Amenisaliti anang'ang'ania vitu vyangu

Amenisaliti anang'ang'ania vitu vyangu

Wana jamii wenzangu mimi ni mwanaume wa miaka 29 nimekuwa na uhusiano na msichana kwa miaka 3 mwishoni mwa mwaka niligundua kuwa ana uhusiano na mtu mwingine na nilipombana kwa maswali alikubali na kusema wamekuwa pamoja kwa miezi 8 ila wameachana wiki mbili zilizopita nimeumia sana maaana nilimwamini mno, nimeamua kuachana nae ila nilimpa laptop yangu ya gharama sana ya laki 9 kwa makubaliano nitamnunulia ya kwake ila baaada ya usaliti aliofanya nimeona anipe mali yangu .Cha ajabu anang'ang'ania kwa kusema anaitumia na kwa sasa hawezi kunipa,kipekee sipendi fujo nafikiria kutumia nguvu ila naona ni utoto na naweza kusababisha matatizo.Naombeni ushauri nifanyeje?

fanya kama imepotea. Kitendo cha wewe kumpigia simuu au kuwasiliana naye kwa njia yoyote kwa ajili ya laptop itakufanya uje ubadili mawazo na kurudiana naye. Na iwapo utarudiana naye atakudharau maana atajua udhaifu wako ulipo. Mfute yeye pamoja na laptop katika kichwa chako.
 
rafiki yangu alisema kiutani

haki za mpenzi/gf ziainishwe kwenye katiba

naanza kuelewa huo utani waweza kua jambo muhimu sana
 
kachukue tena liustaarabu tu bila ugomvi
bt usimrudie hafai huyo
msaliti hyo

Ubarikiwe dada, hakika umeonesha busara na ni tumaini langu maneno haya hayaishii katika keyboard tuu. Wasichana wote wangekuwa kama wewe hakika matatizo katika relationships yasingekuwa mengi kama sasa.
 
mwanaume ndo kaweka price tag,PC kitu kidogo sana,ths kind of thng once happened to me,NILIRUDISHA PC YAKE mapema tuu,na sikumdai chochoteee...he js proved how stupid he was

Yap PC ni kitu kidogo, kwa nini aking'ang'anie.? Yaani pamoja na usaliti alioufanya na kukiri kwa mpenziwe bado tuu ana guts za kung'ang'ania PC aliyoazimwa.?

Umetolea mfano wewe uliokutokea, kwa busara ukaona urudishe PC. Why nawe usimshauri huyo binti arejeshe hiyo PC..?
 
siwez jua what kind of rshup they had,bt the thing is si ALIMPA MWENYEWE BILA SHURUTI,basi amwachie...sio ishu yani kuny'angany'ana vitu aisee,ni ujinga yani,mi cjui nmeumbwaje but mara nyingi siogopi kuachia hata vitu ambavyo they meant a lot to me..i js let it go,and Mungu mkubwa i got PC nyingine,tena macbook,sio ki'toshiba hcho alichosepa nacho
 
Yap PC ni kitu kidogo, kwa nini aking'ang'anie.? Yaani pamoja na usaliti alioufanya na kukiri kwa mpenziwe bado tuu ana guts za kung'ang'ania PC aliyoazimwa.?

Umetolea mfano wewe uliokutokea, kwa busara ukaona urudishe PC. Why nawe usimshauri huyo binti arejeshe hiyo PC..?

pc hairudishwi apa...tena ningekuwa mie ata sijibishani nae....angechoka mwenyew kudai
 
Wana jamii wenzangu mimi ni mwanaume wa miaka 29 nimekuwa na uhusiano na msichana kwa miaka 3 mwishoni mwa mwaka niligundua kuwa ana uhusiano na mtu mwingine na nilipombana kwa maswali alikubali na kusema wamekuwa pamoja kwa miezi 8 ila wameachana wiki mbili zilizopita nimeumia sana maaana nilimwamini mno, nimeamua kuachana nae ila nilimpa laptop yangu ya gharama sana ya laki 9 kwa makubaliano nitamnunulia ya kwake ila baaada ya usaliti aliofanya nimeona anipe mali yangu .Cha ajabu anang'ang'ania kwa kusema anaitumia na kwa sasa hawezi kunipa,kipekee sipendi fujo nafikiria kutumia nguvu ila naona ni utoto na naweza kusababisha matatizo.Naombeni ushauri nifanyeje?

Jitutumue ununue nyingine, hiyo mwachie ili mawasilano yakomee hapo hapo (unless bado unampenda)
 
pc hairudishwi apa...tena ningekuwa mie ata sijibishani nae....angechoka mwenyew kudai

Hahahaaahha..! Usifanye hivyo kwa mushi, yaani akikumbuka machungu ya kugegedewa plus kumrusha PC yake. Nadhani atakodi AK 47 kabisaaa.
 
Hahahaaahha..! Usifanye hivyo kwa mushi, yaani akikumbuka machungu ya kugegedewa plus kumrusha PC yake. Nadhani atakodi AK 47 kabisaaa.

teh...apo kwa mushi kdg isue....lakin kingeeleweka tu......atlst I died tryin.......kwa ufupi io pc asingeipata aisee...maana kama kudhalilishana tumeshadhalilishana....kiendacho kwa mganga hakirudi ng'oo...kalagabao!!!!
 
Lakini si wameachana madam mbona unakuwa mkali jamani,Raisi muda wake unapoisha yale ambayo hakuyafanya atayafanya anayekuja yeye aruidishe tu hiyo laptop then atanunuliwa na mwingine atakayeshika madaraka
Angekuwa amemmimba mngesa airudishe hiyo mimba?
 
Si ushamba na wala si umasikini, bali inarudisha confidence na hadhi kwa mwanamume. Ningekuwa mimi ningemshauri jamaa aende kwenye vyombo vya usalama. kama ana shida kweli na laptop na anaihitaji plus vithibitisho vya umiliki wa laptop kama anavyo hiyo ni case rahisi sana. Atapata laptop yake bila matatizo.

Ila kama ana moyo wa kusamehe, haitokuwa mbaya pia akisamehe.
Hadhi ya mwanaume haitafuti kwa kulialia na vitu vidogo, huo ni udhaifu na kutokujiamini,. mwanaume mwenye hadhi yake, anaejiamini hawezi kudai vitu kwa mwanamke aliyeachana nae hata kama ingekuwa gari sembuse laptop ya laki 9!.
 
kachukue mi nilishadai hadi dictionary na vitop we uache laptop acha uzembe kijana
 
Hiyo potezea,mbona wewe hurudishi utamu ulioupata?
 
Hadhi ya mwanaume haitafuti kwa kulialia na vitu vidogo, huo ni udhaifu na kutokujiamini,. mwanaume mwenye hadhi yake, anaejiamini hawezi kudai vitu kwa mwanamke aliyeachana nae hata kama ingekuwa gari sembuse laptop ya laki 9!.

Hahahaaaa....! Mwanamme wa shoka na anayejiamini ni yule anayedai haki yake mpaka mwisho na anayesimamia anachokiamini mawazoni mwake. Huyo anayeachia kitu katika mahusiano huku akiamini anastahili na anahaki nacho huyo si mwanamme wa shoka bali ni mwanamme jina.

Haya mambo ya kuendesha mahusiano kizungu ndio yanayowaharibu wavulana wa sasa. Kuna mipaka inatakiwa ichorwe kwenye mahusiano ili mwanamke aeleweke na mwanamme aeleweke.
 
hivi unadhani kuna kitu gani alimpa? Mi mnaniudhi mnaposema mnatupa wakati tunapeana na wote raha twasikia!!

Yaani mkuu hawa watoto wa kike wanajidhalilisha wenyewe, kwa kauli hii inadhihirisha kuwa wanakuwaga katika mahusiano kwa kutegemea benefits kama hizi. Halafu wanasema wanataka wathaminiwe na waheshimiwe. How come nikuheshimu kama wewe mwenyewe hujiheshimu na hujitambui.?
 
Mapenzi ya utoto hayo!!
We muachie bana na yeye akisema umrudishie alivyokua anakupa utaweza weyeee
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom