Marcossy A.M
Member
- Aug 21, 2008
- 61
- 24
Wagumu,
Baada ya takribani miaka minne ya uvumilivu na kujitenga nimerejea hapa jukwaani tuendelee kujadiliana na kupashana habari zenye tija kwa nchi yetu. Miaka minne hii niliitumia kwa mambo makubwa matatu:
1. Kujiendeleza kielimu na kukamilisha utafiti: Hii ikumbukwe ni kujiweka sawa kiakili na kuongeza uzito wa heshima jukwaani kufikia PhD ambayo mwisho wa mwaka 2016 nilitunukiwa pale SuA. Lakini pia iliendana na kukamilisha utafiti wangu juu ya Umasikini Tanzania (kuna mengi ya kuongea hapa);
2. Kushiriki ipasavyo kwenye siasa na uongozi wa nchi. Itakumbukwa kuwa nilijitosa jimbo la Morogoro Mjini 2015. Pamoja na kumabulia nafasi ya pili lakini kuna mengi nimejifunza na bado ni masomo sahihi kwa wanasiasa wetu na hatima ya uongozi wa nchi yetu; na
3. Kuweka mawazo, masomo na mitazamo yangu kwenye maandishi (naogopa kufa bila kuacha alamu jumuishi shirikishi fungashio). Nimekamilisha kuandika kitabu changu cha kwanza: Why is Tanzania Poor? Na ambacho kwa sasa kinapatikana mitandaoni na kwa kuagiza amazon.com. Ninaamini taarifa na uchambuzi wa yaliyomo huko yatasaidia sana nchi yetu na wanaoijali.
Kwa sasa napatikana,
Asanteni