All good men are married, soo sad

Fereke

Senior Member
Apr 13, 2011
141
500
Tumaini la kwanza ni kwa Mungu ambaye ndiye aliyeweka agano takatifu la ndoa. Kutamani ndoa ni Kutamani jambo takatifu sana.. Na umwambie Mungu hivyo kuwa natamani na nahitaji kutimiza agano lako.
Yeye anaijua nafsi yako kama kweli unatamani kwa Nia takatifu au malimwengu tuu.
Kama na kwa kutimiza kusudi lake mwenyewe atakupa hata leo.
Ila hutaweza kumgundua kuwa ndie mume wako. Maana mume Mwema huwa hatambuliki kirahisi unaweza akawa ni yule unayemdharau zaidi.

Kupenda ni kujifunza.. Upendo wa mapenzi ni artificial sio natural.. So you can learn to love. Upendo wako na mama mzazi ni natural hata mgombane vipi bado bond yenu haitenganishiki.
Ila upendo wa mwenzi ni artificial lazima ulindwe kwelikweli. Maana ni created so must be maintained vinginevyo ndio ndoa zinazovunjika au ndoa zilizojaa Mateso na uharamia.
Je unataka mume kweli??? Una uhakika? Ondoa vigezo vyote ila tuu mwambie Mungu nipe mume wa kunifaa(full stop).

Mungu anamjua wa kukufaa.
 
Somoche

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
5,034
2,000
Una akili ndogo sana.

Kuwa na wake 30 hakukuzuii kuwa na michepuko kama ana tamaa.

Selemani alikuwa na wanawake 700 lakini hakuridhika, bado akawa na michepuko 300.

Kuoa wake wengi haijawahi kuwa tiba ya michepuko.
Basi Subiri Mumeo umzae mwenye akili nyingi kama zako...la sivyo utajdinywa sana huku ukisaka mume huku mitandaoni na usimpate kamwe....
 
madindigwa

JF-Expert Member
Aug 30, 2017
1,826
2,000
salaam.

Ama kweli wanaume smart wanao jitambua wanaojua thamani ya mwanamke, wote wameoa inasikitisha sana.

Hivi inawezekana vipi kila mwanaume anae onesha interest kwangu nikamuelewa nikija kumcheki kidoleni nakutana na pete? Hivi ni mimi tu au na wanawake wengine wanakutana na changamoto hii?

Wakuu, sio kwamba wanaume waoaji hawapo, wapo tena wengi sana tatizo ni je huyo anaekuja moyo umempenda? mtu wa kuishi nae lazima moyo umpende.

Je ina maana wakaka ambao hamjaoa ni kweli kwamba hamna sifa kama za hawa married men? kweli hampo?
Nimekuja hapa kusema la moyoni na si kwamba huku ninapoishi hakuna wanaume, wanaume wapo ila wengi wao wameoa, amHbao hawajaoa unakuta moyo haujampenda.

Umri umeenda ninahitaji kuwa na familiya ambayo nitakuwa huru nayo bila lawama. Niwe wazi kuna mtu yupo tiyari kwenda kwetu hata leo tatizo ni mme wa mtu. ana kila sifa ya mwanaume ninaemtaka lakini tatizo ndo hilo. Sijaingia mahusiano nae kwa sababu zifuatazo:,

1: Nitamwambia nini mama?
2: Namuogopa Mungu,
3: Familiya yake wakijua nitafanyaje mimi?
4: Nitakosa raha ya kuwa nae huru, nitakosa raha ya kuwa karibu na ukweni ( mbaya sana)
5: Nitalaumiwa na jamii etc

Hivyo basi nikaona siwezi hiki kiwanja chenye mgogoro, I deserve to have my own family:

Wewe mwanaume,
1) umri 37-45
2) mkristo mcha Mungu ukiwa RC itapendeza
3) Mchapa kazi haswaaa, mtafutaji kama mimi ( staki mwanaume anaelialia yeye kila siku hana hela lawama haziishi huyu hapana)
4) Anajipenda na anapenda kuishi maisha safi
5) mrefu
6)caring person, etc

Kama una hizo sifa njoo pm.
hakuna mtu asiependa vitu vizuri, hakuna asiependa mafanikio, ndo maana nimekuja hapa maybe nikakutana na mtu ambae tunaendana.

Kuhusu mimi,
1: age 35 ndo maana natafuta mzee mwenzangu.
2) sina mtoto, sijawahi kuolewa ila mwanaume huyo akiwa na mtoto mmoja na hana mgogoro na mzazi mwenzie mtamlea coz I like kids.
3) Elimu chuo kikuu
4) Kazi ninayo
5) kinywaji situmii
6) Rangi , rangi safi ya kati situmii mikorogo
7) Dini RC
8) mchapa kazi haswaa with brain.

Mume wangu nimechoka kukusubiri, nimekufuata huku nisije angukie mikononi mwa mme wa mtu. tho ana kila kitu ninachokitaka lakini nikikumbuka mme wa mtu sumu nalia, usichelewe plz nina muda mchache wa kufanya maamuzi.

GOD BE WITH YOU.
Mungu akujaalie
 
Doha City

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
15,701
2,000
Nyie wanawake wenye 35+ munakuwaga na mawivu sana hamchelewi kumchomea mtu ndani nyie.

Na kumpata jamaa wa umri huo 37 mwenye sifa zako wengi washaoa. Labda umpate single Father.
Kila LA kheri
 
Akili Unazo!

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
3,543
2,000
salaam.

Ama kweli wanaume smart wanao jitambua wanaojua thamani ya mwanamke, wote wameoa inasikitisha sana.

Hivi inawezekana vipi kila mwanaume anae onesha interest kwangu nikamuelewa nikija kumcheki kidoleni nakutana na pete? Hivi ni mimi tu au na wanawake wengine wanakutana na changamoto hii?

Wakuu, sio kwamba wanaume waoaji hawapo, wapo tena wengi sana tatizo ni je huyo anaekuja moyo umempenda? mtu wa kuishi nae lazima moyo umpende.

Je ina maana wakaka ambao hamjaoa ni kweli kwamba hamna sifa kama za hawa married men? kweli hampo?
Nimekuja hapa kusema la moyoni na si kwamba huku ninapoishi hakuna wanaume, wanaume wapo ila wengi wao wameoa, amHbao hawajaoa unakuta moyo haujampenda.

Umri umeenda ninahitaji kuwa na familiya ambayo nitakuwa huru nayo bila lawama. Niwe wazi kuna mtu yupo tiyari kwenda kwetu hata leo tatizo ni mme wa mtu. ana kila sifa ya mwanaume ninaemtaka lakini tatizo ndo hilo. Sijaingia mahusiano nae kwa sababu zifuatazo:,

1: Nitamwambia nini mama?
2: Namuogopa Mungu,
3: Familiya yake wakijua nitafanyaje mimi?
4: Nitakosa raha ya kuwa nae huru, nitakosa raha ya kuwa karibu na ukweni ( mbaya sana)
5: Nitalaumiwa na jamii etc

Hivyo basi nikaona siwezi hiki kiwanja chenye mgogoro, I deserve to have my own family:

Wewe mwanaume,
1) umri 37-45
2) mkristo mcha Mungu ukiwa RC itapendeza
3) Mchapa kazi haswaaa, mtafutaji kama mimi ( staki mwanaume anaelialia yeye kila siku hana hela lawama haziishi huyu hapana)
4) Anajipenda na anapenda kuishi maisha safi
5) mrefu
6)caring person, etc

Kama una hizo sifa njoo pm.
hakuna mtu asiependa vitu vizuri, hakuna asiependa mafanikio, ndo maana nimekuja hapa maybe nikakutana na mtu ambae tunaendana.

Kuhusu mimi,
1: age 35 ndo maana natafuta mzee mwenzangu.
2) sina mtoto, sijawahi kuolewa ila mwanaume huyo akiwa na mtoto mmoja na hana mgogoro na mzazi mwenzie mtamlea coz I like kids.
3) Elimu chuo kikuu
4) Kazi ninayo
5) kinywaji situmii
6) Rangi , rangi safi ya kati situmii mikorogo
7) Dini RC
8) mchapa kazi haswaa with brain.

Mume wangu nimechoka kukusubiri, nimekufuata huku nisije angukie mikononi mwa mme wa mtu. tho ana kila kitu ninachokitaka lakini nikikumbuka mme wa mtu sumu nalia, usichelewe plz nina muda mchache wa kufanya maamuzi.

GOD BE WITH YOU.
Seriously need your number otherwise Good Morning
 
sherina

Member
Jul 16, 2021
24
75
Sio kiasi hicho
Smtimes maisha ni kuangalia options zilizopo

who said ukiwa mke wa pili hutaishi vizuri?.

labda kama hujampenda huyo mtu
no simaanishi sitoishi vizuri, kwa nini nisiishi vizuri wakati ana maisha safi? naogopa kelele za familiya yake, na kutokua nae free. thats all.
 
KateMiddleton

JF-Expert Member
Mar 15, 2021
1,053
2,000
no simaanishi sitoishi vizuri, kwa nini nisiishi vizuri wakati ana maisha safi? naogopa kelele za familiya yake, na kutokua nae free. thats all.
kelele kutoka wapi na ameridhia mwenyewe?kutokua nae free kivipi na kila mke ana mji wake?

we sema tu huyo bwana hujampenda...
 
sherina

Member
Jul 16, 2021
24
75
kelele kutoka wapi na ameridhia mwenyewe?kutokua nae free kivipi na kila mke ana mji wake?

we sema tu huyo bwana hujampenda...
hakuna mwanamke mwenye ubavu wa kumkataa hyu mwanaume. wanawake tuna tamaa za vitu vizuri na kila kitu kizuri anacho. yeye mwenye yuko fit appearance.
kelele ninazo maanisha ni mke wake. wewe huwezi elewa.ila wanaume walofanikiwa wake zao sio kwa wivu huo, na nimefatilia hawana mgogoro wowote. inshort naogopa kurogwa wacha niwe wazi. ila asipopatikana hapa sitokuwa na chaguo. ntakubali nisimangwe nimefata mali. ahaaa
kuna siku moja alimtuma dereva anipeleke nyumbani. nikakataa nikapanda zangu daladala.( namkwepa) join akanitumia sms.hivi
'unanikataa kisa nina mke? hakikisha ukipata mtu wa kukuoa akupende na akupe furaha kama ambayo ningekupa. ukijichanganya ukaenda kuteswa huko hii nafasi hutoipata tena ' duh
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom