Pole mkuu.
Mimi sitofautiani na waliotangulia ila nitoe ushauri kidogo ama kusisitiza.
1. Ondoka haraka hapo unapoishi, process zako zote kuanzia baraza la usuluhishi ni lazima usiwe unaishi na huyo mtu.
2. Uendapo katika Baraza la usuluhishi hakikisha kuwa unapambana haswa, ikiwezekana hata vurugu, yaani wao Baraza wasitoke na suluhisho la ninyi kuwatenganisha ila watoke na suluhisho la ninyi kwenda mahakamani kwa kuwapa barua.
Kwanini nasema hivi, Baraza wanatazama huu mgogoro wenu ni wa ngapi, mshawahi kuwekwa chini na kupatanishwa, ukubwa wa mgogoro n.k
Baraza endapo likaona vurugu ni kubwa huwa siku hiyo hiyo wanatoa barua ili iende mahakamani na kwa bahati mbaya baraza la usuluhishi wanasheria hawaruhusiwi, hata kama una ndugu hawaongea chochote kile, wazungumzaji ni ninyi tu.