Amazing: Form iv leaver wawa ma-house girl | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amazing: Form iv leaver wawa ma-house girl

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Shoo Gap, Apr 20, 2011.

 1. Shoo Gap

  Shoo Gap JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 236
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nimekutana na mabinti watatu sasa waliomaliza kidato cha nne mwaka jana ambao wanafanya kazi za house girl. Mwanzoni sikuyaamini macho na masikio yangu. Siku ziliposogea na kukaa na kuzungunza nao niligundua kuwa ni sahihi wao kufanya kazi hiyo kwani uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana. Nina maana elimu ya msingi na miaka minne ya sekondari haikuwakomboa. Mimi kama mwalimu ninasikitika sana kuona jinsi ambavyo jamii na taifa wakiongozwa na waalimu tumeshindwa kuwaandaa watoto kukabiliana na changamoto za maisha. Yaani hawa niliowaona wamefeli CSEE na pia elimu ya maisha tu.

  Hii ni dalili mbaya sana kwa Taifa na wadau wote wa elimu. Tunakipeleka wapi kizazi chetu cha leo? Kuna dalili zinazoonesha wazi kesho si ajabu kukuta F6 leaver au hata Graduate akitafuta kazi ya House girl, kutokana na mfumo mbovu wa elimu.

  Ni lazima tuchukue hatua haraka ili wanetu, wanafunzi wetu, watoto wetu wasifikike hapa hawa mabinti walikofikia. Angalau akifeli CSEE basi awe ameelimika kukabiliana na maisha akitumia rasilimali zinazomzunguka.
   
 2. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mimi pia ni mwalimu kama wewe, lakini sioni mantiki ya kutumia neno 'amazing'. Kuna ajabu gani mimi sielewi.

  Mtu akimaliza kidato cha 4 anatakiwa afanye kazi gani? Nimewahi kuishi Spain kidogo na nimekutana na watu wenye shahada ya uzamili wakifanya kazi zinakaribu kufanana na hizo ulizotaja.

  Ukiwa kama mwalimu ulitakiwa utuambie kuwa katika kazi yako unadhani unawaandaa wanafunzi wako wawe akina nani katika jamii. Je, unawapa elimu inayowapa 'ujuzi' fulani? Endapo wewe ni mwalimu wa shule za upili unayetumia mtaala huu wa MoEVT unalo jibu!

  Tunahitaji wasaidizi wa nyumbani WASOMI, na si mbumbumbu!
   
 3. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Nani kasema house girl maana yake mtu asiyeenda shule?
   
 4. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Mkuu nasema hili tena.. mtaala mzima wa elimu ya tanzania una mashaka!...

  Mtoto ambaye ni kiazi darasani "mjinga" asiyekuwa mwepesi kuelewa haraka katika elimu ya TZN ilivyokaa huyu mtoto hasaidiwi atabaki vilevile atamaliza shule na mtihani mgumu sana wa necta.. "

  Tofauti na wenzetu mtoto huyu huyu mzito kuelewa katika nchi za wenzetu atafundishwa ili aelewe na atapewa mtihani standard kumpima kile alichosoma...

  wakati nipo mwaka wa kwanza chuoni huku ughaibuni katika department ya physics wanafunzi wa mwaka wa pili wana solve physics ambayo mi niliisoma Advance mzumbe pale. nikashangaa kweli..! ingawa ni mwanafunzi niliyesoma PCB "so i wasnt i big fun of physics" but nilikuwa naweza nikasolve yale maswali but siwezi kuyafanya katika vitendo practically bt they can!

  back to the topic serikali iangalie upya mtaala wa elimu TZN
   
 5. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,934
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Lugha za watu hizi! Nijuavyo mimi ukisema 'amazing' mara nyingi unaashiria kustaajabishwa kwa namna ya kufurahisha!
   
 6. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu hiyo ni kazi kama kazi zingine za kuajiriwa. Ukizingatia anakula na kulala bure. Je wewe katika mshahara wako ukitoa pesa ya kula na kodi ya nyumba, unabakiwa na kiasi gani cha pesa?. Utagundua ni sawa tu huyo HG.

  Ushauri wangu Jina House Girl Libadilishwe na Waitwe "House Executive" au "House Managers".
   
 7. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Unashangaa hg kuwa iv! Ngoja ufumbuke macho ndipo utagundua baby-sitter ni graduates na watu wenye master!
   
 8. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mhh hivi house girl sio watu jamn acheni kuwadharau
   
 9. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Mkuu, hakuna jinsi kwani ajira ndo hizo zilizopo, bora hii kuliko kuwa mtoto wa mama!
   
 10. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  In the Phillipines kuna degree za uhausigeli zinatolewa na utakutana na house maids wngi tu wenye digrii wakifanya kazi huko huko kwao, UAE, Israel, Hong Kong etc.
   
 11. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Huyu ndugu alipatwa na mshangao kutokana na mtazamo wake juu ya kijana aliyemaliza form iv alipaswa kuangalia fursa zipi katika maisha, yeye kwa mtazamo wake hakuonelea vyema kwa huyu kijana kuangalia kazi za ndani kutokana na mazingira ya kazi yenyewe yalivyojengeka katika jamii yetu. Halafu kama nimemwelewa vizuri SHOO GAP ameshangazwa na ufahamu alionao huyu kijana pamoja na kuwa amemaliza form iv, hakupaswa kuwa kama yeye hivyo alivyomuona.

