Ambao mna marafiki huwa mnawapataje?

emoji1666.png
emoji1666.png
emoji1666.png
emoji1666.png

Yan just like me, marafiki zangu nlonao n wale nlomaliza nao chuo, hatunaga story Zaid ya kuview status, huku mtaani Nako Sina rafiki n mm na kazi zangu basi hata ikitokea shughuli Sina wakuongozana nae, ni tabu kweli kweli nawaza hata siku nikiwa nshughuli nani atanisaidia so sad, and I don't know how to get out this
Anza na kanisani unaweza imba hata kwaya hao ndo watakua watu wa krb
 
Ninajichanganya nao wapi yani nadhani pa kuanzia ndio sina
Nina rafiki zangu wawili ila kwa sasa nimewaweka kwenye level ya ndugu
Amebaki mmoja ambaye ni jirani yangu anaelekea kuwa ndugu pia.
Nilichongundua urafiki hauji from vacuum una sababu zake na haupaswi kuwa forced
Rafiki yangu mmoja nimekutana nae primary wa pili nimekutana nae high school na huyu wa mwisho ni jirani yangu ila wote wana sababu zao katika muingiliano baina yetu.
 
Good morning jf....
Tusio na marafiki tukutane hapa😔

Kuna hili swala nimekua nikijiuliza hivi karibuni, baada ya kuona sasa uzee umeanza kupiga hodi. Najiona umri umetangulia mbele halafu maisha ni kama nayaacha nyuma, ni kama naishi tofauti na umri wangu. Nimesogea umri wa kuozesha, kuondokewa na wapendwa (waliozeeka) na kukutana na mambo mengi ambayo nadhani yanahitaji watu....ila bahati mbaya sasa hao watu ndio sina.

Natamani kuwa na marafiki kuwa na watu, watu wa faida, watu ambao wanaweza kushare ramani za maisha, watu ambao tunaweza kupanga safari kwenda vituo vya wahitaji tukawape misaada, watu ambao nikihitaji kumwagilia moyo najua wapo, watu ambao nikikwama najua watakuwepo, kina mama wenzangu huwa wana vyama umuhimu wa vyama naujua ila mi hata chama sijawahi kuwa nacho....naishi mwenyewe mwenyewe tu hadi nawaza si nitakosa wa kunizika mie mwisho nizikwe na manispaa.

Wenye marafiki mnawapataje???
Ummeolewa au ni single mama,tuanzie hapo kwanza nikushauri kitu
 
Evelyn Salt kuwa na marafiki ni safari.
Kwanza inabidi ujue 'interest' yako baada ya kazi ni nini, 'social status' na 'class yako'. na baada ya hapo ndiyo utaanza mchongo wa kusaka marafiki.
Kama wewe ni mtu wa unywaji, uta 'hang out' huko na utawapembua huko, na hili lazima uwe na 'company' ya washikaji mchangayiko(me+ke bila 'strings attached') ili kuweza kulenga marafiki.
Kama una 'interest' ya 'Gym' basi utapata marafiki kwenye 'Gym' inategemea 'standard' yako ya maisha.
Kazini unaweza kuwa na marafiki lakini kwa uzoefu hawawezi kuwa wengi labda wawe na 'interest na social status' kama yako.
Inabidi ujiunge na Jumuiya ili kupata wa 'kukuzika' au unapopata jambo la kijamii ijapokuwa huwezi kusema ni marafiki na wanakuwa watu wa 'standard' zinazotofautiana sana.
Wengi sisi tuna 'washikaji tu' ambao wanaishia getini lakini marafiki wachache sana..
Kwa hitimisho navyojuwa mimi sehemu ni tatu tu kazini, sehemu za starehe au gym lakini pia huwezi kuwa mwenyewe sana inabidi uwe na 'company' ya mshikaji uliomzoea.
 
Good morning jf....
Tusio na marafiki tukutane hapa😔

Kuna hili swala nimekua nikijiuliza hivi karibuni, baada ya kuona sasa uzee umeanza kupiga hodi. Najiona umri umetangulia mbele halafu maisha ni kama nayaacha nyuma, ni kama naishi tofauti na umri wangu. Nimesogea umri wa kuozesha, kuondokewa na wapendwa (waliozeeka) na kukutana na mambo mengi ambayo nadhani yanahitaji watu....ila bahati mbaya sasa hao watu ndio sina.

Natamani kuwa na marafiki kuwa na watu, watu wa faida, watu ambao wanaweza kushare ramani za maisha, watu ambao tunaweza kupanga safari kwenda vituo vya wahitaji tukawape misaada, watu ambao nikihitaji kumwagilia moyo najua wapo, watu ambao nikikwama najua watakuwepo, kina mama wenzangu huwa wana vyama umuhimu wa vyama naujua ila mi hata chama sijawahi kuwa nacho....naishi mwenyewe mwenyewe tu hadi nawaza si nitakosa wa kunizika mie mwisho nizikwe na manispaa.

Wenye marafiki mnawapataje???
Story of my life😪
 
Mm naona inakuwaga automatic ila jifunze kujichanganya na watu penda kusalimia kushirikiana na watu kwenye msiba na sherehe pia marafiki watakufuata tu
 
Back
Top Bottom