Ameamua kuni unfriend mpaka kwenye fecebook

Ameamua kuni unfriend mpaka kwenye fecebook

MZIBHAZI

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
520
Reaction score
139
Ni msichana niliyeishi nae miezi kama 7 tulikua tunaishi poa tu badae kulitokea kutoelewana tukaishi mbali na mbali lakini kwakua nilikua nampenda sana nilimsihi na kujishusha yaishe, lakini yeye alikaza nikatumia mpaka rafiki zake wakimwambia kuhusu mimi hataki hata kuwasikiliza, nikimpigia simu hapokei nikimwamdikia sms hajibu.

Nikakaa kama miezi mitatu nikajaribu kumcheki na kumwambia naenda kumsalimia akanimkasirikia sana sana fecebook alikua rafiki, lakini naona juzi kaniunfriend sijui hata nifanyenini? Hivyi huyu tunaweza kurudiana kweli au nikomae kivyangu.

Ingawa roho inauma na nampenda sana na kwanini kaniunfriend? Ndio najiuliza wakati marafiki zangu wote bado rafiki zake na akiongea nao wanaitana shemeji ingawa wakimwambia kuhusu mimi anawachenjia.
 
Duh! Duniani kuna mambo, nimejikuta nacheka sana. Pole sana kijana
 
subiri shule zifunguliwe urudi upige kitabu hao wapo tu ukimaliza mambo yako watakuja tu.

Kua na Adabu basii wewe unadhani kila mtu ni mtoto mkuu hapa shauri kama huwezi pita tuu
 
Hahahahaaa Kwanini umecheka Bhululu ebu toa ya Moyoni mkuu tushauriane kiongozi

Mkuu huyo achana nae asikupotezee mda wako ukashindwa kufanya mambo ya maana. Wanawake wako wengi sana. Usijione kama umepoteza, jipe mda wa kutuliza akili yako, na kumsahau, ingawa itachukua mda kidogo, ila taratibu utazoea. Kila la kheri.
 
Urafiki ni mkataba na sio lazima uwe wa milele. Tujifunze kukubaliana na mabadiliko ya tabia za watu. Heshimu maamuzi yake nawe tafuta opportunity nyingine. Hakuzaliwa kuwa wa umoja wa kudumu.
 
Una umri gani rafiki? Kabla hamjaanza kuishi pamoja na mdada huyo mlifahamiana kwa muda gani....???
 
Kaza buti fanya yako anakujalibu kukuona unampendaje mpotezeeeee kwa kufanya yako na tafuta mwingine fashta utaona yeye menyewe anaaanza ona wivu amini hilo
 
Polee ila tunashindwa kutoa ushauri maana hamueleweki maana utaskia nina mke mara leo mschana. Kama sikosei ushaleta uzi kuhusu mke leo tena msichana. Anyway.
 
Polee ila tunashindwa kutoa ushauri maana hamueleweki maana utaskia nina mke mara leo mschana. Kama sikosei ushaleta uzi kuhusu mke leo tena msichana. Anyway.

We Luckyline ebu toq ushauri apo mama angu tufanyeje ishakua maji ya shingo ujue
 
nikusaidie jambo japo najua utapuuza

USIMFATE FATE,WALA KUMPIGIA SIMU WALA KUMTUMIA MARAFIKI ZAKE(jikaze usimtafute) nakupa week moja tu lazima arudi kwako
 
Kaka always nawashauri humu kuwa..."Mwanaume lazima uruhusu moyo wako uwe kama Jalala" lazima wakati wote uandae moyo wako kupokea mazuri na mabaya...siyo mazuri tu...! ukiweza hili nakuhakikishia....pressure hutaipata, stress hutakuwa nazo...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom