Wanaume tukumbushane katika suala hili

Intelligent businessman

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
26,179
52,892
Bro,
Kikao cha hiki kijiwe sio kama kile cha wanaume wa UWABATA, Hachana na wanaume wasiojielewa, hatuna haja ya kuunda 'hashtag' hizo pigo waachie wanawake.!

Hachana na wanaume wasiojielewa, wao na wake zao wanalumbana kila siku,
Unajua kwa nini.!? Kwa sababu hawajielewi.!
Hawavai kilemba cha uwanaume mbele ya wake zao, hata matunzo madogo madogo kwao wanaona ni kujilamba kiwiko.

Sio kwamba hawana, ila wamekaririshwa ujinga na wahuni kadhaa wanaoongoza Dunia wanaotaka kuharibu Ubinadamu.
Najua hapa hujaelewa bro, ni story ndefu.!

Wanaume hawa wanawakandamiza wake zao kiasi kwamba wake wanaanza kuunda hashtag kutetea umuhimu wa majukumu ya wanaume kwao, inafika hatua matunzo ya kawaida kama chakula inaonekana ni "Kodi" wanaiita kodi ya meza.

Hata wenye kipato kikubwa wakishajua matunzo wanayotakiwa kutoa kwa wake zao ni "Kodi" basi wanapambana kulipa kodi kidogo, kama ilivyo kawaida ya Ubepari.
Mchezo huu ulianza miaka karibu 300 iliyopita huko Ulaya "walipogundua" biashara za viwanda, bidhaa na fedha.

Mfumo huu wa maisha wa kutengeneza faidia tu waliouita "Capitalism" sasa wameanza kuuweka katika maisha ya watu na mahusiano,
Hakuna Utu tena.!
Kila mtu anataka kumfanya mtu mwingine "kitega uchumi" kutengeneza faidia.

Bro,
Sisi bado tuna akili, tunajua ukiachana na faida ya kiuchumi, Maisha bado yapo hata kama kungekuwa hakuna pesa za mfumo wa makaratasi, hata kama kungekuwa hakuna Haki za Binadamu kwenye maandishi, hata kama maandishi yenyewe yasingekuwepo bado maisha yangeendelea tu.

Najua ni ngumu kuelewa bro maana nakurudisha mfumo wa Maisha wa zamani kidogo ulikuwa na Undugu kati ya mtu na mtu, huu mfumo uliitwa Ujamaa, hacha ule ujamaa wa kisiasa kuna ule Ujamaa wa kale mababu zetu waliishi mwanaume akiwa mwanaume na mwanamke akijua nafasi yake.

Maisha yaliendelea, hakukuwa na kutafuta Maisha, maisha yalikuwepo tu as long as kila mtu alikuwa hai, na upendo ulikuwepo kwa kila aliyekuwa hai, Ubinadamu ule wazungu wanaoitwa Humanity ulikuwa sio wa kulipia, Ubinadamu ule Utu wenyewe haukuwa kitega uchumi.
Watu hawakuwa wajinga Maisha yalisonga.

Leo sasa, Bro.!
Wanaume wanajiita "Bahiri"
Wanawake wanajiita "Cash-Madam"
Hilo neno Bahiri asili yake ni kwenye ule Ubepari wa kuunda Faida tu katika kila nyanja ya Maisha, kimamtoni wanaita "Capitalist"
Cash Madame imekuja kuziba pengo la "Whatever Man Can Do..."

Wanawake 'wote' sasa wameambukizwa hicho kirusi cha Capitalism, wanaona kila mwanaume ni biashara tayari kwa kujivunia faida ambayo hawajui wataitumia wapi.
Inachekesha mahitaji ya kawaida ya wanawake, wanawake wenyewe wameamua kuyaona ni "Kodi" inayotakiwa kulipwa "Kisheria" na mwanaume yeyote.

Sasa kwa kuwa ni Ubepari, Kodi ndo jambo pekee ambalo linaonekana kukwamisha "biashara" hata wanaume hawataki kulipa Kodi, hii ni kwa mfanya biashara yeyote na huo ndio mfumo ulivyo ndivyo ulivyoundwa.

Sasa bro unajiuliza wananunua na kuuza nini mpaka walipane kodi.!?
Mpaka mwanaume awe na hela ndo anachukuliwa kama mtu kwenye jamii, kwani ananunua Mwanamke.!?
Nimekwambia hachana nao, hawajui walitendalo wako ndani ya kifungo huru cha fikra wanaongozwa na mfumo uliowekwa na wahuni kadhaa miaka hiyo.

Bro,
Sio kwa wanaume tu kuna na hawa ma-Slay Queen ambao kila mmoja anataka ku-trend, kuwa viral huko Tik Tok.
Yuko tayari kuweka mwili wake wote ulio uchi mbele ya filter camera apate followers na jina lake la "pretycutie_official" sasa sijui badae ataolewa na nani. Tunamfahamu, tumesoma nae ukweli anaitwa Magdalena Wanjuki.

Wengi na digrii zao au bado ndo wanazitafuta, kama hataki iPhone basi tafuta simu nyingine lakini huwa anapatwa na vipele na muwasho akinusha harufu ya Tecno na Infinix.
Anataka simu yenye speed kwa ajili ya kuingia Instagram asipitwe na umbea wa Michambo na Juma Lokole, kila ukikutana nae Smartphone ndo kipaumbele chake, na uhakika wa bando.

Sijasema msinunulie shemeji zangu mambo mazuri wanayopenda ila msiende kuchukua watumwa wa wale wanaume wa UWABATA, wao wanaamini kila mwanaume ni kitega uchumi kama walivyofundishwa na hao Mabepari wao, wanadhani mwanaume lazima awe ni mwenye pesa.
Nje ya hapo kuna plan B ya kupata sponsor.
Sponsa ni mzee, umri wa enzi za mwalimu.

Bro,
Sisi sio kwamba tukae bila kutafuta pesa, lakini pesa isiwe kipaumbele cha Maisha, kuna wale wanaotafuta pesa utafikiri hilo ndo lilimleta Duniani, nimekwambia hachana nao watu wa hivyo, Ishi kwenye Maisha yako na hizi propaganda za Kodi na Capitalism weka uvunguni mwa kitanda chako cha miti.

Mwanamke usiwe kama unamlipa akupende ila unaweza kumrudishia fadhili za upendo wake, mpe vitu vizuri, mhudumie, usimtenge, muoneshe ushirikiano hacha kuwa wanaume wa UWABATA, kama una familia vaa uanaume wako hacha mahitaji nyumbani kwa kiwango cha kipato chako mpaka moyo wako usikusute kwa lolote.

Bro,
Kama bado ndo unatafuta mwanamke, Epuka matapeli, kuna hizi Pisi zinazotaka zione mwanaume ni yule tu mwenye ofisi yenye AC awe anaendesha kama sio V8 au V6, basi anadhaniwa hajui kupenda na amefeli maisha.

Hawa mabinti wa kupika ugali with a pinch of salt na blue band na kucha zao kama mwewe, watahisi nawatukana maana hawanioni vizuri, kila kifuniko cha jicho kimepakwa rangi yake huku wakifunikwa Uoni kwa kichaka cha nyasi bandia juu ya nyama za kope.
Kuwa nao makini sio kwa kuwa hawajui kufua bali hata kulea kizazi chako watasubiri ku-Google.

Hawa wanaoona sisi wabangaizaji hatuna lolote ndio 2035, kama sio kuwa wameoana na wanawake wenzao, basi watakuwa na mabango ya "Natafuta mwanaume yeyote" nitakuwa palee na screenshot za Comments walizoziandika kwenye makala zangu zikisomeka "Tafuta hela wewe..."

Bro,
Fanya maisha yako bila kuendeshwa na mwanamke mtumwa wa wanaume wa UWABATA.
Kama anakuuliza Funguo ya Ofisi iliyoko posta mwambie tu ukweli wewe una kijiwe chako cha kuuza kahawa kwenye kituo cha waendesha guta pale Kigogo sokoni alafu utasikia alivyozoea kuambiwa kuna hela inasikiliziwa.

Utamkutana leo, kesho asubuhi atakwambia anakupenda pia, kesho jioni utajua ambavyo ana siku nyingi hajala chips kuku, ambavyo ana hamu ya kutoka out na marafiki zake, kabla ya kukwambia Nywele zake huwa anapaka Deudoranti ya 35k, Mtumie vocha ya bando elfu 5 anataka kukutumia picha WhatsApp uone aina ya gauni alilopenda ni 75k dukani Sinza.

Huyo piga chini bro,
Hizo ni Pisi za mtandaoni,
Kesho kutwa amkia kijiweni, UsikateTamaa.!

👉 I mean no malice to nobody
FB_IMG_16857249313687362.jpg
 
Ndio maana single mothers hawaishi. Wanadanganywa na wanaume kama nyie nakuvunja ndoa zao wakiamini wananyanyaswa na waume zao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom