Aliyemuua bilionare Erasto

Aliyemuua bilionare Erasto

omoyo

Member
Joined
Oct 25, 2011
Posts
8
Reaction score
4
Hatimaye aliyemmiminia risasi 21 Erasto akamatwa ni mtu wake wa karibu sana na alishawahi fungwa miaka sita kwa ujambazi.

Watu waliomuua mfanyabiashara wa madini Erasto wamekamatwa. Watu hao ni mfanyabiashara mwenzake ambaye anaitwa Sharifu na watu wengine watatu. Inasemekana huyu sharifu ndiye aliyeratibu mauaji hayo kwa kusajili laini mbili za simu ambazo zilitumika kumuweka marehemu kwenye mtego wa kumuua. Alimrubuni mmasai mmoja ambaye ndie aliyesajili laini hizo kwa kitambulisho chake. Baada ya wana usalama kufuatlia mawasiliano ndipo yule masai alipokamatwa na baada ya mahojiano alijieleza kuwa sharifu alimwomba amsajilie lain kwa kitambulisho chake kwani yeye hakuwa na kitambulisho. Sharifu alinunua pikipiki mbili ambazo zilitumika kutekeleza mauaji. Sababu kubwa ya mauji haya ni ugomvi wa kugombania wachimbaji wadogo ambao mara nyingi huzama kwenye mgodi wa Tanzanite one na kuiba madini na hatimae kumuuzia Erasto na Sharif. Source- mtaani Mererani.
 
Hatimaye aliyemmiminia risasi 21 Erasto akamatwa ni mtu wake wa karibu sana na alishawahi fungwa miaka sita kwa ujambazi.

Naskia hadi sasa wameshakamatwa watu watatu..na wamemtaja aliewatuma na malipo walipewa 150M.
 
mmh! ni nani huyo? maana Arusha mtu akitaka kulipiza kisasi anakutoa uhai.
 
Sasa kwa taarifa zisizo rasmi mtu anayeaminika aliyemua erasto ni rafiki yake wa karibu mnoo na mfanyabiashara mwenzake wa mawe ustaadh shariff. Huyu yeye ndio alitoa hela za kufanyia kazi.
 
Kuweni wapole wakuu kwani kila kitu najaribu kuiweka sawa kabisa na nitakuja full kwani mambo yanaendelea barabara~~~~~~~~~~~na huyu Odhitas Sharif yeye asilimia 1OO% kama haki itatendeka hakika anaweza akalamba mvua nyingi sana~~~~~~~~Kaeni mtindo wa kula kwani kila kitu chaja.
 
mtu wake wakaribu? mke wake? mdogo wake? au?
 
Back
Top Bottom