Anachokifanya Komu ni 'kichekesho cha kisiasa'

Ukweli lazima usemwe. Kila chama cha siasa kina sera, itikadi na Imani yake. Wanachama hujiunga kwa kuvutiwa na kuwa tayari kufuata mambo hayo. Kuhama chama ni kutotaka tena kufuata mambo hayo. Kisiasa, kibinaadamu na kijamii, kuhama chama ni haki ya kila mwanachama na mwananchi wa nchi hii. Lakini, kuhama chama hakupaswi kutanguliwa na 'vishekesho vya kisiasa'.

Kitendo cha Mbunge wa Moshi Vijijini, Mhe Komu kutangaza kuwa atahama CHADEMA na kujiunga na NCCR-Mageuzi baada ya Bunge kuvunjwa ni kichekesho cha wazi cha kisiasa kinachoonyeshwa na mwanasiasa huyo nguli wa siasa za kiupinzani na kimapinduzi nchini. Iko wazi kuwa ameshaamua kuhama CHADEMA. Hana tena chochote na cha namna yoyote na CHADEMA. Hana hata cha kungoja.

Kichekesho cha Komu kina sura mbili. Moja, anataka ajadiliwe na afukuzwe CHADEMA. Ni kwakuwa ameshaamua kukihama chama hicho lakini bado 'anang'ang'ania' kuwemo. Atafaidikaje? Mbili, Komu ataendeleaje kuwa Mbunge wa chama ambacho tayari ameshatangaza kukitoka na haamini chochote tena cha chama hicho? Mbunge Komu aache kuendelea kutuchekesha wafuatiliaji wa siasa hapa nchini.

Uamuzi utakuwa umesoma ramani nzima yakiwemo ya mafao yake ya kibunge. Kama hakufanya hivyo na ana hofu ya kuyapoteza, atakuwa hajaamua vyema.
Mimi siamini kama Komu bado atakuwa na akili timamu. Mwenye akili timamu hawezi kunena/kutenda hivyo. Walio karibu naye wamchunguze.

Si ajabu kuhama chama. Cha ajabu ni mtu kusema kwamba nitaendelea kuwepo kwenye chama hikihiki. Halafu wakati fulani nitaondoka!
 
Ukweli lazima usemwe. Kila chama cha siasa kina sera, itikadi na Imani yake. Wanachama hujiunga kwa kuvutiwa na kuwa tayari kufuata mambo hayo. Kuhama chama ni kutotaka tena kufuata mambo hayo. Kisiasa, kibinaadamu na kijamii, kuhama chama ni haki ya kila mwanachama na mwananchi wa nchi hii. Lakini, kuhama chama hakupaswi kutanguliwa na 'vishekesho vya kisiasa'.

Kitendo cha Mbunge wa Moshi Vijijini, Mhe Komu kutangaza kuwa atahama CHADEMA na kujiunga na NCCR-Mageuzi baada ya Bunge kuvunjwa ni kichekesho cha wazi cha kisiasa kinachoonyeshwa na mwanasiasa huyo nguli wa siasa za kiupinzani na kimapinduzi nchini. Iko wazi kuwa ameshaamua kuhama CHADEMA. Hana tena chochote na cha namna yoyote na CHADEMA. Hana hata cha kungoja.

Kichekesho cha Komu kina sura mbili. Moja, anataka ajadiliwe na afukuzwe CHADEMA. Ni kwakuwa ameshaamua kukihama chama hicho lakini bado 'anang'ang'ania' kuwemo. Atafaidikaje? Mbili, Komu ataendeleaje kuwa Mbunge wa chama ambacho tayari ameshatangaza kukitoka na haamini chochote tena cha chama hicho? Mbunge Komu aache kuendelea kutuchekesha wafuatiliaji wa siasa hapa nchini.

Uamuzi utakuwa umesoma ramani nzima yakiwemo ya mafao yake ya kibunge. Kama hakufanya hivyo na ana hofu ya kuyapoteza, atakuwa hajaamua vyema.

Kwa hiyo kwa sasa atakuwa Mbunge wa NCCR Mageuzi kwa tiketi ya CHADEMA???
 
lengo la komu ni kutaka afukuzwe than yeye aende mahakamani! mahakama inaposikiliza anaendelea kupiga hela
 
Ametoa notice, ukiwa na cheo cha uongozi kwenye ajira, sii inatakiwa utoe notice ya miezi 3 au 6. Pili huyu ni mchaga asilia, hawezi achia hata senti tano, huwa kwao wanakamua mawe mpaka yanatoa maji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom