Aliyeongoza matokeo kidato cha 4; amshukuru Mungu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyeongoza matokeo kidato cha 4; amshukuru Mungu

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Pdidy, Feb 9, 2012.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,151
  Likes Received: 5,578
  Trophy Points: 280
  Kwanza hongera kwa shemeji zangu
  sasa natumaini dunia kama si tanzania wanajua kwanini ttumejzana pale NA SI KWA KUBAHATISHA KAMA WANAVYOTABIRI NA CHAKULA SIO WALI /UGALI BALI ONGEZA NA NDIZI UWE NA AKILI
  tra
  bandari
  ikulu
  wizara za serikali
  nk
  si hicho tu 2015 tunataka kuingiiaaaa ikulu kabisa tushachok a kutomasana tomasana getini ikulu...hii inaonyesha kwamba watanzania wengi wanakubali sasa wachaga awakubahatisha kujazana
  sehemu nyeti za serikalini na sasa wamehamia kwenye ngo zinazonuka hela nyingi nyingi

  lengo kuu haswa ni kumpongeza kashemeji changu jamani andrew swai kwa kuionyesha tanzania
  wachaga atukuja dar kuangalia matairi ya gari wala kuhesabu magari ya showrooms tumekuja kutafuta
  maisha kihalali kupitia elimu

  kwa niaba ya familia ya mushi,moshi,sarangawe,kinabo,marealle,keteleei,
  na familia zoteeee za kichaga tunakupongeza shemeji kwa kukomaa na shule
  hii ndio future iliobakia kwenye dunia hii natumaini mungu aliekufikisha hapo
  anajua wapi unapotakiwa kufika ...na sie wakina kirenga,,urewedi na wengineo
  tunakutakia heri na fanaka na wengine wote waliomfwatia kwa kuonyesha nia ya kumpita shemeji yetu swaii

  kafondao swaii
   
 2. M

  Makupa JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  wazazi wapeni watoto wenu ndizi hiyo ndio siri ya mafanikio
   
 3. I

  Ismaily JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2012
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani wakristo wanaakili kweli mana seminary zao zinaongoza kila mahari,jamani waislam wenzangu tujitahidi na sisi tuweke mkazo ktk masomo ya dunia.
   
 4. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Hongera mdogo wangu Dre, Drew, Andre, Andrew!! Juhudi ziendelee ufumue F6, chuoni na maisha kwa ujumla. Maana kuna wengine wana akili za darasani ila za maisha hola & vice versa. Fanikiwa yote kijana wa Swai!!

  Pdidy tukutane kunywa mbege basi.
   
 5. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Ingekua ndo hvo wakurya nao wangejipongeza,maana wao kuongoza matokeo ya necta huwa ni kitu cha kawaida tu kwao.
   
 6. tete'a'tete

  tete'a'tete JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 474
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera sana mdogo wangu! kila la heri...lakini inabidi tuwaombee na wale wengine walioandika bongo fleva kwenye mitihani kwani nao ni watoto wetu vilevile...na wazazi nao walijitahidi kwa hali na mali kuwalipia ada lakini walichokifanya hata mzazi unaweza pigwa na butwaa kubwa...kizazi hiki mungu tusaidie..
   
 7. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2012
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  hongereni wachaga ....
   
 8. aikaruwa1983

  aikaruwa1983 JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,360
  Likes Received: 1,185
  Trophy Points: 280
  machalari + kitochi + Kitimoto = Division One............pts 7
   
 9. Bakulutu

  Bakulutu JF-Expert Member

  #9
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 1,895
  Likes Received: 313
  Trophy Points: 180
  Saana tuu dogo,bila kusahau ukoo wa massawe,kavishe,urio,MRINA,shirima,laswai,tarimo,shao,bororoni,urassa na watu wote wa kaskazini tunadhamin juhudi zako.
  Safi sana Swai,karibu kabohora.
   
 10. Igabiro

  Igabiro JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huu ukabila utaisha lini humu jamvini?
   
 11. amkawewe

  amkawewe JF-Expert Member

  #11
  Feb 9, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 2,029
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Baba ni kichwa mtoto amedaka toka kwa dingi
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Siri ni ndizi na kitimoto......
   
 13. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,151
  Likes Received: 5,578
  Trophy Points: 280
  nina chuo changu marekani
  nimeamua kumtunuku dr andrew swai jioni hii kwa kweli amenifurahisha
  hivi ndugu zetu mbona yale majina 10 bora majina yetu ayawapo ama atusomi embu tuwekeni sawa ama watoto wetu wakionwa majina yao rashd..nk mnatukaata maksi jamani ??
   
 14. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #14
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,151
  Likes Received: 5,578
  Trophy Points: 280
  siku mkiamua kusoma na kuacha kushinda vyuoni na kula ndizi za bukoba sio mshale

  embu wataalamu wandizi tusaidieni swai alikula aina gani kuna ndizi hadi za kichina jamani
   
 15. African American

  African American Senior Member

  #15
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha ukabila wewe! umejuaje kwamba ni mchagga au unatumia staili ya she Basalehe ya kuangalia jina julius na mohamed na kusema wakristu wanapendelewa?
   
 16. King2

  King2 JF-Expert Member

  #16
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 1,289
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ukabila na Udini hautujengi sisi wote ni WaTanzania.
   
 17. African American

  African American Senior Member

  #17
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tukiendekeza utambuzi wa mafanikio ya watu kwa makundi tutapandikiza mbegu ya baadhi ya makundi kudhani kwamba wao kiasili wamezaliwa kuwaongoza wengine, matokeo yake tutakwenda rwanda au romania.
   
 18. Mtafiti1

  Mtafiti1 JF-Expert Member

  #18
  Feb 9, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 264
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Siku mtakapoacha kuwasema wachagga.Kila siku mnaanzisha mada wachaga hiki, wachaga kile
  Leo wamejianzishia wenyewe kujipongeza mnaiona ngondo!
  Waacheni wajipongeze.
  Hongereni WACHAGGA. HUWA TUNATAMANI TUWE KAMA NYIE NDIO MAANA KILA SIKU TWAWASEMA.
   
 19. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #19
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,151
  Likes Received: 5,578
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Wednesday, 08 February 2012 21:57 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]0diggsdigg

  [​IMG] Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Marian Girls, Roselye Tandau (16) akishangilia jijini Dar es Salaaam jana baada ya kutangazwa mshindi wa pili katika mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha nne wa mwaka 2011. Picha na Venance Nestory

  Fredy Azzah
  BARAZA la Mtihani la Taifa(Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana yanaonyesha kuwa asilimia 53.59 ya wanafunzi 426,314 waliofanya mtihani huo wamefaulu. Hata hivyo, wakati asilimia hiyo ambayo ni sawa na wanafunzi 180,216 wakifurahia matokeo hayo, wenzao 3,301 wamefutiwa matokeo kutokana na udanganyifu ikiwamo mfanano usio wa kawaida wa majibu. Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Joyce Ndalichako alisema wasichana waliofaulu ni 90,885 sawa na asilimia 48.25 na wavulana ni 134,241 sawa na asilimia 57.51.

  "Mwaka 2010 watahiniwa waliofaulu walikuwa 223,085 sawa na asilimia 50.74, hivyo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.63," alifafanua Dk Ndalichako. Wanafunzi 10 bora Dk Ndalichako aliwataja wanafunzi 10 bora kitaifa kuwa ni Moses Andrew Swai kutoka shule ya Feza Boys, Rosalyn Tandau kutoka Marian Girls, Mboni Mumba kutoka St Francis Girls na Sepiso Mwamelo kutoka St Francis Girls. Wengine na shule zao kwenye mabano ni Uwella Rubuga (Marian Girls), Hellen Mpanduji (St Mary's Mazinde Juu), Daniel Wallace Maugo (St Joseph Millennium), Benjamin Tilubuzya, (Thomas More Machrina), Simon Mbangalukela (St. Joseph Millennium) na Nimrod Rutatora (Feza Boys).