  Hata nami nilipatwa na mshangao wa namna hii mwanzoni wa mwaka huu pale tulipokuwa tunatafuta binti wa kutusaidia shughuli za ndani, kuna kijana mmoja alituahidi kutuletea mdogo wake. Siku alipokuja huyu binti niliongea nae na mwisho nilitaka kupata hakika kama amepata elimu ya msingi, badala yake alinieleza amemaliza form 4 kidogo nilipatwa na mshituko kama ndugu yangu.

  Lakini na mimi nili-experience kitu ambacho SHOO GAP amejaribu kuelezea hapo juu kwamba ufahamu wake ulikuwa chini sana, vitu vingi alionekana kuwa anavishangaa. Siku moja nilimwomba binti yangu kunichukulia dairy yangu chumbani, basi yeye aliuliza kwa mshangao sana kwamba hicho ni kitu gani.

  Kweli tunahitaji kuchukua hatua katika kuongeza value ya elimu tunayopata hapa nchini, haswa katika hizi shule za kata.
   
 12. Papa Diana

  Papa Diana JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 304
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Inawezakuashiria kwamba kiwango cha Elimu kinapanda au sahihi zaidi idadi ya watu wanaohitimu elimu ya sekondari na vyuo inaongezeka wakati kazi zenye hadithi elimu hiyo hazitoshelezi!!!!..yaani hata ma-house wanabidi angalau wemefikia form four! Nchi za ulaya (nasikia hata Nigeria pia) unaweza kukuta mtu na Degree lakini anafanya kazi sehemu kama Best Bite/MacDonalds......

  Lakini hata hivo mimi ningependa kumwajiri mtu mwenye elimu kama housegirl nyumbani (form six leaver) nikijua kwamba atanisaidia zaidi nyumbani...hata homework za watoto wakirudi kutoka shule.....

   
 13. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Siku hizi Watanzania waliowengi hasa mijini wanaishi kisomi - somi hivyo wanahitaji wasaidizi waliosoma na kuelewa lugha ya kiingereza japo kidogo. Mitaala yetu haiwaandai wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuweza kujitegemea watakapohitimu, bali huwaandaa kuendelea na elimu ya juu. Bahati mbaya mwanafunzi asipofaulu mtihani 'hana pa kwenda'. Tuitathmini mataala yetu kwa ajili ya kuandaa vijana wetu waweze kujitegemea.
   
 14. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Ukigraduate form iv na dv 0 yako huna tofauti na mtu aliyeishia la saba.
   
 15. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Mwl.uko sahihi. Ila fikria pia kama wote tungefaulu na kwenda mbele au wote tukawa PhD holders,si mwishowe mmoja angemtumikia mwenzie? Au ukumbuki feudal mode ilivo rise? Lazima wawepo. Hata ivo we unamshangaa housegirl wakati mimi namshangaa mwalimu anayekubali mshahara wa lak3 na kuzunguka na zigo la fito kuhesabisha namba wakati mi kama mhasibu na mkaguzi wa hesabu nazunguka na pen na laptop tu,pia kuna mtu ananishangaa pia,anazunguka na hummer akikagua miradi yake. Ivo ivo wote tunaishi!
   
 16. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #16
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hapo kwenye red,kilicho kushangaza ni kipi na jibu unalo?
  pia mkuu ulitaka wafanye kazi ofisi ya waziri mkuu na wakati hapo kwenye blue umefafanua?.
   
 17. Mahai

  Mahai JF-Expert Member

  #17
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Educational system ya Tanzania ni mbaya sana na watoto wataendelea kufeli sana kama serikali haibadilisha hii system. Unless watoto wote wapelekwe kwenye shule za private ambazo system yao ni bora zaidi kitu ambacho hakiwezi kutokea.
   
 18. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #18
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,655
  Likes Received: 2,897
  Trophy Points: 280
  Ha ha haaa! Mbaya zaidi anayetumia neno 'amazing' ni mwalimu anayewafundisha hao Form IV, halafu anategemea wasiwe ma-house girl! Amazing! Tehe tehe!
   
 19. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #19
  Apr 21, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mshaara wa house girl ambaye ana elimu kuanzia form four ni TShs 150,000/- na pia ana marupurupu ikiwa pamoja na sehemu ya kulala na chakula pia anakatwa NSSF, Hapo itakuwa imetulia na wala hakutakuwa na shida ya kuwapata
   
 20. Shoo Gap

  Shoo Gap JF-Expert Member

  #20
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 236
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nashukuru Mgombezi kunielewa nilichomaanisha, uwezo wao wa kufikiri hawa mabinti hauendani na kiwango chao cha elimu.

  Nashukuru wengine pia walionipa uzoefu wa nchi nyingine, lakini ni vizuri tukakubali ukweli huu kwamba Tz tulizoea kuwaona std 7 na hata ambao hawakumaliza std 7 wakifanya kazi za house girl. Mitaala yetu haijaandaliwa kuwawezesha wnfz kujitegemea, na kuyatumia mazingira yao ili kuboresha maisha yao. Ni kweli hatuwezi kulingana wote kielimu, na hatuwezi wote kufanya kazi zinazofanana, ni lazima kuwa na maisha ya kutegemeana. Lakini, ninapaswa kutegemea utendaji nzuri zaidi kwa house girl wa f4 kuliko wa std 7.
   
Loading...