TANZIA Aliyekuwa Askofu Mkuu wa TAG, Prof. Rainwell Mwenesongole wa Upanga CCC ametwaliwa na Bwana!

Kwa hiyo malengo makuu ya CCC ya kipindi hiki ni kuwa na miradi mikubwa ya kiuchumi kuliko kuhubiri injili tena?
Hongera zao!
Bora unisaidie kuuliza
Badala ya kuangalia kanisa linapanua VP huduma zake kufikia watu wengi zaidi wamjue Yesu
Watu wanawaza project zilizoavhwa na Mwwnisongole
Hawajui kanisa sii Mali ya mtu. Ni Mali ya Mungu
 
Pale TAG CCC Upanga kwanza anatakiwa aletwe Mchungaji Msomi ambaye ataendana na maono ya pale na awe na uwezo wa kuendesha project kubwa kubwa.

Askofu Mwenisongole ameondoka ameacha project ya ujenzi wa jengo la ghorofa floor 12, na ameacha limefikia floor ya tano, kwa hiyo Mchungaji atakayeletwa pale anatakiwa ahakikishe anakamilisha hiyo project.
Mpaka sasa hivi kanisa la TAG Upanga CCC lina thamani ya Shilingi Bilioni 8, mpaka ujenzi kukamilika thamani itafikia Shilingi Bilioni 15.
Mchungaji ysyote mwenye maono ya kazi ya Mungu na mwwnye nia ya dhati katika kumtumikia Mungu anawwza
Acheni propaganda
Mimi nashangaaa kanisa halijawahi kuwa Mali ya mtu ni Mali ya Mungu na washirika ndio waamuzi lakini wachungaji siku hizi ananunua kiwanja Cha kanisa anaandika jina lake inakuwa Mali yake Kwa sadaka za washirika
 
Lile kanisa la CCC upanga baada ya kifo Cha Mwenisongole linahitaji lipate Mchungaji toka makanisa makubwa yenye wasomi na viongozi wengi na ambayo kiongozi wake ana uzoefu mkubwa kwenye Mambo ya projects na jinsi ya kupata funds za projects kubwa

Pale wa kushika anafaaa awe Mchungaji Yared Dondo wa City Harvest au Askofu Mkuu mwenyewe Mtokambali Akubali kwenda Lile kanisa . Askofu mkuu Mtokambali analiweza bila shida Pia

Mwingine ninayemwona ana uwezo ni Mchungaji Rony Swai wa Dar es salaam Calvary Temple Lililoko Tabata

Askofu Mwenisongole kaacha kazi kubwa Bado kukamilika

Hao waombwe mmojawapo akashike pale .
Huu ndio ujinga wa watu wengi
Ndii maan wachungaji wameacha kuhubiri injili ya kwwli wanawaza pesa TU
Waumini nao hvyohvyo
Hivi mnamuelewa Mungu vizuri
Mungu anapangiwa watumishi?
Kwani hakuwa na uwezo wa kumuwwka mwwnisongole amalizie miradi? Mbona amemchukua
Kanisa limeacha kuangalia misingi halisi ya kuwafundisha watu kutubu na kumeudi a Mungu wachungaji na waumini wanWaza miradi
Nilitegemea watu waseme kazi kubwa aliyoicha Mwwnisongole ya kuifkisha injili vijijini inatakiwa impate mchungaji makini lakini badala yake
Hahahaha
 
Kuna taarifa kwamba aliyekuwa askofu mkuu wa TAG askofu Prof Rainwell Mwenesongole ambaye pia ni mchungaji kiongozi wa Upanga CCC amefariki dunia.

Taarifa zimetolewa na Sam Sasali wa Clouds tv katika ukurasa wake.

Updates;

Imethibitika ni kweli askofu Mwenesongole amefariki dunia usiku wa kuamkia leo na msiba uko nyumbani kwa marehemu eneo la Makonde Mbezi beach.

Hayati Mwenesongole ni baba mzazi wa mbunge wa Mbozi George Mwenesongole.
RIP kwa wafiwa ila huyu mzee nae nilianza kumsikia nikiwa shule ya msingi ,hivi hawa waheshimiwa wao hawana ukomo? kwani mara askofu mkuu TAG akaondoka mara papu mchungaji kiongozi CCC, wawe wanapumzika huu umungu mtu wa kuwa bila wao basi kanisa linakuwa si kanisa hauna tija, naona wengi wanajigeuzageuza tu mara askofu mkuu akitoka uaskofu mkuu anakuwa askofu wa jimbo yaani ni sawa na mtu alikuwa raisi ukiisha mhula wake anakuwa mbunge, akina Malasusa hadi leo wamekaza scrubu!
 
NaIfahamu shule kadhaa za sekindari za binafsi na za seeikali hapa Dsm wakati wa vipindi vyao vya dini hawana walimu wanaotoka makanisani kwenda mashuleni kufundisha dini
Watoto wanajiongoza ongoza TU ilimradi
Halafu wachungaji wamekaa TU makanisani kusubiri kuendesha miradi
Wanaona watoto hawana sadaka wanawaacha
Badala ya kuvuna roho zao Sasa
Biblia inaswma mles mtoto katika njianimpasayo .. ...
Halafu maadili yameporomoka
Wazazi hatuna maadili vyote hvyo hawavioni wanangangania miradi
Wengine wanasubiriu kuuza maji ya upako
Wachungaji angalieni roho za watu zaidi mengine mtazixishiwapppp
 
Acha uzembe ndugu yangu.
Mtumishi wa Mungu ni binadamu wa kawaida kabisa, anaishi na wanadamu, na amejaa udhaifu mwingi kama walivyo binadamu wengine, hana kitu kingine cha ziada kuliko mwanadamu mwingine yoyote, lakini amepewa nafasi ya kuwatumikia watu chini ya utaratibu wa Mungu.

Kama kuna mambo mtumishi wa Mungu anayafanya sirini basi hayo atajuana na Mungu wake lakini yale anayoyafanya hadharani ni mambo yetu na tuna haki ya kuyapima na kuyahukumu. Hiyo ni kazi yetu sisi wanadamu.

Biblia inasema, watumishi halisi wa Mungu tutawapima (tutawahukumu) kwa matunda (matendo) yao. Hivyo sisi hapa tunayo haki kwa 100% kumhukumu Askofu Mwanisongole kwa matendo yake. Kwenye suala la kutetea haki za watanzania waliokuwa wanaonewa vikali na serikali ya Magufuli, bila shaka Askofu Mwanisongole aliamua kukaa kimya au kuungana na watawala kwa kuwapongeza. Askofu Mwanisongole hawezi kulikwepa hili, na huko aliko litamfuata.
usihukumu na wewe urahukumiwa
 
Mchungaji ysyote mwenye maono ya kazi ya Mungu na mwwnye nia ya dhati katika kumtumikia Mungu anawwza
Acheni propaganda
Mimi nashangaaa kanisa halijawahi kuwa Mali ya mtu ni Mali ya Mungu na washirika ndio waamuzi lakini wachungaji siku hizi ananunua kiwanja Cha kanisa anaandika jina lake inakuwa Mali yake Kwa sadaka za washirika
Mwongo mkubwa wewe huwezi andika jina lako kiwanja Cha kanisa hutapata vibali vya ujenzi toka serikalini

UKijenga kanisa vibali vyote vya ujenzi lazima visomeke jina la kanisa na hutolewa ukishaambatanisha hati ya kiwanja yenye jina la kanisa

Au wewe unaongekea makanisa ya makuti ? Nani akupe kibali Cha kujenga kanisa kiwanja binafsi? hayupo.

Ukienda TU kuomba kibali Cha ujenzi wa kanisa lazima upeleke hati ya kiwanja inayosomeka jina la kanisa sio Jina lako binafsi Au la mkeo
 
Hela ya waumini,kanisa la Mungu linakuwa kanisa la mtu binafsi,huu ndio ujasiriadini.
La binafsi kivipi wakati hati zote haziko kwenye jina lake binafsi ziko Kwa jina la kanisa.Na akaunti zote za Benki ni za kanisa na zinasomamiwa na uongozi wa kanisa ? Hujui hata unachoongea
 
Bora unisaidie kuuliza
Badala ya kuangalia kanisa linapanua VP huduma zake kufikia watu wengi zaidi wamjue Yesu
Watu wanawaza project zilizoavhwa na Mwwnisongole
Hawajui kanisa sii Mali ya mtu. Ni Mali ya Mungu
Mungu aliyeagiza watu waokoke ndie huyo huyo ialiyeagiza kuijengewa mahekalu mazuri Ya kumwabudia
Kanisa linalojengwa si Mali binafsi ya mtu ni Mali ya Kanisa na Lina hati zote za kanisa sio binafsi

Kwa taarifa yako hata ukitoa kiwanja kanisa lijengwe utawajibika kwanza kubadili hati ya kiwanja isomeke jina la kanisa kabla kupata kibali Cha ujenzi toka serikalini

Hizo porojo za kusema sijui za kujenga kanisa la mtu ni habari za vijiweni kajaribu wewe kuomba vibali vya ujenzi wa kanisa kwenye kiwanja chako binafsi utagomewa utaambiwa badili jina na matumizi kwanza kisomeke Cha kanisa Kwa jina la kanisa na badili matumizi kutoka kuwa kiwanja Cha matumizi binafsi kuwa Cha kanisa
 
Ndugu yangu, acha kujifanya hujui yanayoendelea huko makanisani.

Nani asiyejua kuwa karibu 90% ya haya makanisa yamejengwa mitaani kwenye mazingira ya makazi ya watu na hakuna suala la vibali wala nini.

Nani asiyejua kuwa mengi ya haya makanisa yalipo sasa hapo awali yalikuwa yanatumika kwa shughuli zingine kisha yakabadilishwa matumizi. Mengine talikuwa magodauni, vilabu vya bonge, gereji, nyumba za watu nk.

Nani asiyejua kuwa mengi ya haya makanisa/madhehebu yalisajiriwa kama mali ya mtu (huduma yake binafsi) na ujenzi wa kanisa unabakia kuwa mali ya huduma, na huduma ni mali yake.
 
RIP kwa wafiwa ila huyu mzee nae nilianza kumsikia nikiwa shule ya msingi ,hivi hawa waheshimiwa wao hawana ukomo? kwani mara askofu mkuu TAG akaondoka mara papu mchungaji kiongozi CCC, wawe wanapumzika huu umungu mtu wa kuwa bila wao basi kanisa linakuwa si kanisa hauna tija, naona wengi wanajigeuzageuza tu mara askofu mkuu akitoka uaskofu mkuu anakuwa askofu wa jimbo yaani ni sawa na mtu alikuwa raisi ukiisha mhula wake anakuwa mbunge, akina Malasusa hadi leo wamekaza scrubu!
Ndugu yangu mambo yote ni pesa tu, wanakamua mpaka uzeeni, na wote wanabanana mjini tu.

Kuna mamia ya vijiji hapa Tz kumejaa upagani na wachungaji hawataki kwenda huko, wachungaji wengi wamebakia mjini kunyang'anyana kondoo walionona tu.
 
Neno hayati linatumiwa kwa wanajeshi na amir jeshi mkuu na wasaidizi wake wawili yaani makamu na waziri mkuu.

Wengine wote ni marehemu kwa heshima zao hapa duniani
Yaani binadamu kqa ubaguzi, mpaka marehemu tumewapa madaraja. Kuna marehemu daraja la heshima na marehemu kajamba nani.

Lakini wote wanaenda kuoza na kuwa fossils.
 
Ndugu yangu, acha kujifanya hujui yanayoendelea huko makanisani.

Nani asiyejua kuwa karibu 90% ya haya makanisa yamejengwa mitaani kwenye mazingira ya makazi ya watu na hakuna suala la vibali wala nini.

Nani asiyejua kuwa mengi ya haya makanisa yalipo sasa hapo awali yalikuwa yanatumika kwa shughuli zingine kisha yakabadilishwa matumizi. Mengine talikuwa magodauni, vilabu vya bonge, gereji, nyumba za watu nk.

Nani asiyejua kuwa mengi ya haya makanisa/madhehebu yalisajiriwa kama mali ya mtu (huduma yake binafsi) na ujenzi wa kanisa unabakia kuwa mali ya huduma, na huduma ni mali yake.
Unaongekea mambo ya zamani ambayo Kwa sasa hayana uhalisia Kwa asilimia 90 Kwa pande zote Kwa makanisa na misikiti .

Pili kumbi ziko Kwa ajili ya kukodiwa Kwa sherehe,au ibada hivyo usishangae kukuta ukumbi unatumiwa Kwa ibada Na pili godown kubadilishwa jengo la ibada pia si ajabu ni taratibu TU kufuatwa mfano kanisa la Efatha pale Mwenge ni kanisa kubwa sana lililonunua magodown na kubadilishwa na kupata vibali yatumike kama kanisa

Hata baa kubadilishwa kanisa au msikiti ni jambo zuri kwanza unaondoa haramu na kuweka halali na Kwa sababu lilikuwa jengo la watu wengi yaani walevi kulibadili kuwa kanisa wala sio kazi kubwa Kwa sababu tayari lilikuwa likitumiwa na watu wengi likiwa na huduma nyingi za kuhudumia watu wengi kama vyoo nk ni jengo la jamii ya watu wengi.Na ingependeza sana baa nyingi zigeuzwe kuwa majengo ya kuabudia
 
Ndugu yangu mambo yote ni pesa tu, wanakamua mpaka uzeeni, na wote wanabanana mjini tu.

Kuna mamia ya vijiji hapa Tz kumejaa upagani na wachungaji hawataki kwenda huko, wachungaji wengi wamebakia mjini kunyang'anyana kondoo walionona tu.
Nafikiri hata Biblia huijui vijijini kwenye upagani wanaotakiwa kwenda ni wainjilisti sio wachungaji!!

Eneo lenye upagani mwingi anayetakiwa kwenda ni mwinjilisti naona huelewi hata mpangilio wa huduma katika mwili wa Kristo Na kazi zao
 
Pamoja na mambo yote aliyowahi kuyafanya, huyu Askofu hakuwa muadilifu kwa jamii kwa kipindi chote cha utawala wa Magufuli.

Huyu Askofu, yeye binafsi na kanisa lake la TAG waligeuka kuwa waongo na wanafiki ili kujipendekeza kwa Magufuli. Hawa maaskofu wa TAG na wapentekoste wengine ndio walifikia hatua ya juu ya unafiki ya kumuita na kumpa tuzo ya uadilifu Magufuli!

Wakati watanzania wakiuwawa, wakiteswa, kudhulumiwa na kufanyiwa kila ubaya na utawala wa Magufuli, huyu askofu na wenzake walikuwa kimya au kumimina pongezi kwa Magufuli.

Kwangu binafsi ninapenda kusema huyu Marehemu hakuwa tena na mchango wowote kwa jamii ya watanzania labda kwa dini yake.

Ninatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu, lakini ninasikitika kusema hapa kuwa, Marehemu hakuwa tena na faida yoyote kwetu kijamii, na bora amepumzika.
Magufuli alitesa na kuua akina nani hao, lini na wapi? Thibitisha hilo kwanza. Mimi nikiropoka mbowe ni mbakaji haiwezi kua kweli mpaka nithibitishe unakaji wake.
 
Back
Top Bottom