miguu bila kuchoka.

Kutokana na mambo ya kijamii mwaka 2017, 2018 na 2019 nilipata nafasi ya kuyatembelea tena baadhi ya maeneo tajwa habo juu kwa kupanda kwa gari barabara ya Sango na Shia kuelekea huko Kihochi na nilichokiona kilinifanya nitafakari kwa mara ya kwanza kuwaza kugombea “Ubunge wa Moshi Vijijini”. Ijapo natambua watu wa huko wataniita “Chasaka” ambacho ni ukweli sawia ILA nina uhakika nikigombea Ubunge kupitia “Chama changu” yaani CCM kwa agenda ya kuboresha miundo mbinu ya barabara, maji na Shule Kongwe nitashinda kwa kishindo (Naomba nisipigwe mawe). Hebu niambie kwanini wenyeji SHIA wasinipe KURA ZA NDIYO ilihali barabara yao imeharibika kiasi kwamba hakuna mwenye gari la abiria (Dala dala) anaethubutu kupitisha gari yake katika njia ya kijiji chao.

Mheshimiwa KOMU hebu niambie niliyoyaona katika hivyo vijiji vichache ni kwamba mimi nina “Makengeza” au hayo ndio maendeleo uliyowaahidi wapiga kura wako? Mh. KOMU hebu niambie niliyoyaona huko ni matokeo ya kususiwa na “Chama changu) CCM kwa vile wewe ni Mbunge wa Upinzani? Mh. KOMU kama utanithibitishia bila mashaka kama “Chama Changu” CCM kimechangia nilichokiona katika sehemu hii ndogo ya Jimbo lako basi nitawaomba wadau kama Mzee Mwanakijiji na na Mkuu Pascal Mayalla nk tuanze maombi ya kufunga na kuomba kutubu kwa niaba ya “Chama Chetu”.

Mh. KOMU kama kudorora kwa maendeleo ya hiyo sehemu ndogo ya Jimbo lako hakujasababishwa “Figisu “ za CCM basi nakushauri ukatubu kwa kuwapotezea “Neglecting” wapiga kura wako na ninakushauri usigombee tena Ubunge kupitia chama chote kile. Ninakuhakishia nikisikia umekuja kwenye “Chama Chetu” CCM na una nia kugombea tena Ubunge , Sisi akina “Chasaka” tutamtafuta mwanachama “Mwadilifu” wa asili ya Moshi vijijini ili akapambane na wewe nami nitakuwa mmowapo wa wapiga Zomari wake.

Mh. KOMU ukitaka kuombewa sala ya toba, usisubiri hadi Bunge livunjwe.
 
Na hayo umeyaona baada ya kusema atatoka chadema?

Tukiwaambia humu kwamba wabunge wa chadema waoneshe mfano kwenye majimbo yao walichofanya, mnakuja hapa mkizungusha mikono kwamba chadema haikusanyi kodi.

Ni upuuzi mtupu bora ccm iendelee kutawala tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Iendelee kutawala tuendelee kuishi kwenye umaskin
 
Ukweli lazima usemwe. Kila chama cha siasa kina sera, itikadi na Imani yake. Wanachama hujiunga kwa kuvutiwa na kuwa tayari kufuata mambo hayo. Kuhama chama ni kutotaka tena kufuata mambo hayo. Kisiasa, kibinaadamu na kijamii, kuhama chama ni haki ya kila mwanachama na mwananchi wa nchi hii. Lakini, kuhama chama hakupaswi kutanguliwa na 'vishekesho vya kisiasa'.

Kitendo cha Mbunge wa Moshi Vijijini, Mhe Komu kutangaza kuwa atahama CHADEMA na kujiunga na NCCR-Mageuzi baada ya Bunge kuvunjwa ni kichekesho cha wazi cha kisiasa kinachoonyeshwa na mwanasiasa huyo nguli wa siasa za kiupinzani na kimapinduzi nchini. Iko wazi kuwa ameshaamua kuhama CHADEMA. Hana tena chochote na cha namna yoyote na CHADEMA. Hana hata cha kungoja.

Kichekesho cha Komu kina sura mbili. Moja, anataka ajadiliwe na afukuzwe CHADEMA. Ni kwakuwa ameshaamua kukihama chama hicho lakini bado 'anang'ang'ania' kuwemo. Atafaidikaje? Mbili, Komu ataendeleaje kuwa Mbunge wa chama ambacho tayari ameshatangaza kukitoka na haamini chochote tena cha chama hicho? Mbunge Komu aache kuendelea kutuchekesha wafuatiliaji wa siasa hapa nchini.

Uamuzi utakuwa umesoma ramani nzima yakiwemo ya mafao yake ya kibunge. Kama hakufanya hivyo na ana hofu ya kuyapoteza, atakuwa hajaamua vyema.
Kichekesho kinaanzia wapi?

Yeye ameamua kuitumia haki yake kikatiba.
Na pia amekwenda mbele zaidi kwa kuwawahi ili msimtimuwe kwenye chama, ndio maana kawawekea kigingi.

Sioni mahali alipochekesha,bali ameonyesha njia mpya ya kufanya siasa za upinzani nchini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sababu wengi hatuelewi kilicho nyuma ya pazia ndo maana tunaona ni kichekesho cha kisiasa.. Hii ni move iliyotengenezwa Lumumba pale.. Kwa vyovyote Komu ameshaahidiwa kiinua mgongo chake chote, na marupurupu mengine, pamoja na kulipwa ada ya kutoka Chadema, iwapo atatimuliwa toka kwenye Chama.. Kwa hiyo hesabu iliyopigwa ni kwa Chadema Kupanick na kumfukuza, ili chama kipate a negative publicity..

Dawa hapo ni kwa uongozi wa Chadema kumuacha tu, kama alivyoachwa Shibuda wakati ulee..
 
Mbona CDM mnatapatapa???? Ni maamuzi yake kisheria....... Nyie mmeshindwa kuwa kitu kimoja ndani, acheni nyumba iendelee kubomoka maana mmeshindwa kuziba UFA, tulieni hivyo hivyooooo....,.
 
Kwa sababu wengi hatuelewi kilicho nyuma ya pazia ndo maana tunaona ni kichekesho cha kisiasa.. Hii ni move iliyotengenezwa Lumumba pale.. Kwa vyovyote Komu ameshaahidiwa kiinua mgongo chake chote, na marupurupu mengine, pamoja na kulipwa ada ya kutoka Chadema, iwapo atatimuliwa toka kwenye Chama.. Kwa hiyo hesabu iliyopigwa ni kwa Chadema Kupanick na kumfukuza, ili chama kipate a negative publicity..

Dawa hapo ni kwa uongozi wa Chadema kumuacha tu, kama alivyoachwa Shibuda wakati ulee..
Umenena ni sawa na Mke mleta chokochoko ili apewe talaka baada ya kupata bwana mpya
 
Back
Top Bottom