Amani na utengamano wa nchi yetu. Ushauri kwa TEC

Amani na utengamano wa nchi yetu. Ushauri kwa TEC

Kwanza ,Nyerere hakudai uhuru kanisa katolic nchini ndio lilithibitisha kwamba Tanganyika inaweza kujitawala baadae ndo Nyerere akatengenezewa njia kanisa halikudai uhuru WA Tanganyika ili yawe hayatunayoyaona

Dr slaa hajawahi fukuzwa labda hujui chochote
Sahihi.
 
Dini zina nafasi kubwa sana kwenye mtengamano na amani ya lo lote lile. Ndiyo maana kwa kuliona hili, baadhi ya nchi serikali zake zinatawaliwa na dini moja, hususanj huko Uingereza nk Anglican High Church..

Nchi yetu ina dini kuu mbili, waislamu na wakiristo. Ingawa katiba ya nchi yetu inasema serikali haina dini lakini ukweli unabaki pale pale kwamba dini hizi mbili zina influence (nguvu) kubwa sana kwenye utengamano na amani ya taifa letu.

Ndiyo maana hata kama haiko kwenye maandishi ya kikatiba, mtiririko wa utamaduni wetu ukuu wa nchi umekuwa wa kupokezana kati ya hizi dini kuu mbili. Alianza mkiristo (Nyerere), akafuata muislam (Mwinyi), akaja mkiristo (Mkapa), akafuata muislam (Jakaya), halafu akaja mkiristo (Magufuli) na sasa tuna muislamu (Samia). Na bila shaka awamu ya saba atakuwa mkiristo.

Mtiririko huo haukuja kwa bahati mbaya (coincidence). Ni utamaduni wetu wa kuheshimu nguvu ya dini zetu hizi kwenye ukuu wa nchi na ndiyo uliochangia kwa kiasi kikubwa kwa amani tunayojivunia ya taifa letu. Na mara zote isipokuwa awamu hii dini hizi zimekuwa na utiifu mkubwa kwa mkuu wa nchi na serikali yake. Dini hizi zimekuwa zikituaminisha kuwa mkuu wa nchi ni chaguo la Mwenyezi Mungu na kwa wakristo 'ya Kaisari mpe Kaisari, ya Mungu mpe Mungu'.

Inasikitisha kuona kwamba katika awamu hii ya muislamu, TEC ambayo mtendaji wake mkuu ni ndugu au swaiba mkuu wa kiongozi wa chama kimoja cha siasa anayeutafuta ukuu wa nchi kwa njia ya yote ile ikiwemo ya vurugu, limekuwa likimsakama na kumdharirisha sana mkuu wa nchi na serikali yake. Hotuba wa raisi wa TEC ya Pasaka inaonesha wazi matakwa ya kanisa hili la kuingilia kesi iliyoko mahakamani ya mtuhumiwa wa uvunjifu wa amanj ya nchi yetu ambayo TEC wanaita ni kesi ya watuhumiwa wa kudai haki.

Hotuba/ waraka wa Pasaka ni tofauti sana ule wa Eid El Fitri wa waislam uliojitikita kwenye kudumisha amani. TEC mnakotaka kutupeleka si pa zuri. Huyo katibu mkuu wenu, Dr Kitima, hana tofauti na aliyekuwa kabibu mkuu wenu, Dr Slaa, Mtimueni kama mlivyofanya kwa Slaa akaungane naye kwenye siasa na kuoa.
Hao TEC mbona walikuwa wanamsema Magufuli Mkatoliki mwenzao.....acheni hoja za kitoto.Yaani kiongozi badala yan kujibu hoja anajificha kwenye kichaka cha udini,ipo siku atajificha kwenye kivuli cha uanamke na kuna siku atasema kwa sababu yy ni wa upande mwingine wa Muungano
 
Mh. Freeman Mbowe alichelea chelea mwana kulia matokeo yake alikuja kulia mwenyewe na hadi leo anaendelea kulia. Kwa kipindi kirefu Tundu Lissu alionesha wazi ukosefu wa utiifu wa hali ya juu kwa Freeman Mbowe hadi kufikia kumporomoshea matusi na kukinukisha. Mbowe akachelea kumchukulia hatua kali za kinidhamu, matokeo yake alilia yeye na hadi leo analia.

Mbinu hizo chafu sasa kazielekeza kwa mkuu wa nchi na serikali yake. Na haya kayasema wazi wazi hadharani mbele ya kamera, si mara moja au mara mbili bali kila mra. Sasa hawa TEC wanataka huyu mkuu wa nchi na serikali yake aendelee kuchelea chelea ili kitokee kama kilichomtokea Bw. Mbowe? Yaani kweli hata ungalikuwa wewe ungalimchelea kweli mtu mwenye nia (intent) na matendo (overt actions) yenye kusudi (attempting) ya kukinukisha achukue nchi?

Sikiliza maungamo yake ya uhaini: Sasa kwa nini TEC inataka kuizuia mahakama kutafisiri kisheria haya anayoyasema na kuyatenda huyu mtu?


View: https://youtu.be/Pgu4VfqBGKs?si=rWJ7yaVNkAwXL7OC

Hujitambui wewe njoo ule kitimoto akili ikukae sawa
1000265347.jpg
 
Atakayeamua km Lissu kafanya uhaini au la ni mahakama tuliza makalio. Serikali ina uwezo na wajibu wa kumweka yeyote mpk kizuizini ikimwona anahatarisha amani, shukuruni huyo amepelekwa mahakamani. Mnatumia vibaya uhuru mliopewa na serikali mmesahau mlikotoka.
Sijui kama unaelewa area of contention. Kesi za kubumba ni matumizi mabaya ya madaraka, muda wa mahakama na fedha za taxpayers. Tumeziona hizi kesi za ajabu ajabu zikijirudia kama vile nchi yetu haina watu wenye akili timamu. Kwa mfano, kesi ya Mbowe ilikuwa na tija gani? That’s idiocy. Pure and simple!
 
Back
Top Bottom