  Wasichana 10 bora
  Kwa upande wa wasichana kumi bora, Dk Ndalichako aliwataja na shule walizotoka kwenye mabano kuwa ni Rosalyn (Marian Girls), Mboni (St Francis Girls), Sepiso Mwamelo (St Francis Girls), Uwella Rubuga (Marian Girls) na Hellen Mpanduji (St Mary's Mazinde Juu). Wengine ni Lisa Chille (St Francis Girls Mbeya), Elizabeth Ng'imba (St Francis Girls Mbeya), Doris Noah (Kandoto Sayansi Girls), Herieth Machunda (St Francis Girls Mbeya) na Daisy Mugenyi (Kifungilo Girls Tanga).

  Wavulana 10 bora
  Wavulana kumi waliofanya vizuri zaidi katika mtihani humo ni Moses Andrew Swai (Feza Boys), Daniel Maugo (St Joseph Millennium), Benjamini Tilubuzya, (Thomas More Machrina), Simon Mbangalukela (St. Joseph Millenium) na Nimrod Rutatora (Feza Boys). Wengine ni Simon Mnyele (Feza Boys), Paschal Madukwa (Nyegezi Seminary), Henry Stanlay (St Joseph Millenium), Fransisco Kibasa (Mzumbe) na Tumain Charles (Iliboru).
  Shule 10 bora
  Matokeo hayo yanaonyesha shule kumi bora zenye zaidi ya watahiniwa 40 kuwa ni St. Francis Girls ya Mbeya, Feza Boys, St Joseph Millenium, Marian Girls, Don Bosco Seminary, Kasima Seminary, St. Mary's Mazinde Juu, Canossa, Mzumbe na Kihaba.

  Matokeo hayo yanaonyesha pia shule 10 bora zenye watahiniwa chini ya 40 kuwa ni Thomas More Machrina, Feza Girls, Dungunyi Seminary, Maua Seminary, Rubya Seminary, St Joseph Kilocha Seminary, Sengerema Seminary, Lumumba, Queen of Apostles- Ushirombo na Bihawana Junior Seminary.
  Shule 10 za mwisho
  Shule kumi za mwisho zenye watahiniwa zaidi ya 40 ni Bwebwera, Pande Daraja, Mufindi, Zirai, Kasokala, Tongoni, Mofu, Mziwa, Maneromango na Kibuta. Na shule kumi za mwisho zenye watahiniwa chini ya 40 ni Ndongosi, St Luke, Igingwa, Kining'inila, Ndaoya, Kilangali, Kikulyungu, Usunga, Mto bubu day na Miguruwe. Waliofutiwa matokeo Dk Ndalichako alifafanua zaidi kuwa watahiniwa 3,301 waliobainika kufanya udanganyifu wamefutiwa matokeo na hawataruhusiwa kufanya mtihani wowote wa Necta kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.

  Dk Ndalichako alisema kati yao watahiniwa waliofanya mtihani huo walikuwa 426,314, sawa na asilimia 94.67 ya watahiniwa wote waliosajiliwa. "Mwaka 2010 watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 458,114 hivyo, idadi ya watahiniwa imepungua kwa watahiniwa 7,790 sawa na asilimia 1.70," alisema Dk Ndalichako. Alisema mwaka jana, watahiniwa wa shule waliosajiliwa walikuwa 349,39 na watahiniwa huku wa kujitegemea wakiwa ni 100,934. Akifafanua zaidi juu ya matokeo hayo, Mtendaji Mkuu huyo wa Necta alisema watahiniwa 450,324 walisajiliwa kufanya mtihani huo ambao wasichana ni 201,799, sawa na asilimia 44.81 na wavulana 248,525, sawa na asilimia 55.19. Alisema jumla ya watahiniwa wa shule 180,216 sawa na asilimia 53.59 ya waliofanya mtihani wa kidato cha nne wamefaulu, kati yao wasichana wakiwa 69,913 na wavulana 110,303.

  Kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea, waliofaulu ni 44,910 wasichana wakiwa 20,972 na wavulana 23,938.
  Waliofutiwa mitihani
  Dk Ndalichako alisema Necta imefuta matokeo ya watahiniwa 3,03 waliobainika kufanya udanganyifu kati yao, watahiniwa wa shule ni 3,301 na wawili wakiwa wa maarifa (QT). Akifafanua zaidi juu ya udanganyifu huo alisema , 182 walikamatwa na wasimamizi wakiwa na makaratasi (notes) sita walikamatwa na simu, watatu walikuwa wakifanyiwa mtihani na watu wengine, wanne walisajiliwa kufanya mtihani kwa majina ya watu wengine.

  Dk Ndalichako aliongeza kwamba, pia watahiniwa 2,896 karatasi zao za majibu zilikuwa na mfanano usio wa kawaida, 155 karatasi zao za majibu zilikuwa na miandiko zaidi ya mmoja, 14 kubadilishana karatasi katika chumba cha mtihani, 18 kukamatwa na karatasi za majibu zaidi ya moja, 25 wakiwa na mfanano usio wa kawaida wa majibu , kuwa na vikaratasi ama kubadilishana vikaratasi. "Mtu mmoja unakuta mitihani yake ya majibu ina miandiko zaidi ya 10, na jeshi la polisi ndilo lililothibitisha kuwa miandiko ya wanafunzi hawa ilikuwa inatofautiana. Alisema pia kuwa, baraza hilo limefuta matokeo ya watahiniwa nane walioandika matusi ya nguoni kwenye karatasi zao za majibu. "Kitendo cha kuandika matusi kwenye karatasi za majibu kinaonyesha utovu wa nidhamu, hivyo pamoja na kuwafutia matokeo ufuatiliaji zaidi unaendelea ili kuona hatua za kuwachukulia," alisema Dk Ndalichako.

  Pia alitoa onyo kali kwa vituo vilivyohusika na udanganyifu huo, huku akisema kwa vilivyobaika vitaandikiwa barua ya kutaka vijieleze kwa nini visifutiwe matokeo. Dk Ndalichako akielezea zaidi juu ya hali hiyo, alisema baadhi ya watahiniwa waliandika nyimbo za kizazi kipya (Bongo fleva) kwenye karatasi zao za majibu huku wengine wakichora michoro isiyo eleweka na wachezaji wa mpira. "Mwingine aliandika bongo fleva, ngoja niwasomee ‘wasahihishaji msinisamehe..., acha utani na girl wangu, najukuja home nakukuta.. nikifeli mtihani naendelea na fani ya muziki," Dk Ndalichako alisoma moja ya karatasi za majibu za watahiniwa hao huku akiruka baadhi ya maeneo akisema ameandika matusi yasiyoweza kusomeka.
  Ubora wa ufaulu kwa jinsi
  Dk Ndalichako alisema ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule unaonyesha kuwa, jumla ya watahiniwa 33,577 sawa na asilimia 9.98 wamefaulu katika daraja la kwanza mpaka la tatu.

  "Wasichana waliofaulu katika daraja la kwanza mpaka la tatu ni 10,313 sawa na asilimia 7.13 na wavulana ni 23,267, sawa na asilimia 12.13," alisema Dk Ndalichako. Aliongeza kwamba, waliopata daraja la nne ni 146,639 sawa na asilimia 43.60 ambao wavulana ni 87,039 sawa na asilimia 45.40 na wasichana 59,600, sawa na asilimia 41.22. Dk Ndalichoka aliongeza kwamba, waliofeli ni 0156,089 sawa na asilimia 46.41, kati yao wavulana wakiwa 81,418 sawa na asilimia 42.47 na wasichana wakiwa 74,667, sawa na asilimia 51.64. mwisho
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 20. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #20
  Feb 9, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mfumo kristo unawabeba ha ha ha ha ha ha.
   
Loading...