Amtwanga talaka mkewe

Pengo

JF-Expert Member
Oct 15, 2009
579
10
Ndoa ya aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kwa takribani miaka 20, Amani Mwenegoha (55), imeingia kwenye skendo nzito baada ya mtumishi huyo wa dini kudaiwa ‘kumtwanga' talaka mkewe kwa kiapo cha mahakamani.

Uwazi lilipata skendo hiyo iliyokuwa nyuma ya pazia kupitia vyanzo vyake makini na kuamua kuichimba kisha kubaini undani wake.

Baada ya Uwazi kuthibitishiwa uwepo wa habari hiyo inayoshtua kwa kiongozi wa dini kuasi maandiko matakatifu, waandishi wake mahiri waliingia mtaani na mtu wa kwanza kumnasa alikuwa ni mke wa mtumishi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mwanuni Mwangile (49) (pichani), ambaye alifunua mengi ya usichokijua juu ya ndoa hiyo.

Katika mahojiano maalum na gazeti hili jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mwangile aliweka kweupe kwa kudai kwamba, mumewe huyo alimtelekeza miaka sita iliyopita huku wakiwa wamejaliwa watoto watatu ndani ya ndoa yao takatifu iliyofungwa mwaka 1988 katika Kanisa Kuu la KKKT, Azania Front, Dar.

Mwangile aliyeonekana kutojua hatma ya maisha yake hasa pale anapoona kuwa yuko kama mtu ambaye hajawahi kuolewa, alisema kuwa katika kipindi hicho chote haamini kama ameachika na kwake ilikuwa ndoto ya alinacha.

Mama huyo aliyeonekana kulilia penzi la mumewe aliendelea kusema kwamba, amekuwa akiishi maisha ya kubahatisha hasa linapokuja suala la kazi ambapo ameweka makazi yake wilayani Kisarawe, mkoani Pwani akiwa mfanyakazi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Aidha, mke huyo wa zamani wa Mwenegoha ambaye kitaaluma ni mwalimu wa muda mrefu, alisema kuwa tangu waoane na Mwenegoha mwaka 1988, wana miaka 22 kabla ya kukutwa na fedheha ya talaka hivi karibuni.

Huku akiwa na majonzi makubwa alisema: "Nilisikitishwa sana na tabia ya mume wangu alipoanza ishara za kutokunitaka kabisa na hata kufikia hatua ya kutofika nyumbani tulipokuwa tukiishi, Mtaa wa Wazuki, Masaki, Dar.

"Nilihisi mume wangu ana kimada aliyekuwa akimzuzua kwani hakuwa hivyo."
Akisimulia kwa undani wakati wakiwa Arusha kikazi Mwenegoha akiwa Kiongozi wa KKKT, Mwangile alisema kuwa walikuwa na maisha mazuri kiasi kwamba: "Familia kadhaa zilikuwa zikitamani maisha yetu," alisema mama huyo.

Alisema kwamba, baada ya mambo kuharibika katika Kanisa la KKKT, Arusha, Mwenegoha alirejea Dar kwa lengo la kuandaa makazi mapya lakini chakushangaza mawasiliano kati yao yalikatika ghafla.

"Kuona hali hiyo, nikaamua kufungasha virago na watoto kuja Dar kwa mume wangu aliyekuwa akiishi Masaki lakini sikupokelewa." Alidai Mwangile na kumalizia kwamba:
"Niliamua kwenda kwa ndugu zangu Kisarawe na katika kipindi hicho ndipo tulipovurugana na mume wangu akaniacha."

Kwa upande wake, Mwenegoha alikiri ‘kumtwanga' talaka mkewe huku sababu kubwa akiitaja kuwa mama watoto wake alikuwa akimnyima usingizi usiku.

"Alikuwa akiamka usiku wa manane na kuanza kusali bila sababu wala kuwepo kwa tatizo lolote. Mimi kama dini naijua sana na kila kitu kina wakati wake, kuna wakati wa kula na hata wakati wa ibada," alisema Mwenegoha na kuongeza:

"Mimi nilimshindwa mwanamke yule na tatizo hili lilikuwa ni la muda mrefu sana, nilichelewa tu kuchukuwa hatua madhubuti lakini baadaye niliamua kumpiga chini."
Mwenegoha alisema kuwa alichukua hatua ya kwenda mahakamani kwa ajili ya kiapo cha mahakama cha kutengana na mkewe ili kila mtu afanyanye shughuli na maisha yake.

Kuhusu watoto, Katibu huyo wa zamani wa KKKT alisema kwamba, anaendelea kuwalea kwa kuwa ni wanawe wa ndoa.
"Nimetengana na mke wangu na si watoto, huduma wanapata kama kawaida ikiwa ni pamoja na haki yao ya elimu," alimalizia Mwenegoha.

SOURCE:-GLOBAL PUBLISHERS
 
Ndoa ya aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kwa takribani miaka 20, Amani Mwenegoha (55), imeingia kwenye skendo nzito baada ya mtumishi huyo wa dini kudaiwa ‘kumtwanga' talaka mkewe kwa kiapo cha mahakamani.

Uwazi lilipata skendo hiyo iliyokuwa nyuma ya pazia kupitia vyanzo vyake makini na kuamua kuichimba kisha kubaini undani wake.

Baada ya Uwazi kuthibitishiwa uwepo wa habari hiyo inayoshtua kwa kiongozi wa dini kuasi maandiko matakatifu, waandishi wake mahiri waliingia mtaani na mtu wa kwanza kumnasa alikuwa ni mke wa mtumishi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mwanuni Mwangile (49) (pichani), ambaye alifunua mengi ya usichokijua juu ya ndoa hiyo.

Katika mahojiano maalum na gazeti hili jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mwangile aliweka kweupe kwa kudai kwamba, mumewe huyo alimtelekeza miaka sita iliyopita huku wakiwa wamejaliwa watoto watatu ndani ya ndoa yao takatifu iliyofungwa mwaka 1988 katika Kanisa Kuu la KKKT, Azania Front, Dar.

Mwangile aliyeonekana kutojua hatma ya maisha yake hasa pale anapoona kuwa yuko kama mtu ambaye hajawahi kuolewa, alisema kuwa katika kipindi hicho chote haamini kama ameachika na kwake ilikuwa ndoto ya alinacha.

Mama huyo aliyeonekana kulilia penzi la mumewe aliendelea kusema kwamba, amekuwa akiishi maisha ya kubahatisha hasa linapokuja suala la kazi ambapo ameweka makazi yake wilayani Kisarawe, mkoani Pwani akiwa mfanyakazi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Aidha, mke huyo wa zamani wa Mwenegoha ambaye kitaaluma ni mwalimu wa muda mrefu, alisema kuwa tangu waoane na Mwenegoha mwaka 1988, wana miaka 22 kabla ya kukutwa na fedheha ya talaka hivi karibuni.

Huku akiwa na majonzi makubwa alisema: "Nilisikitishwa sana na tabia ya mume wangu alipoanza ishara za kutokunitaka kabisa na hata kufikia hatua ya kutofika nyumbani tulipokuwa tukiishi, Mtaa wa Wazuki, Masaki, Dar.

"Nilihisi mume wangu ana kimada aliyekuwa akimzuzua kwani hakuwa hivyo."
Akisimulia kwa undani wakati wakiwa Arusha kikazi Mwenegoha akiwa Kiongozi wa KKKT, Mwangile alisema kuwa walikuwa na maisha mazuri kiasi kwamba: "Familia kadhaa zilikuwa zikitamani maisha yetu," alisema mama huyo. Alisema kwamba, baada ya mambo kuharibika katika Kanisa la KKKT, Arusha, Mwenegoha alirejea Dar kwa lengo la kuandaa makazi mapya lakini chakushangaza mawasiliano kati yao yalikatika ghafla.

"Kuona hali hiyo, nikaamua kufungasha virago na watoto kuja Dar kwa mume wangu aliyekuwa akiishi Masaki lakini sikupokelewa." Alidai Mwangile na kumalizia kwamba:

"Niliamua kwenda kwa ndugu zangu Kisarawe na katika kipindi hicho ndipo tulipovurugana na mume wangu akaniacha."

Kwa upande wake, Mwenegoha alikiri ‘kumtwanga' talaka mkewe huku sababu kubwa akiitaja kuwa mama watoto wake alikuwa akimnyima usingizi usiku.

"Alikuwa akiamka usiku wa manane na kuanza kusali bila sababu wala kuwepo kwa tatizo lolote. Mimi kama dini naijua sana na kila kitu kina wakati wake, kuna wakati wa kula na hata wakati wa ibada," alisema Mwenegoha na kuongeza:

"Mimi nilimshindwa mwanamke yule na tatizo hili lilikuwa ni la muda mrefu sana, nilichelewa tu kuchukuwa hatua madhubuti lakini baadaye niliamua kumpiga chini."

