Am feeling guilty, nafsi inanisuta

ningetunza mtoto hilo halina shida kabisa

We jamaa wewe! Sasa kama hili tu la kumdrop mmoja linakumaliza hilo la mmoja kuwa mjamzito na kutunza mtoto si tungekusindikiza kaburini?
Kama uliweza kumpa space huyo mwenye chemistry, mpe space, likizo, yellow card na red kadi huyo mwanafunzi ila mweleze kistaarabu.

Tatizo ni kwamba, hata utumie lugha gani, guilty hauta ikwepa na ujifunze wakati mwingine kwamba maamuzi yana gharama zake.
 
Ndugu kuwa makini. Kama ulikuwa na malengo na huyo mchumba wako wa zamani, kipi haswa kilichokufanya ukaingia tena kwenye mahusiano mengine?

Kwa tabia hii, huna mipaka, yani kila mwanamke anayejilengesha, wewe unazoa tu. Unataka kujiaminisha kuwa ukiingia kwenye ndoa ndio utatulia? Si rahisi hivyo.

Unajisikia unamkosea msichana wa chuo tu. Hujisikii kumkosea huyo msichana unayefikiri atakuwa mke wako. Au unafahamu huko alipo naye anachepuka kama wewe. Kama hivi ndivyo, basi ni kweli huna sababu ya kutokujisikia vibaya kumsaliti. Vinginevyo, wewe jamaa una hatia kubwa, pande zote.

Fikiria siku mke wako mtarajiwa akigundua ulikuwa na mahusiano mengine, hali itakuwaje. Usifikiri kirahisi kuwa kumwacha huyo wa chuo, mambo yanaweza kuishia hapo. Unaweza kuigharimu familia yako unayotarajia kuijenga.

Ukiweza, mwambie na huyo mke mtarajiwa kuwa ulianzisha mahusiano mengine. Muombe radhi. Usitake yeye ajirekebishe halafu wewe unafanya hayo unayotaka ajirekebishe na pengine hili lako likawa ndio baya zaidi.

Waambie wote, kila mmoja kwa linalomhusu. Then, weka msimamo wako kwa kila mmoja. Kaa pembeni, subiria reaction. Basi.

Mke mtarajiwa akisema hapo ndio mwisho. Ukubali. Na umwache mtoto wa chuo aendelee na maisha yake. Umeshaweka bayana kuwa humuhitaji. Usimrudie kwa kuwa umeachwa na mke mtarajiwa. Itakuwa rahisi sana kumtenda tena hapo mbeleni.

Kila la kheri
 
Ahsante kwa ushauri mzuri [emoji120][emoji120]
 
Sijawahi kupata wakati mgumu kuachana na mtu pale ninapoona sihitaji kuendelea nae
 
Uzuri ni kwamba; Wewe si mwanachuo mwenzake kwani angeumia sana mkikutana holini. Huyo mliyeanza naye mbali nadhani ndiye ataumia zaidi akifahamu kuwa unamwacha kwa sababu ya mwanachuo. Mpe haki yake ya ndoa kwani hata kwenu wesha mwita mwali, wifi nk.
Vya chuo viachie vidume vyao.
 
Cha ajabu ni pale utakapo gundua huyo wa Chuo ndo wakufanya nae maisha halafu huyo wa ubani wako karudi kwako na ngwengwe akuambukize.

Kipindi kifupi tu mlichopeana break ukaanzisha mahusiano na mwingine, sasa na upande wa pili nako alianzisha mahusiano na mwingine halafu kwa bahati mbaya wanawake hawajui kuacha....utagongewa mwanzo mwisho.
 
Mwache haina shida sababu kabla yako alikuwa na mahusiano mengi na anajua uchungu wa kuachwa.....maskini labda we ndo mwanaume wake wa kueleweka waliopita wote wahuni tupu [emoji23][emoji23][emoji23]
Mungu muone mtu huyuuu
 
hapana mkuu hana mahusiano yoyote mengine am sure
 
[emoji120]
 
Ungemuoa hata huyo ambaye huna feelings naye!?
😡😡😡


toa ushauri......ningekua muslim ningeoa wote wawili
 
[emoji22][emoji22][emoji22][emoji26][emoji22][emoji26]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…