Aliye Juu Mngoje Chini ! ?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliye Juu Mngoje Chini ! ??

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Goodrich, Mar 17, 2012.

 1. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Tangu nilipokuwa shule, mara ya kwanza kusikia msemo Aliye juu mngoje chini nilitatizika sana.
  Sikuelewa mtunzi wa msemo huu alikuwa na kinyongo, wivu au kukata tamaa.
  Hata hivyo niliishia kuamini kuwa muasisi wa msemo huo alijikubali kuwa yeye ni wa daraja la chini siku zote.

  Nadhani msemo ungependeza kama ungekuwa;
  Aliye Juu Mfuate Juu au
  Aliye Juu Muulize Kafikaje nawe ufike Juu.

  Sijui wenzangu mnaonaje?
   
 2. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Yaani kuntu kabisa, Alie juu mfuate huko huko juu, au mie huwa nina mawazo mengine kama mtu anakuudhi sana , ana madharau kwa kuwa anajiona yeye matawi ya juu basi huwa nasema ALIE JUU NITAKUTANA NAE KATI KATI WAKI YEYE ANASHUKA MIMI NAPANDA... lakini hii mara nyingi huwa inatokea kama mtu yupo juu anakuvuruga na kukutolea dharau other wise ALIE JUU MUOMBEE MUNGU AMZIDISHIE NA WEWE AKUPE ZAIDI.
   
 3. amanindoyella

  amanindoyella Senior Member

  #3
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Aliye juu msubiri chini ukiona anakawia mfuate juu!
   
 4. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,828
  Trophy Points: 280
  He was right, why should you waste resources for something that nature/somebody/(somewhere) will provide it for free
   
 5. Straddler

  Straddler JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Aliye juu, mshushe chini..!!:lol:
   
 6. M

  Martinez JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 518
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  Aliye Juu, Muulize Kafikaje ?
   
 7. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Nayo njema! Badala ya kumngoja chini
   
 8. M

  Martinez JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 518
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  Ili iweje ?
   
 9. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo umekaa chini unamsubiri. Fanya kazi, uwe kama yeye !
   
 10. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,491
  Likes Received: 4,764
  Trophy Points: 280
  Be Nice to the People on your way up as you might meet them on your way down
   
 11. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Mkuu CHUAKACHARA ungelitumia Kiswahili ingependeza.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Thats the problem. You are focused on the way down !!!
   
 13. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #13
  Nov 25, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Thats the problem. You are focused on the way down !!!
   
 14. p

  prince pepe JF-Expert Member

  #14
  Nov 27, 2012
  Joined: Sep 4, 2012
  Messages: 215
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unataka kusema hata mkokoten nao uwe mkokofote?
   
 15. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #15
  Nov 27, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,738
  Likes Received: 8,316
  Trophy Points: 280
  Mh...msemo huu ulikuwa fundisho kwa wale waliopata madaraka ulani na wanayatumia vibaya/kuumiza wenzao.
  Hivyo, ni kumbusho tu kwa wale wanaoonewa (waliochini) kwa usihangaike kumloga, kumkaidi, kupoteza muda wako kujaribu kumshusha..,mwisho wa siku atarudi chini tu kwani wazungu wanasema, "Corruption may take you to the top, but it takes character to keep you there"
  Haimanishi, ukae chini unamgoja ashuke halafu basi. Kwani pia walisema, "mvumilivu hula mbivu" na "mchumia juani hulia kivulini" endelea kuchumia huko juani kwani ama kwa hakika wakati atakaposhuka, Mungu atakupandisha kwa halali...
   
 16. kidde I'm

  kidde I'm Member

  #16
  Nov 29, 2012
  Joined: Nov 28, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  safi huo ni mtazamo wako mzuri sana, lakini tambua kuwa hiyo ni methali na methali huwa na lugha ficho iliyobeba hekima ndani yake katika lugha ya kiswahili kuna maana mbali mbali kwa baadhi ya maneno au sentensi kuna maana ya msingi na ile ambayo mzungumzaji huibaini, maana halisi ya aliyejuu ................ ni kwamba mfano watu wawili wenye nguvu wanapigana basi mmoja lazma ashuke/awe mpole kuepusha utata zaidi, hivyo ashuke na kumsubiri ashuke (apunguze hasira wataelewana)
  Haya ndio maono yangu wewe Je?
   
 17. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #17
  Nov 29, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Kweli hilo nalo neno, msemo wa mkosaji.
   
 18. mshana jr

  mshana jr JF-Expert Member

  #18
  Nov 29, 2012
  Joined: Aug 19, 2012
  Messages: 81,517
  Likes Received: 81,736
  Trophy Points: 280
  ndugu yangu hiyo ni misemo ya hekima na tunu ya lugha yetu adhimu ya kiswahili, tafsiri yake si ya moja kwa moja kama wengi wanavyofikiri ipo mingine mingi tu kama chelewa ufike,fimbo ya mbali,mtaka cha uvunguni, asifiaye mvua ,nk nk
   
Loading...