Ni nini hatma ya ma-house girl? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni nini hatma ya ma-house girl?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ramthods, Jul 9, 2010.

 1. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2010
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Mara nyingi ninapokuwa na hoja tofauti kidogo na wanajamii wengi au ninapotofautiana mtazamo hupenda kushirikisha watu - ili kujua mtazamo wao ni upi hasa.

  Na leo ningependa niwashirikishe jambo ambalo kwa muda sasa nimekua nikisema "Kuna siku nita posti hapa JF", ingawa sina uhakika kama kuna thread kama hii iliyowahi kutangulia awali.

  Najua wengi wetu (hasa hapa Dar) tunaishi na hawa wadada wanaotusaidia shughuli mbalimbali majumbani mwetu. Inawezekana wewe ni mwajiri, mwana familia, au kwa namna moja au nyingine unaishi na house girl hapo nyumbani kwako.

  Ukweli hawa wadada huwa wanatusaidia sana, na tumewapa nafasi nyeti kama kutupikia chakula, usafi wa nyumba, kwenda sokoni, kutulelea watoto n.k. Ukiangalia mshahara tunaowalipa ni kidogo sana ukilinganisha na ukali wa maisha ya leo. Kwa kifupi, hautoshi kufanya jambo lolote lile la maana. Jaribu kufikiri house girl anayelipwa alfu 20,000 kwa mwezi - hiyo inatosha tu kukunua "vijiguo" na mafuta - haiwezi fanya jambo lolote lile la maana.

  Miezi kama miwili hivi iliyopita tulikua tunapiga story na mzee mmoja (mtu wa makamo kama miaka 56 hivi) kuhusu house girl wake. Nikashtuka aliponiambia kuwa house girl wake amekuwa akiishi nae kwa takribani miaka 15 sasa. Navyozungumza na wewe, umri wa huyu house girl ni miaka 34, na mshahara wake ni sh 40,000 - bado hajaolewa!

  Kuna house girls wengi ni visirani (najua hilo wengi tunalijua), ila kuna house girls wengine tunaishi nao, na kwa tabia zao wanakua kama moja ya watoto wa nyumbani - wana kila sababu ya kupewa hiyo nafasi kutokana na tabia zao zilivyo nzuri!

  Huyu mzee alimsifia sana house girl wake kwa tabia nzuri na jinsi walivyoishi nae kipindi hichi chote. Huyu mzee ana mtoto yupo Form 2. Huyu mtoto amebebwa na huyu house girl tangu akiwa na mwezi mmoja. Ingawa anamwita huyu house girl dada, ukweli huyu house girl ni kama mama yake mdogo hivi!

  Baada ya kushtushwa na hii hadithi, ukafika wakati wa swali muhimu ambalo hata hivyo sikutaka kumuuliza pale pale nikihofia angejisikia "aibu" kwa kiasi fulani.

  "Baada ya kukaa na mtoto wa mtu kwa muda wote huo, ukimwona kama sehemu ya familia yako, na ukijua hasa kuwa mshahara unaompa ni mdogo sana usioweza kufanya chochote cha maana katika maisha yake - ni nini hasa ulifikiria cha kumrudishia kwa fadhila zote hizo alizokukarimu kipindi hicho chote?"

  Kwa kweli hili lilinihuzunisha mno. Jaribu kujiweka upande wa familia ya huyu house girl - kama mama, baba, kaka, dada - vyovyote vile - alafu utaona ni kiasi gani inahuzunisha.

  Najua wengi wetu tunaweza sema - "Tumewaajiri na tunawalipa!" - ingawa ukweli ni kwamba wale waliowahi pata bahati ya kuwa na ma house girl wazuri, hawa ma house girls hujituma na kufanya kazi kama sehemu ya familia, na sio kama waajiriwa. Wanastahili kulipwa kama wafanyakazi, na kama sehemu ya familia pia. Kupata kile ambacho hata wewe ungependa watoto au ndugu zako wapate. Mfano elimu au future nzuri ya maisha. Ila hatuwapi hiyo nafasi, na hatufikirii hatima ya hawa watu. Tunapokea fadhila bila kujali kurudisha chochote kile, hata kama ni kidogo!

  Hapa jirani yetu kuna msichana mmoja aliletwa toka mkoani kama house girl. Baada ya muda akawa anauza duka la jumla (nadhani aliacha kule kwa mwajiriwa wake wa kwanza ambako alifanya kwa muda mrefu tangu akiwa msichana mdogo). Yule mama aliyemwajiri dukani akagundua kuwa yule msichana alikua na "sharp mind", akampeleka shule ya QT (ile unayosoma miaka miwili form 1 - 4).

  Huyu msichana alifaulu, akaenda kusoma tena mwaka mmoja form 5 - 6, akafaulu. Mimi nimemaliza chuo 2008 hapo UDSM. Ila nilishangaa wakati wa kufanya clearance nikakutana na huyu dada anajaza form pamoja na wanafunzi wa mwaka wa kwanza!

  Kweli Mungu mkubwa! Nilivyorudi nyumbani nikwambambia mama kuwa yule msichana nimekutana nae UDSM, mama ananiambia ni kweli, amepata mkopo hivo anaenda chuo kikuu.

  Kwa waliopo UDSM mwaka wa 2, wanaweza wakawa wanamjua huyu msichana. (Hope atakuwa amewahadithia rafiki zake safari yake ndefu ya maisha).

  Je, ni wangapi wetu tumeziba ndoto kama hizi zising'ae kumulikia ulimwengu? Kama house girl wako umeishi nae kama "mwanao" kwa muda wote huo, shukrani yako kwake kama "mwanao" ni ipi?

  Hawa ma house girl ni watoto kama watoto wetu tu. Ni shida za maisha ndizo zimewafikisha hapo walipo.

  Kama wana uwezo, tusiwe wachoyo kuwaendeleza. Japo hata kwa course ya kiingereza - pengine ikabadilisha future yao.

  Je, nini nin hatma ya house girl wako? (Wale wenye house girls visirani, naomba msichangie kwa upande huo!)
   
 2. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hii ni changamoto mhimu sana kwetu sote tunaokaa na mahousegirl. Kwa kweli hawa watu wanahitaji sana kuheshimiwa na kupewa umhimu sawa na watoto wetu. Hebu niambie huyu binti atakavyomthamini huyu tajiri wake. Hongera zake huyo mama. Naamini atapata thawabu kubwa mbele za Mungu.
   
 3. M

  Magezi JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Huyo mama nampongeza kwa kumjali huyo binti. Lakini ma-housegirl wengi huhalibiwa na wamama kwani huwachukia sana wakidhani watachukua nafasi zao kwa waume zao. Binafsi napenda sana kumsaidia binti wangu wa kazi lakini tayari nakutana na vigingi kutoka upande wapili.

  Wito wangu tu ni kwamba tuwasaidie hawa mabinti wetu wa kazi kwani ni watoto/wadogo wetu pia.
   
 4. PlanckScale

  PlanckScale JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2010
  Joined: Sep 28, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Mkuu nakubaliana kabisa na msimamo wako kuhusu wasaidizi nyumbani.

  Kuweka uwazi, mimi msaidizi wetu ambaye tunakaa nae, tunamuongeza mshara kila mwaka. On weeekend yuko ofu Kuanzia jumamosi mchana mpaka Jumatatu asubuhi. Anapata nafasi ya kwenda kwao kama mara mbili kwa mwaka. Makorokoro yote ya nyumbani (sabuni, mafuta, n.k) ni juu yetu. Hawajibiki kufanya kaziI baada ya saa 2 usiku. Hayo mambo ya kumfanyiza kazi mtu 24 hrs / 7 days a week hatuna!

  For us, there are two main reasons for this "policy";
  One - Ubinadamu.
  Two - we have also been there. Having worked in all kind of low paying jobs huko majuu, me and my wife definitely know what it means being at the low end of the social hierarchical.

  There is also an issue of trust and security...It is a good thing to take care of someone who is looking after your precious thing - your child. I am sure you have heard of the horror stories...
   
 5. B

  BA-MUSHKA Member

  #5
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wazo jema sana. wengi huishia kupigwa, mshahara mdogo na kukopwa 'mzigo' wakipata mimba wanafukuzwa.
   
 6. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #6
  Nov 24, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kwakweli tunapaswa kuwalipa fadhila me nilibahatika kuwa na hg 3 lakini wote hawakunipa nafasi ya kuwalipa fadhila kwa umapepe wao so sikukaanao sana
   
 7. B

  Brandon JF-Expert Member

  #7
  Nov 24, 2010
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 336
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mh,ni kweli kuna hg mapepe balaa,mi kuna mmoja nilikuwa nae alikuwa anamfungia mtoto ndani anaenda kwa bwana zake. Ila huyu wa sasa namshukuru mungu, she is such an angel. Nasubiri mtoto wangu akifika two years namtafutia shule. Ana akili nzuri sana na ameshajua kiingereza kidogo maana ndo lugha ya hapa home.
   
Loading...