Alinificha hajazaa baada ya miaka 3 ndio ananiambia ukweli

Nimeshamuuliza anasema baba wa mtoto huyo kawa teja hajielewi na hataki kusikia habari ya mtoto hivyo majukumu ya mtoto wake ni yake. na kipato chake na changu huwa tunaviweka pamoja na kupanga cha kufanya

Basi ampeleke Huko kwa ndugu zake na atafute jinsi ya kumlea Huko Huko kuepusha visitation Za baba YAKE Kwako in future. Au ukubali goli Hilo Ambalo tayari umeshafungwa na uendelee na maisha.
 
mjali tumbo una matukio mengiii....kila siku unapata tukio jipya!......inamaana jana tu hapa umepata kipato cha kuweza kumuoa yule chizi wako ulompenda; na huyo chizi kapona kwa siku moja?......we dogo unazingua kama Gogle

Wadau mimi nataka mwanamke wa kuoa lakini sina hela kabisa. Je mtu unaaweza kuoa wakati huna mshiko? Nifanyeje ili niweze kuoa?) hiki ndo alichokiandika jana, asitusumbue ati!
 
miaka mingi iliyopita aliyekuwa rafiki yangu wa kike aliwahi kuniambia "Chizenga,mimi sina mahusiano na mtu mwingine,kwanza nikitaka kuwa na mahusiano na mtu mwingine nitakuwa naye na HUWEZI KUJUA"

ningekuwa mtu wa kutafakari sana ningejiuliza ana hakika gani kwamba siwezi kujua?ukweli ni kwamba uhakika wa kauli yake hiyo ni kwa sababu alikuwa na mtu na aliona sijui

miaka mingi baadaye tukiwa sio marafiki tena nilikuja kugundua wakati ule akisema yale alikuwa pia na mahusiano na mtu mwingine,

uzoefu wa mahusiano unaniambia ya kwamba wanawake wana siri nzito wanazoishi nazo lakini huwa wanazianika bila wao kujua kupitia maongezi

namna mojawapo ya kujua,ukiona mwanamke anakuambia kitu from nowhere unashangaa anakuambia jambo flani,tena hilo jambo mlikuwa hata hamzungumzii,au haliendani na mazungumzo yaliyokuwapo au hata hujauliza weka kwenye mabano jambo hilo siku moja utajua kilichojificha ndani yake

mjali tumbo, siku aliyokuambia kuwa hana mtoto ulimuuliza?
 
Cha msingi hapa wewe komaa na mkeo, pia tambua kuwa huyo mtoto ni binadamu na anahitaji malezi kutoka kwa wazazi/mzazi wake, kwa hiyo FUNGUA moyo wako, na ikibidi mchukue ukae nae hapo ili apate malezi yanayomstahili. Hauwezi jua siku moja huyo mtoto ndo anaweza kukusaidia maishani kushinda hata hao watoto waliotoka kiunoni mwako.

Take Care.

Mkuu Bill nakubaliana na uchambuzi wako.

Ila, cha kujiuliza kama aliweza kudaganya wakati ule kutokana na mazingira yaliyokuwepo, kuna uhakika gani kuwa huko mbele hayatatokea mazingira ya kumfanya adanganye tena?!
 
Tulikutana chuoni na kufahamiana mwaka 2008 ,mwaka 2009 tulimaliza na kupata ajira yeye akiwa education na mimi engineering tukapata ajira na kuanza maisha ya ndoa katika kipindi hicho chote mpaka naenda kwao aliniambia hajawaku kupata mtoto kama mimi kutokana na masomo.

Mwaka jana mwezi wa nane ndio ananiambia anamtoto wake yuko kwa shangazi yake alimzaa alipomaliza kidato cha sita akisubiri kuja chuo 2005.

Na kwamba mwanae na yuko darasa la nne na inabidi katika bajeti zetu tulweke hilo.

sasa kinachoniumiza ni kwa nini alinificha na sasa tunaingia kwenye garama tusizo plan?binafsi napata tabu kama kuna mapenzi ya kweli maana hata baadhi ya rafiki na ndugu sijui watanionaje.

