Ama zake ama zangu……………….!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
AC6mMqH5gJzZAAAAAElFTkSuQmCC

Siku hizi sina raha, na mke wangu nyumbani

Nirudipo kazini humkuta, kajiinamia

Nauliza vipi mke wangu, mbona umekasirika, hushindwa kunijibu hubakli anaalia

Nazidi kumbembeleza sana sana mke wangu ee, mwisho naye kaamua kunielezeaaa

Eti anafahamu mambo yangu yotee, nifanyayo nikiwa kaziniii

Eti nina wanawake wengi sana mie, hivyo basi anataka tutenganeee

Namfikiria ampaye maneno mke wanguu, nami sitokubalii namsaka mbea huyooo

Jamani……………

Rudia mwanzo……………………………

Ama zake eee ama zangu, ole wake akae akijua labda nismtambueee……

Naelewa nia yake ni kutaka kunigombanisha,imekuwa sikai na kufurahi mimi na mke wanguuu

Mtu huyoo adui yangu, kanitafuta kwa siku nyingi naona amenipataaa

Hao wanaitwa DDC Mlimani Park Sikinde……………..
 
ebu na umjue fasta ili umkomeshe iyo tabia ya kutaka kukuvurugia amani ya nyumba
nakuachia kibao cha majirani wabaya.......... hawaitakii ndoa yangu mema na msondo ngoma na pia usisahau gubu la mawifi na umbea wa vijana jazz band
 
Hii sio story mkuu,we sema tu yaliyokusibu ili tuchukue hatua.......ni Canta kakuchonganisha na mamake?
 
Hii sio story mkuu,we sema tu yaliyokusibu ili tuchukue hatua.......ni Canta kakuchonganisha na mamake?
Mkuu Bishanga hata wewe tunavunjiana heshima kweli..............................? LOL
 
Last edited by a moderator:
jamani baba ngina pole punguza hasira yatakwisha hayo ni ya hapahapa duniani wala hayatoki kwa Mungu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom