Amos Makalla, Legacy yako ni Jiji la Dar es Salaam kuwa Safi

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,048
Nimesoma Dar, nimeishi Dar kabla sijahamia Mkoani Ruvuma, kusema kweli Dar imekuwa na sifa kuu 3

1. Uchafu

2. Mipango miji mibovu iliyopelekea ujenzi holela wa Makazi hadi maeneo ya biashara( vibanda vya machinga)
3. Joto na foleni za Barabarani

Namba tatu ni sababu zilizo nje ya uwezo wa binadamu! Joto ni sababu za ki jeografia zaidi ingawa kwa foleni imetokana kwa kiasi kikubwa miundombinu mibovu!

Kwa namba moja na mbili naamini unaweza kushughulika nayo. So far kwenye kuwapanga machinga napenda niseme tena big up umeonesha inawezekana ingawa Kuna maeneo madogo bado unapwaya maana wanaonekana kurudi taratibu kwa kubeep mfano Barabara za mjini na mwenge bila kusahau ubungo. Usilale endelea kukomaa na kusimamia maelekezo ya mamlaka jiji hilo lipendeze na kuwa bora

Kwa Mbezi Mwisho napenda nikwambie pale unatakiwa kufanya jambo! Kama Kuna hela tafuteni njia mjenge soko la kisasa la wafanyabiashara pembeni ya stand ya Magufuli. Uzuri maeneo yapo mengi pale ni kuweka tu mkandalasi afanye leveling na mnajenga soko kubwa sana linaloweza kuwa la mfano kwa Dar nzima. Muwapange wamachinga kwenye Hilo soko na mwisho mbomoe na kuchoma vibanda vyote vibavyoharibu mipango mizuri na muonekano wa Barabara ile muhimu.
Inawezekana kwa Barabara ya Morogoro kupendeza Kama Barabara ya Mwenge- Morroco. Tukueni uamuzi sasa


Mwisho kama uzi unavyosema legacy yako kwa Watanzania ni kuipanga na kusimamia mipango miji Dar es Salaam ikiwemo suala la Wafanyabiashara wadogo na usafi kwa ujumla. Kauli ya Mhe. Rais leo naomba ikufahamishe rasmi kuwa hapo ndo nyota yako ilipo. Simamia hilo kwa nguvu zako zote na kuanzia hapo unaweza kuonekana kuwa unaweza kwa nafasi za juu zaidi ya hapo.
 
Back
Top Bottom