Alisafiri kamkuta mkewe ana mimba ya mtu mwingine

Alipima ukimwi na kujikuta salama lakini kuhusu mimba alitaka mumewe arudi waamue la kufanya.

Huyu dada mwehu au alitaka kumpa presha za bure mume wake, kama hakuwa ameambukizwa ukimwi na kwa kusubiri uamuzi wa mume wake inamaana yupo tayari pia kutoa hiyo mimba, sasa alimsubiri mume wake ili iweje? kwani angetoa tu hiyo momba na kutulia ili asimuumize roho mume wake angekosa nini? Mshauri jamaa aachane na huyu mwehu atakuja kumuua kwa presha tu, akimuacha kwa hili siku nyingine atakuja kugongwa na mtu akaja kumuelezea jamaa yake kisha aombe msamaha.
 
Utakubalije kwanza kutoka out kama mume wako hayupo, tena usiku?? Kwa kuonyesha upendo miezi sita si mingi kwa kumsubiri umpendaye, kwani maeneo ya starehe huwa yana vishawishi vyake, so angekaa mbali nayo.

Pili utakubalije offer ya mwamume usiyemfahamu vizuri. Hayo ni matokea ya free lunches!!! Tuache kupenda dezo, zina madhara makubwa!!!
 
Kuna Mnamibia tulikuwa nae kwenye kozi ya miezi 6 America ya kusini baada ya kurudi nyumbani kanipigia simu mkewe ana mimba ya mtu mwingine ya miezi 5.Jamaa kachanganyikiwa anadai mkewe alitoka na rafiki zake wa kike wakaenda disco kitu ambacho alikuwa anafanya mara moja moja hata mumewe akiwepo[ladies nightout].Siku hiyo wenzake walikuwa wakicheza akaja mwanaume aliyeonekana msaarabu na kuomba kukaa naye,baada ya maongezi ya kawaida jamaa akaamka kufata kinywaji na kuomba kumletea na yeye.Baada ya kunywa kinywaji hakumbuki kilichotokea akajikuta kwenye chumba cha hoteli akiwa uchi asubuhi ya pili huku akiwa peke yake.Aliporudi nyumbani na kuwapigia simu rafiki zake wakamwambia hata wao walishangaa alivyoondoka gafla wakadhani hakujisikia vizuri na kurudi nyumbani.Alipima ukimwi na kujikuta salama lakini kuhusu mimba alitaka mumewe arudi waamue la kufanya.Hajaripoti polisi kwakuwa hamjui jamaa aliyembaka.
Rafiki yangu anadai anampenda sana mkewe na angeweza kutoa mimba bila ya yeye kujua na muda pia ungeruhusu.Yuko njia panda kuhusu kulea mtoto wa mtu huko wenyewe hawana mtoto.Nimshaurije?

kichekesho! waamue la kufanya wakati mimba sio ya mume wake? huyo mwanamke hayupo serious kabisa, khaa ningekuwa mie ndio mwanaume hapo ningemwacha moja kwa moja, mwanamke hatumii akili yake ya kuzaliwa japo kidunchu? nani anahakika kama kweli alijishtukia tu asubuhi chumbani? halafu kama mmeamua kutoka nyie kama nyie iweje mhangaike na kibia ki1 viwili vcvyo na muelekeo?
 
haya kupenda penda ofa......kama ni mie nampiga chini mwanamke huyo.......
Utapiga chini wangapi Yo Yo! Dunia ya leo imejaa ulaghai, wakweli ni wachache sana. Utampata mwingine na akakuonyesha vituko hadi ukamkumbuka huyo aliyeamua kusema ukweli.
To err is human, to forgive is devine!
 
Mh it could happen to you too au kwa vile ninyi hamzibebi hizo mimba?. Hakupenda na inaonekana kabisa alitiliwa vitu katika hicho kinywaji. Kwa vile si kwamba alitoka bila idhini ya mumewe hajafanya kosa hapo.

Kosa lake la 1: Kukubali kinywaji toka kwa mtu asiyemfahamu vizuri. (Ila angejuaje kama hana nia nzuri naye?)

Kosa la 2: Kuwa honest sana kwa yeye kumsubiri mumewe aje waamue hatima ya mimba hiyo. Angeweza kabisa kuitoa na kisha kuuchuna na kuplay yirgin mary mumewe akirudi. BUT alikuwa mwaminifu and I give her 5 for that what if angeamua aitoe mwenyewe bila kusema je angekufa katikati ya hilo zoezi? wewe kama mumewe ungesemaje baada ya kujua ukweli ( hasa kuwa alileweshwa kwa dawa za kulevya tuseme) na kubakwa?

mie huo uaminifu wake nauchukulia kama ni mjinga/mpumbavu.
 
Huyu dada mwehu au alitaka kumpa presha za bure mume wake, kama hakuwa ameambukizwa ukimwi na kwa kusubiri uamuzi wa mume wake inamaana yupo tayari pia kutoa hiyo mimba, sasa alimsubiri mume wake ili iweje? kwani angetoa tu hiyo momba na kutulia ili asimuumize roho mume wake angekosa nini? Mshauri jamaa aachane na huyu mwehu atakuja kumuua kwa presha tu, akimuacha kwa hili siku nyingine atakuja kugongwa na mtu akaja kumuelezea jamaa yake kisha aombe msamaha.

kwanza huyo mwanaume siamini kama ni msamaria ki hivyo, ulee mimba ya mwanaume mwenzio mchezo? mie hii ishu hainiingii akilini kabisa.
 
Utakubalije kwanza kutoka out kama mume wako hayupo, tena usiku?? Kwa kuonyesha upendo miezi sita si mingi kwa kumsubiri umpendaye, kwani maeneo ya starehe huwa yana vishawishi vyake, so angekaa mbali nayo.

Pili utakubalije offer ya mwamume usiyemfahamu vizuri. Hayo ni matokea ya free lunches!!! Tuache kupenda dezo, zina madhara makubwa!!!

inategemea na mnavyoishi humo ndani, wengine huwaga tunatoka bila tatizo ili mradi uage ki undani mtu akuelewe, hapo pengine mie ndipo panaponimaliza, huyu mwanamke cdhani kama yupo timamu, na amgande sana huyo mumewe mana ndio anaeweza kuvumilia ujinga wake.
 
kwanza huyo mwanaume siamini kama ni msamaria ki hivyo, ulee mimba ya mwanaume mwenzio mchezo? mie hii ishu hainiingii akilini kabisa.
inategemea na mnavyoishi humo ndani, wengine huwaga tunatoka bila tatizo ili mradi uage ki undani mtu akuelewe, hapo pengine mie ndipo panaponimaliza, huyu mwanamke cdhani kama yupo timamu, na amgande sana huyo mumewe mana ndio anaeweza kuvumilia ujinga wake.

...ndio muamini kuna watu 'wanalambishwa!' :(
 
Ah Mbu wanalambishwa nini?......

.....aaaa, kumbe hukumsoma kisale kule kwenye ile thread ya; https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/26456-limbwata-3.html

haya basi, ngoja nikumegee alivyosema;

kisale kisale is online now
kisale has no status.
Member

Join Date: Tue Mar 2009
Posts: 27
Thanks: 0
Thanked 5 Times in 5 Posts
Rep Power: 0

Default Re: Limbwata

Jamani niwaambie limbwata lipo,tena muwe makini kabisa na haya mambo!Kuna ishu moja ilitokea huko mkoani Iringa mama mmoja aliamua kumpa mume wake limbwata kwa vile alikuwa anapata hela nyingi ila hatulii nyumbani kabisa.

baada ya kumuwekea hayo madawa aliyopewa kwa mganga mwanaume alitulia ndani kupitiliza,akawa haendi kufanya biashara zake,akawa hataki hata kutoka ndani ya nyumba,kunya humo humo,kukojoa humo humo,hata kuoga,baada ya miezi 3 kupita hela zikaisha mwanamke akaanza kuhangaika,

alivyorudi kwa mganga ,mganga akamwambia yeye mwenyewe hawezi kumrudisha kwenye hali yake ya kawaida kwa sababu alizidisha dawa tofauti na kipimo alichoambiwa na mganga.ilikuwa shughuli pevu ndugu wa mwanaume walivyokuja kugundua ndugu yao yupo ndani miezi 3,wao walifikiri kasafiri,

walipoenda kumtembelea ilikuwa shughuli kumtoa ndani,alikuwa anaonekana ana akili timamu ila hataki kutoka nje ya nyumba,walisaidiana wanaume kama 10 hivi ndio wakafanikiwa kumtoa nje.yule mwanamke akachapwa viboko akamtaja mganga aliyempa dawa,nae akakamatwa na wanakijiji ila tatizo alikuwa hawezi kumrudisha kwenye hali ya kawaida.

mpaka mzee mmoja alivyojitokeza akampa jamaa midawa ya miti shamba akawa kawaida kabisa.ilibidi amfukuze mke wake na mganga akalipa faini ofisi ya kijiji.
Kwa hiyo wana jamii hii ishu acheni masihara ipo.Ni kuomba Mungu uliye nae asije kukuwekea hilo Limbwata la ukweli.Ila mimi mwenyewe naona hii kitu sio nzuri hata kidogo.
 
Kwahiyo nyamayao we ungeitoa mimba na kuuchuna?

...kuna 'vitoto' vingine visiki matata,...chokonoa chokonoa na wewe, havitoki ng'oo!... ushawahi kusikia ectopic pregnancy? vinaweza kumtoa mtu uhai hivi hivi!
 
Pia chochote kinawezakutokea wakati wa utoaji huo, wanaweza wakachokoa vibaya ukaharibu kizazi, unaweza hata kupoteza maisha.

Nasikia kuna watu ambao kiukoo mimba zao huwa hazitolewi sijui kama ni kweli maana nlishawahi kuambiwa;
'Kwetu mimba zetu huwa hazitolewi sasa wewe ukibeba mimba yangu afu uende ukatoe shauri yako.'
 
Nawashukuru sana wote mliochangia mada hii nawajulisha kwamba wazazi wa pande zote mbili walikaa na kuamua waache mtoto azaliwe na apewe familia ya kizungu ambaye hawana mtoto.na wenyewe wajaribu kupata mtoto mwingine baada ya muda kupita.
 
MHHH!
Kwanini familia ya kizungu? walifuata taratibu za kisheria na uamuzi ulishatolewa au ni wazo tu walilokuwa nalo?
 
MHHH!
Kwanini familia ya kizungu? walifuata taratibu za kisheria na uamuzi ulishatolewa au ni wazo tu walilokuwa nalo?

Hao wazungu ni raia wa Namibia na maongezi yameshafanyika wanasubiri mtoto azaliwe wakamilishe taratibu za kisheria.
 
Hao wazungu ni raia wa Namibia na maongezi yameshafanyika wanasubiri mtoto azaliwe wakamilishe taratibu za kisheria.
ok... na wazazi watarajiwa ni watanzania/wako Tanzania? Hao wanamibia wako huko Namibia au??
Samahani kwa maswali mengi maana nataka kujua ili kuona kama huo mpango unakubalika kufuatana na Sheria za Tz za Kuasili ( adoption)
 
Ungesoma post #01 ungeelewa,wazazi ni wanamibia jamaa tulienda naye kozi ya miezi 6 Chile aliporudi akakuta mkewe ana mimba ya mtu mwingine.
 
Back
Top Bottom