TANZIA Aliyekuwa Askofu Mkuu wa TAG, Prof. Rainwell Mwenesongole wa Upanga CCC ametwaliwa na Bwana!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,940
141,915
Kuna taarifa kwamba aliyekuwa askofu mkuu wa TAG askofu Prof Rainwell Mwenesongole ambaye pia ni mchungaji kiongozi wa Upanga CCC amefariki dunia.

Taarifa zimetolewa na Sam Sasali wa Clouds tv katika ukurasa wake.

Updates;

Imethibitika ni kweli askofu Mwenesongole amefariki dunia usiku wa kuamkia leo na msiba uko nyumbani kwa marehemu eneo la Makonde Mbezi beach.

Hayati Mwenesongole ni baba mzazi wa mbunge wa Mbozi George Mwenesongole.
 
RIP askofu.
Huyu ni miongoni mwa maaskofu wa kipentekoste aliyekuwa muadilifu sana katika masuala ya imani.
Kanisani kwake upanga miaka hiyo ya 1991 ndipo palipokuwa na ibaada mbili kwa jumapili yaani ya kiingerza na ya kiswahili.
Wengi wa maofisa wa balozi nyingi nchini waliokuwa walokole walisali kanisani kwake.
 
Sijawahi kumsikia huyu
Naona alikuwa sio mtu wa siasa na dini
Alikuwa kiongozi mkubwa serikalini kabla ya kuacha kazi kwa hiari bila kustaafishwa wala kutumbuliwa akaenda kufanya kazi ya uchungaji
Zamani watu waliacha kazi kuwa wachungaji tofauti na sasa ambapo jobless hutafuta kuwa wachumgaji

Wachungaji. Wengi wa kilokole watu wazima wengi waliacha kazi zao nzuri TU kuwa wachumgaji watu kama Moses Kulola alikuwa architect

Mtume Maboya alikuwa Askari

Mtume na Nabii Mwingira alikuwa kiongozi KKKT
Moses Magembe alikuwa doctor nk

Kwa Sasa makanisa karibu yote makubwa kwa madogo yawe Katoliki,KKKT , Anglican, Pentecost nk yanachukua ma jobless na kuwapa uchungaji au upadri
Yesu hakuchukua mtu yeyote jobless na kumfanya mtume wote aliowaita walikuwa na kazi Zao za kuwaingizia vipato vya uhakika

Mwenisongole ni mmojawapo aliyeitwa ki kweli kweli akaacha kazi nzuri kwenda uchungaji
 
Neno hayati linatumiwa kwa wanajeshi na amir jeshi mkuu na wasaidizi wake wawili yaani makamu na waziri mkuu.

Wengine wote ni marehemu kwa heshima zao hapa duniani
Haya sawa twende hivi: hayati ibilisi joka kuu.
 
Alikuwa kiongozi mkubwa serikalini kabla ya kuacha kazi kwa hiari bila kustaafishwa wala kutumbuliwa akaenda kufanya kazi ya uchungaji
Zamani watu waliacha kazi kuwa wachungaji tofauti na sasa ambapo jobless hutafuta kuwa wachumgaji

Wachungaji. Wengi wa kilokole watu wazima wengi waliacha kazi zao nzuri TU kuwa wachumgaji watu kama Moses Kulola alikuwa architect

Mtume Maboya alikuwa Askari

Mtume na Nabii Mwingira alikuwa kiongozi KKKT
Moses Magembe alikuwa doctor nk

Kwa Sasa makanisa karibu yote makubwa kwa madogo yawe Katoliki,KKKT , Anglican, Pentecost nk yanachukua ma jobless na kuwapa uchungaji au upadri
Yesu hakuchukua mtu yeyote jobless na kumfanya mtume wote aliwaita walikuwa na kazi Zao za kuwaingizia vipato vya uhakika

Mwenisongole ni mmojawapo aliyeitwa ki kweli kweli akaacha kazi nzuri kwenda uchungaji
Correction: Moses Kulola alikuwa mwalimu by profession na sio architect.
 
Asante kwa ufafanuzi huu
Sikuyajua yote haya
 
Back
Top Bottom