Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,178
- 7,320
Miujiza mingine mingine imeshuhudiwa huko Samunge jana baada ya mtu mmoja kuripoti kwa babu kuwa ameibiwa pochi na simu. Babu alimwambia mtu huyo ambaye ni Mkenya kuwa asiwe na wasiwasi, kwani atarudishiwa vitu vyake. Babu alitangaza na kuomba aliyechukua vitu hivyo arudishe, lakini hakuna aliyejitokeza. Hapo ilibidi Babu apige maombi mafupi, ambapo muda mfupi baadaye alijitokeza mtu mmoja akiwa na vitu hivyo na kuomba msamaha.
Alipohojiwa alisema kuwa baada ya maombi ya Babu, alianza kuhisi kupewa kipigo na vitu/watu asiowaona, na kuanzia hapo akaanza kupoteza nuru ya kuona, ndipo alipoamua kwa haraka kurudisha vitu hivyo kabla hali haijazidi kuwa mbaya...