Alitokea kuwa
binti mzuri aliyenivutia machoni mwangu.
Tabia na busara zake vilistahili kusifika kwa mujibu wa nilivyomsoma na
kumfahamu
ingawa ni kwa muda mfupi (kadiri ya miezi 6 ya uhusiano wetu)
Kifupi alikidhi vigezo vyangu binafsi,
Alistahili kuwa mama mtarajiwa wa watoto wangu wazuri kama tungejaaliwa
kuwa pamoja.
Mwenyezi Mungu hamfichi mja wake.
Mbali ya kuwa mtaratibu, mkimya na mwenye kuonyesha kunijaali katika
muda mfupi.
Binafsi, nilikuja kung'amua kuwa alikuwa yuko na kimuhemuhe cha kuingia
katika ndoa na pengine ndio sababu ya yeye kuwa mnyenyekevu wa aina ile
kwangu.
Tofauti na mie, Mimi mishale yangu ya uhusiano bado ilionyesha bado
niponipo kamili kwa kipindi kile.
Ilinibidi nimuweke wazi juu ya msimamo wangu, kwa sababu sina hulka ya
kucheza na muda wa wengine.
Basi bwana, binti kwa ujinga wake (nadhani) Kwakuwa pengine alikuwa
'desparate' na ndoa akaamua kujivisha Mabomu hivyohivyo.
Liwalo naliwe akiamini kuwa pengine nitabadilika mbele ya safari.
Akajiachia, Mguu-pande mguu sawa, Kanivulia 'Thong' yake.
Nifanyeje? Mzee mzima 'nikajilia' vyangu.
Maisha yakawa yanaenda.
Mimi niliamini muda muafaka ukifika hakika nitamvika Pete ya uchumba
kidoleni mwake na mchakato wa kuhamia kambi ya wala 'Tunda kwa idhini
rasmi' basi tutafanya hivyo (Nililenga kum-surprise baadae kidogo)
Baada ya miezi sita kupita katika uhusiano wetu, taratiiiiiibu binti
akaanza visa vya hapa na pale.
Kwakuwa nilimpenda nilijaribu kumsihi kuwa asiwe mapepe awe na subira
kwa kuwa siku zote mazuri hayahitaji pupa.
Hasa, Ukizingatia kuwa kuamua na kulikabili jambo ambalo tungedhamiria
kulienendea (Ndoa)
Si la kukurupuka,Tungehitajika kujipanga haswa.
Lakini binti aliona kama vile namchelewesha,
Akaongea mengi sana.
Na hapo ndipo nilipoanza kuyaona kwa kiasi makucha na rangi yake
halisi.
Nyodo zenye nakshi ya dharau kwa mbali vilitawala.
Nilijiaminisha kuwa kama hana Mtu anemtia kiburi (Kumshikia akili)
Basi atakuwa kapata bwana mtarajiwa aliemuahidi ndoa.
Mimi sikutaka wala kuhitaji sana marumbano, kwa roho safi niliachia
behewa likatike.
Moyoni Iliniuma, na nilisikitika sana lakini sikuwa na jinsi.
Yapata miaka minne sasa. Naweza sema kidonda na maumivu ya uhusiano
wangu na binti huyu vilishapona ingawa Naweza kukiri kuwa makovu bado
yapo na yananipa kumbukumbu mbaya juu ya uhusiano wangu na binti huyu.
Hata hivyo ni wikimbili tu zilizopita;
Huyu bi dada kaanza mawasiliano mfulizo na mimi mithili ya mvua za
masika.
Ni wazi yupo wanguwangu kama vile anataka kurudishia minyororo ya
behewa la uhusiano wetu ambalo alilikata yeye mwenyewe kwa mikono yake
mwenyewe.
Tumeongea mengi sana Lakini kikubwa kuliko yote.
Eti, Angefurahi kama tunge-spend weekend moja pamoja.
Nilipomuuliza ki-intelijensia kama hana mwanamme, akanijibu kifupi tu
eti, "I'm free like a bird and ready to mingle."
Hajui tu anazidi kunitia kichefuchefu.
Nakiri kuwa binti huyu aliniumiza, alinitesa na alinikera
Kwangu mimi anastahili adhabu na si ndogo.
Wakati bado naifikiria adhabu ya kumpa natoa nafasi kwa wanajopo.
Kama kuna mwenye adhabu ambayo anadhani ni stahiki kumpa huyu binti au
maoni ya nini nifanye pengine asisite.
kunipa.
NAWASILISHA.