Mtu Alie Nyikani
JF-Expert Member
- Nov 9, 2022
- 1,355
- 3,090
Wakuu kwema?
Leo hii, moyo wa taifa letu unapitia majaribu. Kumekuwa na ongezeko la matukio ya utekaji, mateso na mauaji ya raia hasa wale wanaotoa maoni tofauti au kusimamia haki. Hali hii inaleta hofu, giza, na ukimya wa kulazimishwa.
Matukio haya yameipaka doa nchi yetu ambayo kwa muda mrefu imejulikana kwa amani na utulivu
Lakini pamoja na hayo yote, bado nina imani.
Nina imani kuwa hii si Tanzania ya milele. Nina imani kuwa ukimya huu si ushindi wa uovu. Ninaamini kuwa damu ya wasio na hatia haitapotea bure. Kila tone ni kilio cha haki, na haki huwa haipotei – huchelewa tu. Nina imani kuwa dhuluma haiwezi kushinda milele.
Serikali, kwa upande wake, inapaswa kufanya kazi yake kwa uwazi na kwa haki. Uhalifu hauna rangi ya chama wala dini – wote wanaohusika na utekaji na mauaji lazima wawajibishwe kwa mujibu wa sheria, bila kinga wala kufichwa nyuma ya taasisi. Vyombo vya usalama visitumike kuumiza, bali kulinda.
Ni wajibu wa kila mmoja wetu viongozi wa kisiasa, wanaharakati, waandishi, watu wa dini, vijana, na wazee – kusimama kwa wima na kutetea utu, uhuru, na haki za kila Mtanzania.
Tunaweza kutofautiana kimawazo, lakini tusikubali kutofautiana katika utu. Amani ya kweli haipo kama watu wanateswa kwa maoni yao.
Hizi zama za giza zitapita.
Na Tanzania yetu – ile ya upendo, haki, na sauti za watu – itarudi salama.
Stay Safe
Soka
Mdude
Ally Kibao