Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,792
- 11,952
Habari zilizotufikia ni kwamba Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, Jaji Mark Bomani amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Septemba 11, 2020, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mtoto wake amethibitisha kifo hiki. Shughuli za msiba zipo nyumbani kwa Marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Jaji Mstaafu Mark Bomani enzi za uhai wake akiwa na mkewe wakikata keki katika hafla ndogo ya kusherehekea miaka 50 ya ndoa yao mwaka 2017
UPDATE 14-09-2020: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aongoza mazishi
--
WASIFU WAKE KWA UFUPI
Mark Danhi Bomani alizaliwa Januari 2 1932, Bunda, mkoani Mara.
Mark alikuwa kati ya watoto kumi wa Mzee Bomani ndugu zake wengine wakiwa Daniel, Paul, Emma, Francis, Martha, Yona, Washington, Phoebe & Neema.
Mark Bomani alisoma shule ya msingi Mwamanyili, Nassa ambapo baba yake mzazi ndiye alikuwa mwalimu wake. Baada ya kumaliza shule ya Msingi, alijiunga na shule ya Bwiru Boys ambapo alisoma mpaka darasa la 10 na baadae alifaulu kuendelea na masomo ya secondary katika shule mashuhuri ya Tabora Boys. Baada ya kufaulu kidato cha 6, Mark alichaguliwa kwenda chuo cha Makerere College nchini Uganda.
ELIMU:
1953 – 1957B.A (Politics, Economics and History), Makerere University, Uganda
1957 – 1958: Diploma in Social Welfare Policy, Institute of Social Studies, The Hague.
1958 – 1961: Bachelor of Laws (LLB), London University
1961: Barrister -at-Law, Lincoln’s Inn, London
KAZI:
1954: Mwakilishi wa Makerere Student’s Guide kwenye Mkutano wa Kimataifa (International Union of Students Conference), Prague, Czechoslovakia.
1959: Kiongozi wa Umoja wa Wanafunzi wote kutoka Tanganyika (Tanganyika Students Association), Makerere University
1962: Wakili wakujitegemea katika mkoa wa Mwanza
1963: Wakili wa Serikali. Akateuliwa na J.K. Nyerere kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu
Katika kazi ya mwanzo aliyoifanya katika cheo chake kipya ilikuwa ni kusaidiana na Mwanasheria Mkuu Roland Brown kutayarisha nyaraka zote za kisheria za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
1963: Alishiriki katika utayarishaji wa Mkataba wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (Charter of the African Development Bank), Casablanca, Morocco.
1963: Mjumbe katika ujumbe wa Tanganyika uliokwenda Addis Ababa, Ethiopia kuandaa mkataba wa nchi huru za Afrika (Charter of the Organization of African Unity)
1964: Mjumbe wa Kamati ya Wajumbe wa Nchi za Afrika ya Mashariki iliyoundwa kwa madhumuni ya kuangalia uwezekano wa kuunda Shirikisho la Afrika ya Mashariki
1964: Mjumbe wa Tume ya Rais iliyoundwa ili ipendekeze mfumo mpya wa Kidemokrasia wa Chama kimoja. Mapendekezo ya Tume hiyo ndiyo yaliyokuwa Msingi wa mfumo wa Chama kimoja cha Siasa
1965– 1976: Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa kwanza mwananchi. Kati ya mambo ya kwanza aliyoshughulikia nikutafuta majaji na mahakimu kutoka nchi za nje ambao waliajiriwa na serikali ya Tanzania katika kipindi ambapo majaji na mahakimu wengi walikuwa wazungu au wahindi. Kati ya watu aliyowachagua ni pamoja na Telford Georges kutoka Trinidad & Tobago aliyekuwa Jaji Mkuu.
1965: Mbunge na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya TANU
1967– 1976: Mjumbe wa Kamati iliyoundwa kwa madhumuni ya kupendekeza mfumo mpya wa ushirikiano kati ya nchi za Afrika ya Mashariki. Hatma yake ilikuwa kuundwa kwa Jumuiya ya Afrka Mashariki (East African Community)
1974: Mshauri wa FRELIMO katika kuandaa Katiba mpya ya Msumbiji na utaratibu wa Serikali yake
1976: Baada ya kuombwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Rais J.K. Nyerere alimruhusu Mark Bomani kujiunga na Utumishi wa Umoja huo kwa madhumuni maalum ya kusaidia katiak matayarisho ya Uhuru wa Namibia.
1976: Naibu Mkurugenzi (Deputy Director), U.N Institute for Namibia, Lusaka, Zambia
1978: Baada ya kuombwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kuwa mshauri wake wa mambo ya kisheria, Mark Bomani alikwenda Namibia na Afrika ya Kusini kuzungumzia juu ya utaratibu wa kukabidhi madaraka kwa wananchi. Taarifa ya mapendekezo ya ujumbe huo ndiyo iliyowezesha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha Azimio Na 435 ya mwaka 1978 ambayo hatimaye yalileta uhuru wa Namibia.
1990: Mark Bomani aliandaa katiba mpya ya Namibia baada ya kupata uhuru
1991: Mark Bomani aliombwa kuwa Jaji Mkuu wa Namibia lakini badala yake akaomba awe mshauri wa masuala ya Sheria na Katiba kwa miaka miwili tuu akiamini kwamba muda huo ungetosha kabisa kutoa mchango wake kwa wana-Namibia.
1992: Bomani aliteuliwa na Rais Mwinyi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Wataalam wa Zanzibar na wa Tanzania Bara iliyoundwa kutoa mapendekezo juu ya namna ya kumchagua Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na mgawanyo wa madaraka kati yao na Bunge. Rais Mwinyi pia alimteua Mark Bomani kuwa Jaji.
1993: Mwenyekiti wa Kamati Maalum (Legal Task Force) iliyopewa jukumu la kukarabati sekta yote ya Sheria nchini, chini ya mradi wa Benki ya Dunia, Wahisani mbalimbali.
1993:1995: Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
1993: Mwenyekiti wa Tume ya Utangazaji
1995: Bomani ajitosa siasa kuomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi kuwa mgombea Rais.
1995:
Baada Mwalimu Nyerere kuchaguliwa kuwa Mpatanishi wa mgogoro wa Burundi na Umoja wa Mataifa na OAU, Nyerere akamuomba Bomani kuwa msaidizi wake kazi aliyoifanya mpaka Mwalimu Nyerere alipofariki mwaka 1999. Baada ya Nelson Mandela kuchaguliwa kuwa mpatanishi mpya, Bomani akawa msaidizi wake na kwa pamoja wakaweza kufanikisha azma ya kupatanisha pande husika mnamo Agosti 2000.
2007:
Rais Kikwete alimteua Bomani kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya watu 12 kupitia upya sera ya madini.
2018:
Mwenyekiti wa CCM, John J.P. Magufuli alimteua kuwa mmoja wa wajumbe watano wa Bodi ya Kwanza ya Udhamini ya CCM.
Mark Bomani aliendelea na shughuli za uwakili kupitia kampuni yake ya Bomani & Company Advocates. Mark Bomani alikuwa mkurugenzi na muanzilishi wa kampuni ya Serengeti Breweries. Pia alikuwa mkurugenzi wa Bodi ya Benki ya NCBA.
Baadhi ya mada kuhusu Jaji Bomani
> Jaji Mark Bomani: Serekali 2 au 3 zisijadiliwe kwenye Bunge la Katiba!
> Jaji mstaafu Mark Bomani naye atoa mpya..
> Jaji Mstaafu Mark Bomani akataa Tanzania kuitwa Tanzania Bara, ataka iitwe Tanganyika
> Jaji Mark Bomani: Ni vizuri kukawepo kura ya maoni kuhusu Muungano (Referendum)
> Jaji Mstaafu Mark Bomani aunga mkono Serekali 3 asema wasemao ni harama hawana mashiko
> Muungano lazima ujadiliwe kwa Ukweli na Uwazi! - Jaji Mark Bomani
> Jaji Bomani: Wageni wanaimaliza nchi kupitia sekta ya madini
> Jaji Bomani apigilia msumari Katiba Mpya
> Jaji Bomani: ZEC imejipunguzia imani
> Jaji Bomani awachafua wazanzibari
> Bomani: Gamba litapasua CCM