Ndugu kuwa makini. Kama ulikuwa na malengo na huyo mchumba wako wako wa zamani, kipi haswa kilichokufanya ukaingia tena kwenye mahusiano mengine?
Kwa tabia hii, huna mipaka, yani kila mwanamke snayejilengesha, wewe unazoa tu. Unataka kujiaminisha kuwa ukiingia kwenye ndoa, ndio utatulia? Si rahisi hivyo.
Unajisikia unamkosea msichana wa chuo tu. Hujisikii kumkosea huyo msichana unayefikiri atakuwa mke wako. Au unafahamu huko alipo naye anachepuka kama wewe. Kama hivi ndivyo, nasi ni kweli huna sababu ya kutokujisikia vibaya kumsaliti. Vinginevyo, we we jamaa una hatia kubwa, upande zote.
Fikiria siku mke wako mtarajiwa akigundua ulikuwa na mahusiano mengine, hali itakuwaje. Usifikiri kirahisi kuwa kumwacha Huyo wa chuo, mambo yanaweza kuishia hapo. Unaweza kuigharimu familia yako unayotarajia kuijenga.
Ukiweza, mwambie na huyo mke mtarajiwa kuwa ulianzisha mahusiano mengine. Muombe radhi. Usitake yeye ajirekebishe halafu wewe unafanya hayo unayotaka ajirekebishe yeyea na pengine hili lako likawa ndio bays zaidi.
Waambie wote, kila mmoja kwa linalomhusu. Then, weka msimamo wako kwa kila mmoja. Kaa pembeni, subiria reaction. Nasi.
Mke mtarajiwa akisema hapo ndio mwisho. Ukubali. Na umwache mtoto wa chuo aendelee na maisha yake. Umeshaweka bayana kuwa humuhitaji. Usimrudie kwa kuwa umeachwa na mke mtarajiwa. Itakuwa rahisi sana kumtenda tena hapo mbeleni.
Kila la kheri