Simlaumu mtoto wala siumii matunzo yake bali kule kudanganywa.
pole kwa kununua mashine used ila endelea kuchunguza utajua mengi sana anaonekana anakuzidi akili kwa kitendo cha kukuficha inamaana hata simu haongei nae na kipindi unaoa hukujua ulikuwa haupo makini sana pole
 
siamini tu yani
halafu siku hizi siamini amini tu

Inawezekana my dada hata sisi wanaume tunaweza kua na watoto tukaficha ila mara nyingi wadada ndoi hufanya hivyo?ila hilo swala la kumuingiza kwenye bajeti hapo napatlia shaka

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hayo ni mambo yapo katika mahusiano. Kuna kudanganya kwenye mapenzi. Hata sisi huwa hatuwaambii ukweli pale inapotokea tumezaa kabla ya ndoa. Wanakuja kuelewa baadae sana, wanakuwa hawana jinsi. Mwisho wa siku ni kusameheana na kuendelea kuishi (ili mradi tu muwe mlikuwa mnaishi kwa amani). Nitakupa mifano miwili. Jamaa alioa akiamni kabisa kuwa mkewe kamaliza kidato cha nne. na vyeti alikuwa anaviona vikwa nyumbani. Mkewe nae alikuwa amepata kazi nzuri tu (hilo pia lilithibitisha kuwa mwanamke huyo alikuwa na elimu hiyo) Sasa ikawa kila akimwambia mkewe aende shule anakataa. Wenzake wote wakawa wanaenda shule wanamaliza yeye mmmmm. Tatizo kwenye familia hiyo lilikuwa ulevi wa mke na kila mara kufumwa amekaa kihasarahasara sehemu mbayambaya Ndani ya mizozo hiyo ndio jamaa akaja kujua kuwa mkewe alikuwa anatumia vyeti vya kufoji kazini. Hiyo ilikuwa baada ya miaka 15 kupita wakiwa pamoja. usuluhishi ukashindikana wakatengana.
 
Tulikutana chuoni na kufahamiana mwaka 2008 ,mwaka 2009 tulimaliza na kupata ajira yeye akiwa education na mimi engineering tukapata ajira na kuanza maisha ya ndoa katika kipindi hicho chote mpaka naenda kwao aliniambia hajawaku kupata mtoto kama mimi kutokana na masomo.

Mwaka jana mwezi wa nane ndio ananiambia anamtoto wake yuko kwa shangazi yake alimzaa alipomaliza kidato cha sita akisubiri kuja chuo 2005.

Na kwamba mwanae na yuko darasa la nne na inabidi katika bajeti zetu tulweke hilo.

sasa kinachoniumiza ni kwa nini alinificha na sasa tunaingia kwenye garama tusizo plan?binafsi napata tabu kama kuna mapenzi ya kweli maana hata baadhi ya rafiki na ndugu sijui watanionaje.

Simlaumu mtoto wala siumii matunzo yake bali kule kudanganywa.
Baba wa mtoto yuko wapi? au wewe ni UNICEF?
 
Wadau mimi nataka mwanamke wa kuoa lakini sina hela kabisa. Je mtu unaaweza kuoa wakati huna mshiko? Nifanyeje ili niweze kuoa?) hiki ndo alichokiandika jana, asitusumbue ati!

wengine tunaruhusiwa kuowa wake wanne ndugu. hivyo kuowa mke wa kwanza usishangae kusikia nataka kuowa tena.
 
ndio maana mie nimesema siamini..huu ni utunzi mwingine tu
Wadau mimi nataka mwanamke wa kuoa lakini sina hela kabisa. Je mtu unaaweza kuoa wakati huna mshiko? Nifanyeje ili niweze kuoa?) hiki ndo alichokiandika jana, asitusumbue ati!
 
pole kwa kununua mashine used ila endelea kuchunguza utajua mengi sana anaonekana anakuzidi akili kwa kitendo cha kukuficha inamaana hata simu haongei nae na kipindi unaoa hukujua ulikuwa haupo makini sana pole

haongei na mwanae kabisa na ndugu zake walikuwa kama wanamsaidia,yaani alificha sana hata nilipoenda kwao mara ya kwanza huyo mwanaye wala hakuletwa aliachwa huko kwa shangazi ingawa ni majrani.
 
cc: HHHK
halafu mwwanamke aliye na mtoto ni rahisi kumgundua..mara nyingi maumbile hujionyesha
Wadau mimi nataka mwanamke wa kuoa lakini sina hela kabisa. Je mtu unaaweza kuoa wakati huna mshiko? Nifanyeje ili niweze kuoa?) hiki ndo alichokiandika jana, asitusumbue ati!
 
