Ally Hapi awa mbeba magunia

Ally Hapi awa mbeba magunia

Haijalshi kama alikuwa anatafuta kiki au ni kweli.

Tazameni video clip jinsi aliyekuwa rc na aliyejiita kiboko ya wapinga Magufuli anavyo piga gunia kibabe.

Amakweli hujafa hujaumbika.View attachment 2427744
Hawa ndio wanasiasa wa mfano si wengine kutwa wapo social networks wana payuka payuka. Huyu sasa akiongelea ujasirilimali ana maanisha .
 
Sijaona alipobeba magunia ila naona anasimamia vijana,ni moja kati ya psychological treatment unaposimamia watu halafu ukawa kama sehem yao inatia hamasa kwa unaofanya nao kazi. Ni kitu cha kawaida sana sema sisi binadamu sijui tukoje.
 
Tatizo mmeshakariri lazima ufanye white collar job ndio uheshimike kwenye jamii ili hali unapokea kamshahara kidogo.Ila mtu akiamua kulima au kufuga anaonekana amepoteza.FYI umfikii Ally hata kidogo hizi harakati ameanza kitambo tokea akiwa kwenye uongozi hiyo Kolowasi farm ni ya kitambo acha wivu na porojo.
 
"Kabla hujafa hujaumbika."

Uandishi wako umekaa kishambenga hata umepoteza lengo.
Na wala sijaona chochote cha ajabu alichokifanya kwenye Hiyo clip ! Kwani ukiwa RC au Waziri unakuwa kama yai au nyanya ? Yaani kazi ndogo kama ya kumsaidia mwenzio mzigo kuupakia kwenye gari iwe nayo ni habari. ?!! Hao waheshimiwa ni binadamu kama binadamu wengine na kazi za kutumia nguvu ni lazima wazifanye kwa ajili ya kujenga misuli yao kwa afya zao. ! Mtu akiwa na pesa nyingi haina maana eti kazi ngumu ngumu asizifanye maana huyo mtu sio dhaifu kama nyanya au kama yai kwamba litavunjika!! Tuwaige wazungu wanavyopenda kuishi simple na kuonekana stronger sio kuishi legelege na kuonekana Obesity ni hasara wajameni !!!
 
Huyo alikuwa anafanya hizo kazi akiwa Rc iringa ni mwanaume huyo sio WaDar Pia
Yaani nimeshangaa kuona wapo watu wanaona ni jambo la ajabu sana kwa mtu yeyote mwenye pesa au wadhifa kusaidia kupakia mzigo kwenye Gari! Duh !! 😳
 
Ukabaila ulipenda sana kuwatukuza watu walioitwa wa nasaba bora( nobles) ambao kimsingi walibobea kwenye uvivu( idleness) huku ukiwadhalilisha wafanyakazi(working class), wakulima(peasants), na wafanyabiashara(merchants).

Kibongobongo watumishi wa umma, hasa wenye vyeo vya kisiasa wamejipachika nafasi ya noble families.

Ndiyo maana Hapi anaonekana kituko kwasababu anajinadi kama paisano ingawa bado hajaondoka kwenye nasaba bora.

Lakini kwa uasilia, kufanya kazi kwa aina yoyote kunahusiana moja kwa moja na upatikanaji wa pesa na hivyo tunapaswa kumpongeza huyu kijana(kama kweli amedhamiria) na sio kumshangaa.

Ajabu kubwa zaidi kwa vijana wa kibongo ni kutoweza kuhusianisha kazi na upatikanaji wa pesa!
 
Kibongobongo wanaamini pesa inapatikana ofisini tu na kwenye deals !! Ndio maana vijana wameyakimbia mashamba huku home. !! Bado tupo mbali sana !!
 
Hawa ndiyo wenye akili kuwa mtu akiwa na elimu kiasi fulani siyo mwananzengo tena a akifanya kazi za kiuananzengo anachukuliwa kama kama kibwengo. Akili za ajabu sana hizi ndani ya karne.

Hapa ninapoishi kuna jamaa wana mambo ya kijinga kama haya akinikuta nafanya mambo yangu nyumbani ananiambia utakuwa umechanganyikiwa kwa mfano yupo aliyewahi kucheka sana aliponikuta nafuga mende na nzi chuma.

Kazi ya elimu ni kipanua maarifa na kuyatumia sehemu yoyote ile. Kuwa Rais, Mbunge, Mkurugenzi n.k siyo vigezo vya kumzuia mtu kufanya mambo anayoyataka na yanayofanywa na wengine.
Tuache ushamba na chuki za kipuuzi
 
Haijalshi kama alikuwa anatafuta kiki au ni kweli.

Tazameni video clip jinsi aliyekuwa rc na aliyejiita kiboko ya wapinga Magufuli anavyo piga gunia kibabe.

Amakweli hujafa hujaumbika.View attachment 2427744
Sasa kama ni mkulima unataka asibebe magunia? Kalia hayo hayo wakati mwenzio anatakatisha fedha ili wasimsumbue huko mbeleni!
 
Back
Top Bottom