Mwenegoha alisema kuwa alichukua hatua ya kwenda mahakamani kwa ajili ya kiapo cha mahakama cha kutengana na mkewe ili kila mtu afanyanye shughuli na maisha yake.

Kuhusu watoto, Katibu huyo wa zamani wa KKKT alisema kwamba, anaendelea kuwalea kwa kuwa ni wanawe wa ndoa.
"Nimetengana na mke wangu na si watoto, huduma wanapata kama kawaida ikiwa ni pamoja na haki yao ya elimu," alimalizia Mwenegoha.

SOURCE:-GLOBAL PUBLISHERS

THIS IS CLASSIC!
RED - Hiki ndicho hasa kisa na mkasa.
Purple - kisingizio kilichokosa maana! Mwanaume wa KKKT utamwacha mke kwa sababu anasali sana?! WATU WENGINE BANA AHHH!!
 
[QUOTE
Purple - kisingizio kilichokosa maana! Mwanaume wa KKKT utamwacha mke kwa sababu anasali sana?! WATU WENGINE BANA AHHH!![/QUOTE]

Hehe hayajakukuta kwa kweli mi imenikuta hiyo mwenyewe maombi toka saa nne mpaka saa nane kila siku. ukimwambia ndio kwanza kesho yake yanaanza saa mbili mpaka saa tisa ukimuuliza unyumba nitapata saa ngapi unajibiwa napatana na Yesu wangu kwanza, na sio kwamba atapatana naye within a week hata miezi inaweza ikachukua sometimes kwa yesu kunawafanya watu wawe vichaa.
 
du

pole mama,

we mama chunguza tu ndani ya baraza la walei humo ndimo mumeo alipotelea
 
Duh mambo haya nilidhani hutukuta sie tu watu wa mataifa kumbe hata huko jikono?? Makubwa!!

Baba yangu yaani umemwacha mama kwa kuwa anasali sana usiku???? Aksante.
 
THIS IS CLASSIC!
RED - Hiki ndicho hasa kisa na mkasa.
Purple - kisingizio kilichokosa maana! Mwanaume wa KKKT utamwacha mke kwa sababu anasali sana?! WATU WENGINE BANA AHHH!!
WOS, una uhakika na unayosema???

Mimi naijua hii issue vizuri....

haya we
 
WOS, una uhakika na unayosema???

Mimi naijua hii issue vizuri....

haya we

Nimeibua hicho from the caption nikashangaa ndugu yangu...siyo maneno yangu.
Samahani kama inasomeka kuwa najua hiki kisa maana hata sikijui!
 
Makubwa haya!
Hivi huyu jamaa si yule alokuwa anaburuzana na maaskofu!? Huyu si mchungaji ni mlei, labda kapata mlei mwenzake huko masaki.
Yasemekana anatesana na mdada mmoja wa BOT alokumbwa na libeneke la EPA akahamishiwa arusha. Wachunguzi tujuze kwa kina.
 
..Mwenegoha siyo mchungaji, alikuwa mwajiriwa wa KKKT.

..pia ameachana na mkewe akiwa tayari si mtumishi wa KKKT.

..hivi ina maana kama ulipata kuajiriwa na taasisi ya kidini, kama bwana Mwenegoha, basi ndoa yako inakuwa immune na misukosuko?
 
Nyie KKKT mbona mnatukwaza siye waamini? Mara mkuu anunuliwe VX V8 na fisadi, mara mkewe apewe MarkX na mtoto wa fisadi, ni nini jamani? Ebu tafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na hayo yote mtarudishiwa.
 
Mwenegoha alishawahi kutibuana na maaskofu na Msuya waziri mkuu mstaafu. Labda laana inamfuata.
 
Katika familia nilizokuwa nazi-admire ni ya huyu Mwenegoha... Enzi hizo alifunika sana pale usharika wa Mjini kati... Shame on him...
 
Mwenegoha alishawahi kutibuana na maaskofu na Msuya waziri mkuu mstaafu. Labda laana inamfuata.

.
Sio siri huyu Mwinigoha kama hali bangi kisiri basi ana pepo mkubwa sana wa ngono. Ona sababu anayoitoa ya kumtaliki mkewe haina nguvu ya aina yoyote kidila zaidi ya kuitukana imani ya kikristo. KKT mna kazi ya ziada.
 
Lakini Bible inasema 'alichokiunganisha Mungu binadamu yeyote asikitenganishe'
 
Back
Top Bottom