Last edited by a moderator:
miaka mingi iliyopita aliyekuwa rafiki yangu wa kike aliwahi kuniambia "Chizenga,mimi sina mahusiano na mtu mwingine,kwanza nikitaka kuwa na mahusiano na mtu mwingine nitakuwa naye na HUWEZI KUJUA"

ningekuwa mtu wa kutafakari sana ningejiuliza ana hakika gani kwamba siwezi kujua?ukweli ni kwamba uhakika wa kauli yake hiyo ni kwa sababu alikuwa na mtu na aliona sijui

miaka mingi baadaye tukiwa sio marafiki tena nilikuja kugundua wakati ule akisema yale alikuwa pia na mahusiano na mtu mwingine,

uzoefu wa mahusiano unaniambia ya kwamba wanawake wana siri nzito wanazoishi nazo lakini huwa wanazianika bila wao kujua kupitia maongezi

namna mojawapo ya kujua,ukiona mwanamke anakuambia kitu from nowhere unashangaa anakuambia jambo flani,tena hilo jambo mlikuwa hata hamzungumzii,au haliendani na mazungumzo yaliyokuwapo au hata hujauliza weka kwenye mabano jambo hilo siku moja utajua kilichojificha ndani yake

mjali tumbo, siku aliyokuambia kuwa hana mtoto ulimuuliza?

sikumuuliza tulikuwa tu kwenye maongez ya kawaida akaanza kunambia shangazi zake wanamsumbua ndio akaniambia nimsamehe kwa atakayonieleza na nimsaidie akanieleza
 
Siku hizi watu waongo sana.. tukianza na huyu mleta uzi, muongo sana!!! Jinsia zote, waongo sana..
 
Tulikutana chuoni na kufahamiana mwaka 2008 ,mwaka 2009 tulimaliza na kupata ajira yeye akiwa education na mimi engineering tukapata ajira na kuanza maisha ya ndoa katika kipindi hicho chote mpaka naenda kwao aliniambia hajawaku kupata mtoto kama mimi kutokana na masomo.

Mwaka jana mwezi wa nane ndio ananiambia anamtoto wake yuko kwa shangazi yake alimzaa alipomaliza kidato cha sita akisubiri kuja chuo 2005.

Na kwamba mwanae na yuko darasa la nne na inabidi katika bajeti zetu tulweke hilo.

sasa kinachoniumiza ni kwa nini alinificha na sasa tunaingia kwenye garama tusizo plan?binafsi napata tabu kama kuna mapenzi ya kweli maana hata baadhi ya rafiki na ndugu sijui watanionaje.

Simlaumu mtoto wala siumii matunzo yake bali kule kudanganywa.
Mbona kawaida tu ndugu yangu au umeanza kumchoka nn? Maana wanaume ndo zetu hizo! Kwani mtoto ni nn na anatumia nn hicho ambacho huwezi gharamia?
 
Mkuu Bill nakubaliana na uchambuzi wako.

Ila, cha kujiuliza kama aliweza kudaganya wakati ule kutokana na mazingira yaliyokuwepo, kuna uhakika gani kuwa huko mbele hayatatokea mazingira ya kumfanya adanganye tena?!

Mkuu Asamwa, suala la kudanganya ni pana na ni la hatari sana ikiwa tu anaedanganywa atagundua. Linahitaji busara ya hali ya juu kutumika

Huyu mama ndio alidanganya ili apate mume, na angeweza kuendelea kukaa kimya, huyo jamaa asingefahamu na angeendelea kuamini kuwa mke wake ni mkweli na hajawahi kudanganya.

Kusema kuwa atakuja kudanganya tena mbele ya safari sio sahihi kwani, mimi na wewe tunajua wenzi wetu watakuja kutudanganya mbele ya safari.

Hii ni sawa na kusema, huyu mwanamke sijamkuta na bikra, kwa maana hiyo alikuwa anatembea na wanaume. Nikimuoa anaweza kuendelea tena kutembea na wanaume wengine mbele ya safari. Kwa maana hiyo utataka kuoa mwanamke mwenye bikra ili asije kutembea na wanaume mbele ya safari. Je hili linawezekana kirahisi rahisi namna hiyo? HAPANA, inategemea na akili za mtu/mhusika
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom