Amshitaki Bi Harusi Kwa Kumkataa Siku ya Harusi

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Mwanaume mmoja wa nchini Malaysia amemfungulia mashtaka ya madai ya fidia aliyekuwa bi harusi wake kwa kumtosa dakika za mwisho mwisho kabla ya harusi kufungwa.

Masran Abdul Rahman mwenye umri wa miaka 32 alibaki haamini macho na masikio yake masaa sita kabla ya harusi baada ya bi harusi wake kukataa kuolewa naye.

Masran amefungua kesi mahakamani akidai fidia ya dola laki tatu na nusu ili kufidia gharama alizoingia kuandaa harusi hiyo.

Mwanasheria wake alisema kwamba Masran na familia yake ilihuzunishwa na kuachwa ikiwa imetiwa aibu na bi harusi Norzuliyana Mat Hassan alipoamua kuuvunja uhusiano wake na Masran muda mchache kabla ya harusi kufungwa.

Mwanasheria huyo alisema kwamba Masran aliwaalika jumla ya watu 1200 kwenye harusi hiyo.

Masran amemfungulia mashtaka aliyekuwa bi harusi wake na baba wa bi harusi huyo akidai alipwe fidia kwa gharama alizoingia pamoja kuumizwa hisia zake.

Taarifa zaidi zilisema kwamba bi harusi aliamua kuvunja uhusiano wake na Masran bila ya kutoa sababu zozote za kufanya hivyo.
 
Hiyo kesi naiunga mkono kwa 100% na fidia inahusu kufidia muda, pesa na udhalilishaji mbele ya jamii!!
 
dah hii kesi ni nzuri sana,nna uhakika hata judge atakae isikiliza ataenjoy sana..
 
Mdada angepaswa kufanya maamuzi ya kuachana way before taratibu za harusi kuanza.
 
Back
Top Bottom