Aliyeandika Mashairi, Mtihani wa NECTA Ahojiwa Clouds FM

Hana tofauti na akina Happy Skilful wanao nunua mtihani !

Mtoto Julius nimemsikiliza kwa makini sana, kwa ufupi he is very very bright. Kwani haoni
kwa nini tung'ang'anie vitabu vya Marx na Lenin (DS) wakati vipaji vya watoto wetu tunavididimiza
kana kwamba elimu ya PhD na vyeti ndiyo kitu pekee na bora duniani. Tuwaangalie akina Abort, Davinci, wavumbuzi mbali mbali akiwemo Jobs (Wa APPLE electronics like i-phones) je, walikwenda shule ya kuwa wavumbuzi?
Pia Archimedes, n.k.

Kwa anayeijua historia ya mapinduzi ya maendeleo atakubaliana na mimi kuwa mwanzo wa mapinduzi hayo
huwa haukubaliki na watu kama akina Dr. J.Ndalichako. Ila hukimbilia kuitangazia dunia kuwa akina Julius
wamekwenda kinyume na maendeleo. Hata Sauli hakuukubali utume wa Yeshua hadi alipopewa stop.

Hata wavumbuzi wa kwanza wa filamu (moving pictures) walikasirikiwa sana na wazungu wenzao baada ya kuwa
sababishia kukanyagana ktk ukumbi baada ya kuonyeshwa kipande cha treni iliyokuwa ktk mwendo. Wale
watazamaji walikimbia toka ktk holi na kukanyagana wakiamini kuwa treni ile ilikuwa halisi (live).
 
Mtoto Julius nimemsikiliza kwa makini sana, kwa ufupi he is very very bright. Kwani haoni
kwa nini tung'ang'anie vitabu vya Marx na Lenin (DS) wakati vipaji vya watoto wetu tunavididimiza
kana kwamba elimu ya PhD na vyeti ndiyo kitu pekee na bora duniani.
Tuwaangalie akina Abort, Davinci, wavumbuzi mbali mbali akiwemo Jobs (Wa APPLE electronics like i-phones) je, walikwenda shule ya kuwa wavumbuzi?
Pia Archimedes, n.k.

Mkubwa mimi hapa sijakupata kabisa, hebu nifafanulie kidogo... una maada kuwa kwa kusoma vitabu vya Marx tunadidimiza vipaji vya watoto au ???? Una maana kwamba ili nasi kwetu watoke kina Jobs tusiwapeke shule watoto wetu au????
 
Mmmmh!

images(7).jpg
 
Jobs (Wa APPLE electronics like i-phones)
Wakati mwingine tunapoteza watoto wakadharau shule kwa kutumia vigezo ambavyo vingine siyo kweli. Ingawa Steve Jobs hakwenda shule, lakini alitumia watu waliokwenda shule katika kuvumbua hizo electronics. Yeye alikuwa na kipaji cha biashara kiasi kuwa aliweza kujua ni bidhaa gani atengeneze ambayo watu watapenda. Halafu anawatumia mainjinia kumtengezea bidhaa hiyo. Injinia wake wa kwanza kabisa aliyemtengenezea ile compyuta ya Apple 1 ni Steve Wozniak.

Miaka yote ya maisha yake Steve anasifika kwa kuwa visionary wa kufikiria product ya kuingiza sokoni, halafu akawatumia watu wa kudesign na kutengezea bidhaa hiyo, ambao ni watu waliosmomea fani ya electronics.

dunia ya leo bila elimu hatuendi popote; tusijirudishe katika miaka hiyo ya zamani kwa kudaia kuwa kama Steve aliweza bila elimu, basi na wewe uote kuwa utaweza bila elimu; chances za nama hiyo ni ndogo sana.
 
Nilimsikiliza kwa makini sana! Nikiwa kama mtu aliyepita pita kwenye saikolojia na uchumi, Namuunga mkono. Moja ya kauli zake ni "WAZAZI WANATUMIA HELA NYINGI KUWATENGENEZEA WATOTO WAO UMASIKINI". Kwa kuweka msisitizo kwenye elimu ya vitabuni, Taifa limekuwa na wahitimu wengi wasiopata nafasi za kuajiriwa. Hali hii huwafanya wahitimu kuwa na maisha duni.
Nasikitika sana!, tena sana kwa kuwa watu wnapindisha mtizamo wa Julius. Julius anataka kuwe na shule ambazo zitatoa elimu ya sanaa kama muziki, mpira, n.k sambamba na elimu ya vitabuni. Uchumi wa dunia ya leo unategemea huduma, sio viwanda kama zamani kidogo. Mataifa mengi yanapata faida kubwa kwa kutoza kodi kwenye huduma za sanaa kama maigizo, muziki n.k.
Huu mfumo wa elimu ya kukremu haitusaidii kitu. Wote tunawwajua waimbaji, wanamichezo n.k wa hapa Tanzania wenye mafanikio makubwa kwa jitihada zao binafsi, ila kwa sasa wanatoa ajira na kuchangia pato la Taifa.
Nimewahi kupita Makongo High School. Pale Makongo kuna wanafunzi 'vilaza' kabisa, lakini kwa kuwa wanavipaji, wamepewa nafasi za kusoma, si mnawafamu Dogo Janja n.k.
Aliendelea kwa kusema, "mimi si wa kwanza kuandika, nenda kaulize Baraza la Mitihani utaambiwa", yeye anaonekana kwa kuwa ametangazwa kwenye vyombo vya habari. Pia alisema, "kama nikakaa kimya, tutakaa kimya mpaka lini?"
LET US THINK CRITICALLY, SIO KUWA WATUMWA WA VITABU.
 
Ndio! Julius ni shujaa kwa kuwa amethubutu kusema na kutetea ukweli hadharani. Najua ukweli unauma, hasa ukweli unakosoa mfumo mbovu. Na watu wengi hulaumu bila ya tafakari ya kina.
 
Kama hivyo ndivyo alivyosema huyu kijana, basi ana akili kulika asilimia kubwa sana ya viongozi wetu. Na kama ameongea bila kua amesoma sehemu, yani ni fikra zake tu basi ni mwerevu zaidi.

Robert Kiyosaki alisema "if children studied what they were interested in, they would find their geniuses and succeed."

“It is said that the fear of public speaking is a fear greater than death for most people. According to psychiatrists, the fear of public speaking is caused by the fear of ostracism, the fear of standing out, the fear of criticism, the fear of ridicule, the fear of being an outcast. THE FEAR OF BEING DIFFERENT PREVENTS MOST PEOPLE FROM SEEKING NEW WAYS TO SOLVE THEIR PROBLEMS.”
 
Sioni ubaya , adhabu ya mitihani iwe kufail tu siyo kingine maana hata Rwambo Franco M, hakwenda shule
 
Back
Top Bottom