Alinitenda, aliniumiza, nataka kumuadhibu

Alinitenda, aliniumiza, nataka kumuadhibu

Aisee Uandishi Wako Mzuri Mpaka Kupelekea Kuhisi Hadithi Ya Kutungwa Kumbe Kweli.
 
Dah kama ni kweli basi nakushauri kabisa achana naye kwa moyo mweupe kabisa tena kwa kumuonesha upendo hio itakuwa adhabu tosha. Ukipanga mengine utakuwa kama yule aliyemgegeda mwanaume mwenzake kama adhabu na akajiua na akaangukia kwa Kova. Nilikuwa na kisa kama hicho nikiwa chuo kiliniumiza sana lakini nilionesha upendo muda wote hadi wakati nafunga ndoa na mtu mwingine yeye alikuwa hajaolewa na yule aliyemlaghai. Niliendelea kumuonesha upendo wa ajabu maana alikuwa rafiki yangu na sasa anapokea mshahara kutoka kwenye ofisi yangu. Hii ilikuwa adhabu kubwa kwake na alikuwa akilia kila tulipokutana. Hivi sasa wife akiingia ofisini napo ni adhabu kubwa kwake maana anajua yeye ndie alipaswa kuwa na nafasi hiyo ila too late. Usifanye kitu kitakachokushushia heshima na utu. Be matured in Decision. Unaweza kuwaza kulala nae hiyo wikiendi kama adhabu na kumbe naye anawaza kukuletea ukimwi kama adhabu kwa kwa waliomtenda
 
Dah una roho ya kishetani.. Khaa are yu for really??? Kwani kwa kosa gani alilofanya??? Nyie mbona mnaongoza kwa kuwaacha wanawake na wanakubali hali halisi na maisha yanaendelea..

Nitake radhi tafadhali,mimi ushetani nimeutoa wapi?mimi ni mtakatifu malaika wa Mungu. Ushetani anao huyo binti kumuumiza mwenzake,akamuacha sasa jamaa amepona tena anarudi kumuumiza,huo ushetani huuoni?

Tuoneeni huruma watoto wa wanawake wenzenu.
 
Wala usifikirie kumuadhibu, mwambie tu unaye wako muhibu....then kimyaaaa........
 
Mnapo ingia kwenye mahusiano mnatakiwa kujua kuna kufurahi na kuumia!
Matarajio yako yalikuwa makubwa maka vile uliweka ahadi na malaika kumbe binadamu!

Kwa maandishi yako hapo mwisho unaonesha huja ujakomaa vilivyo na unatakiwa kuumizwa kama Mara mbili tena na wala hutafukiria kulipiza kisasi bali utachukulia ni part ya mahusiano!

Na kushauri umpe adhabu ya kumpuuza,ina mtosha maana unatakiwa kujiuliza utatoa adhabu kwa wangapi? na utaumiza wangapi?umejuaje kama huto umizwa tena?

Kama unaogopa vita achana na kazi ya uanajeshi!
 
Haina haja ya kushindana nae, sababu yaliyopita yamepita wewe usifanye ukaribu nae na wala usipoteze muda wako kwa visasi
 
kuliko kumpa adhabu nipasie mimi...mkuu
Mimi nina shida nae...mkuu chonde chonde mkuu nipo chini ya miguu yako....usimuadhibu huyo..kiumbe..
KUMBUKA HALUA HAINA MAKOMBO...
 
Usilipe baya kwa baya,
samehe saba mara sabini,
 
Kwani...kuna tatizo gani mtu akidhani kuwa wewe sio chaguo muafaka kwa sasa, lakini baadae akaona unafaa?! Hukuwa tayari wakati yeye yuko tayari, mkaachana kwa ridhaa za wote wawili, hata kama mioyo iliuma...sasa hivi ameona muda muafaka kurudi...amua moja, unamtaka bado rudianeni..humtaki muambie uachane naye. Adhabu kwa nini alichokosa!? Ni wewe hukuwa tayari...si yeye!

Situation kama hizi uwa zinatokea sana.......muhimu kuangalia kama bado unampenda mkaendelea na maisha na kama unaona haumhitaji basi muachane for good.....mambo ya kulipiza unaweza jikuta unaingia matatizoni zaidi.....
 
Unadhani adhabu gani ina mfaa kwa haya maelezo yako?
Nakuelewa, Lakini wengi mnadhani nakurupuka tu kuamua kuwa anastahili adhabu.
Iko hivi; Haikutokea tu siku moja akaamua kunitosa, Alianza kwa vituko vidogodogo ambapo mara zote nimekuwa nikimuelewesha kuwa si sahihi, Nilipoona vimepitiliza nikaamua kuachia ngazi.
Hata mtoto haishauriwi kumuadhibu kwa adhabu kumbwa mwanzo tu wa makosa atakuwa hajifunzi,
Utaweka sheria zako, akikosea utamwambia amekosa, akiendelea utamuelekeza tena, akizidi utamsema, ikizidi zaidi utamkaripia, Utamgombeza na ikibidi utamchapa kabisa.
Sasa kwa huyu yote hayo yalishapita. Lengo ni kumfundisha maisha ya kimahusiano.
Na zinazokera zaidi ni kumbukumbu za vimaneno vyake vya nyodo.
Si kwa nia mbaya hii_muelewe.
 
Alitokea kuwa binti mzuri aliyenivutia machoni mwangu.
Tabia na busara zake vilistahili kusifika kwa mujibu wa nilivyomsoma na kumfahamu
ingawa ni kwa muda mfupi (kadiri ya miezi 6 ya uhusiano wetu)

Kifupi alikidhi vigezo vyangu binafsi,
Alistahili kuwa mama mtarajiwa wa watoto wangu wazuri kama tungejaaliwa kuwa pamoja.

Mwenyezi Mungu hamfichi mja wake.
Mbali ya kuwa mtaratibu, mkimya na mwenye kuonyesha kunijaali katika muda mfupi.
Binafsi, nilikuja kung'amua kuwa alikuwa yuko na kimuhemuhe cha kuingia katika ndoa na pengine ndio sababu ya yeye kuwa mnyenyekevu wa aina ile kwangu.

Tofauti na mie, Mimi mishale yangu ya uhusiano bado ilionyesha bado niponipo kamili kwa kipindi kile.
Ilinibidi nimuweke wazi juu ya msimamo wangu, kwa sababu sina hulka ya kucheza na muda wa wengine.

Basi bwana, binti kwa ujinga wake (nadhani) Kwakuwa pengine alikuwa 'desparate' na ndoa akaamua kujivisha Mabomu hivyohivyo.
Liwalo naliwe akiamini kuwa pengine nitabadilika mbele ya safari.
Akajiachia, Mguu-pande mguu sawa, Kanivulia 'Thong' yake.
Nifanyeje? Mzee mzima 'nikajilia' vyangu.

Maisha yakawa yanaenda.
Mimi niliamini muda muafaka ukifika hakika nitamvika Pete ya uchumba kidoleni mwake na mchakato wa kuhamia kambi ya wala 'Tunda kwa idhini rasmi' basi tutafanya hivyo (Nililenga kum-surprise baadae kidogo)

Baada ya miezi sita kupita katika uhusiano wetu, taratiiiiiibu binti akaanza visa vya hapa na pale.
Kwakuwa nilimpenda nilijaribu kumsihi kuwa asiwe mapepe awe na subira kwa kuwa siku zote mazuri hayahitaji pupa.
Hasa, Ukizingatia kuwa kuamua na kulikabili jambo ambalo tungedhamiria kulienendea (Ndoa)
Si la kukurupuka,Tungehitajika kujipanga haswa.

Lakini binti aliona kama vile namchelewesha,
Akaongea mengi sana.
Na hapo ndipo nilipoanza kuyaona kwa kiasi makucha na rangi yake halisi.

Nyodo zenye nakshi ya dharau kwa mbali vilitawala.
Nilijiaminisha kuwa kama hana Mtu anemtia kiburi (Kumshikia akili)
Basi atakuwa kapata bwana mtarajiwa aliemuahidi ndoa.

Mimi sikutaka wala kuhitaji sana marumbano, kwa roho safi niliachia behewa likatike.
Moyoni Iliniuma, na nilisikitika sana lakini sikuwa na jinsi.

Yapata miaka minne sasa. Naweza sema kidonda na maumivu ya uhusiano wangu na binti huyu vilishapona ingawa Naweza kukiri kuwa makovu bado yapo na yananipa kumbukumbu mbaya juu ya uhusiano wangu na binti huyu.

Hata hivyo ni wikimbili tu zilizopita;
Huyu bi dada kaanza mawasiliano mfulizo na mimi mithili ya mvua za masika.
Ni wazi yupo wanguwangu kama vile anataka kurudishia minyororo ya behewa la uhusiano wetu ambalo alilikata yeye mwenyewe kwa mikono yake mwenyewe.

Tumeongea mengi sana Lakini kikubwa kuliko yote.
Eti, Angefurahi kama tunge-spend weekend moja pamoja.
Nilipomuuliza ki-intelijensia kama hana mwanamme, akanijibu kifupi tu eti, "I'm free like a bird and ready to mingle."
Hajui tu anazidi kunitia kichefuchefu.

Nakiri kuwa binti huyu aliniumiza, alinitesa na alinikera
Kwangu mimi anastahili adhabu na si ndogo.

Wakati bado naifikiria adhabu ya kumpa natoa nafasi kwa wanajopo.
Kama kuna mwenye adhabu ambayo anadhani ni stahiki kumpa huyu binti au maoni ya nini nifanye pengine asisite.
kunipa.

NAWASILISHA.

Sijaelewa anastahili adhabu gani kwa kosa gani.Mwenyewe umeeleza ulimwambia bado upoupo. Jamani wanaume wengi hawapendi kushinikizwa ni kweli lakini, Binti amemaliza Chuo kikuu kwa mfano atakuwa na umrigani? Sasa atajuaje ni miaka gani ya wewe kufikiria? kujipanga? mmoja, miwili, mitatu, saba au muda gani na umri wake unaenda? Msichana/Mwanamke nae ana malengo ya maisha ya kuanza familia wakati fulani na ukizingatia ndoa inatarajiwa kuendana na kupata watoto. Na kuna wengine wanakuwa mioyoni mwao ( maana moyo ni kichaka) amekwishajua binti huyu simuoi lakini maahadi kibao , siku, wiki, miezi,miaka inakatika tena wakati mwingine binti anajiheshimu na kuona huyu ndio mtarajiwa wangu, mwanaume kumbe hayuko kabisa kimoyo, na anajua asilimia 100 kuwa huyu binti sitamuoa lakini bado maahadi kibao. Wanaume wenyetabia hii wabadilike kama huna haja na binti mweleze na achana nae,inauma lakini inauma zaidi unapopoteza miaka kadhaa na kushtukizia mwenzio yuko kwenye maandalizi ya harusi na binti mwingine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom