Alimsomesha chuo, baada ya kumaliza masomo ndugu wakadai hana uwezo wa kuishi nae

McCollum

JF-Expert Member
Jan 10, 2023
384
679
Habari za Jumapili?

Naomba niende moja kwa mona kwenye mada, hiko hivi, kuna kijana ambaye ametokea mkoa mmoja huko Kanda ya Kaskazini, huyu hakuwa na wazazi wote wawili kwani walifariki kipindi alipokuwa mdogo sana. Kwa kipindi kirefu cha Elimu yake alikuwa akiishi na bibi upande wa mama (kuanzia alipoanza darasa la kwanza mpaka alipohitimu kidato cha nne).

Ndugu upande wa baba na mama yake walikuwa wakiishi mbali na mkoa aliokuwa akiishi kijana huyu (Tumuite Dan, hili ni jina la kubuni). Baada ya kumaliza kidato cha nne matokeo yalitoka na Dan alikuwa amefaulu kwa daraja la tatu la mwanzoni. Shida ilikuja kwenye gharama za kumsomeshea A-level, bibi angepata wapi pesa? Hakukuwa na mahala pakupata pesa hizo, baadhi ya wasamaria wema wa mawazo walimahauri kijana Dan amfuate mkuu wa wilaya na kumuomba msaada.

Dan alilichukua lile wazo na kulifanyia kazi, mkuu wa wilaya aliguswa na namna ambavyo Dan alikuwa akiipambania Elimu licha ya kuwa katika mazingira magumu na akaahidi kumsaidia. Ulipofika muda muafaka wa kuanza shuld Dan alikabidhiwa mahitaji ya shule ambayo yalihusisha uniform, madaftari, pesa ya kujikimu lakini upande wa ada yule mkuu wa wilaya alifanya malipo kabla na kumkabidhi Dan pay slip. Sikwamba mkuu wa wilaya alikuwa akitoa pesa zote peke yake, la hasha, mkuu wa wilaya ali"organize" wadau ambao walikuwa wakisaidia kuwasomesha vijana ambao hawakuwa na msaada wowote kutoka kwa ndugu zao (ingawa hawakuwa wengi).



Dan aliingia Advance na alichagua mchepuo wa HGL, na huko baada ya kufanya mtihani wa taifa-NECTA ya kidato cha sita (ACSEE) alipata division two, baada ya kurejea kijijini lwa bibi yake alianza kujiandaa kufanya application za chuo, muda huu Dan alikuwa akijihusisha na kazi ndogo ndogo za kusukuma siku na kumsaidia bibi yake ambaye alikuwa akipata msaada mdogo kutoka kwa ndugu na mara nyingi alikuwa akisaidiwa na majirani ambao waliguswa na maisha yake duni.

Hata yalipotoka majina ya vijana waliochaguliwa kujiunga jeshi jina la Dan halikuwepo, hii ilimpa muda kukaa na bibi yake ambaye ndiye aliyekuwa mama, baba, shangazi, mjomba na ndugu zake wa karibu. Dan alikuwa akisikia tu kutoka kwa bibi zake kwamba kuna baadhi ya ndugu zake ambao walikuwa maeneo ya Ukerewe na walikuwa wakijiweza kiuchumi lakini hakuwahi mwambia kwanini ndugu hao waliamua kuwatupa kiasi hicho na kuwaacha wakijipaka matope ya ufukara wa hali ya juu.
SEHEMU YA PILI
SEHEMU YA TATU
 
DAN AJIUNGA NA CHUO CHA UDSM

Baada ya muda wa kuingia chuo kufika Dan alijiandaa kuelekea Dar Es Salaam, muda huu angalau alikuwa na matumaini ya kuwa maisha yangekuwa mazuri na angeweza kumsaidia bibi yake kwani naye alikuwa miongoni mwa wanafunzi waliopata mkopo wa Elimu ya juu kutoka bodi ya mkopo-HESLB

Dan aliwasili Dar Es Salaam akitokea huko Kaskazini, katika chuo kikuu cha Dar Es Salaam alichaguliwa kujiunga na kozi ya Ualimu wa masomo ya arts (Masomo ya sanaa). Alipopata pesa mara ya kwanza alimtumia bibi yake kupitia jirani ambaye ndiye aliyepokea pesa kwenye simu yake, Dan aliona ingekuwa bora kama angemnunulia bibi yake simu na alifanya hivyo baada ya semisters mbili kuisha (mwaka wa kwanza kuisha).

Baada ya mwaka wa pili wa masono kuanza Dan tayari alikwishakuwa mwenyeji wa Dar hata ule ugeni wake katika stendi mbalimbali za Dar ulikuwa umemtoka kabisa. Baada ya masomo kuwa kichwani Dan aliona ulikuwa wakati muafaka wa kujipatia mpenzi wa kike na hapo macho yake aliyatua kwa Rachel (si jina lake halisi). Huyu Rachel yeye alikuwa akitokea kwenye mkoa mmoja wa kusini mwa Tanzania na alikuwa mtoto wa baba aliyekuwa bwana mifugo na mama ambaye alikuwa akifanya kazi katika Halmashauri (kitengo chake tukitie kapuni kwasasa).

Rachel yeye alikuwa miongoni mwa wanafunzi ambao hawakubahatika kupata mkopo, Dan akaona sio shida kama yeye ana mkopo atajitahidi kadri awezavyo kimsaidia huyo mpenzi wake.

Dan aliamua kujitoa sadaka mazima,
licha ya wazazi wa Rachel kutuma pesa kwa binti yao Dan alikuwa akipambana kumpatia hata robo ya ada huyu alimuona kama mpenzi wake wa maisha. Dan hakuona kama alitakiwa kuwa na kompyuta mpakato kwani angeshindwa kimsaidia mrembo wake, ile pesa ya Laptop aliitumia akiwa na mpenzi wake. Rachel na Dan wote walikuwa wakisoma kozi moja na baada ya kumaliza masomo wote walichukua pesa walizitunza kama akiba na kuamua kuenda kwenye moja ya mkoa wa Kusini mwa Tanzania ili waanze maisha.

NB: Nashindwa kutaja majina ya mikoa na wahusika kwakuwa inawezekana mhusika akapita hapa nankunitambua though sina uhakika kama hiki alichowahi kunisimulia aliniambia mimi pekee, ila kuna baadhi ya vitu ambavyo akiviona angeweza kujua labda mimi ndiye niliyeamua kumuandika humu
 
IMG_3329.jpg
 
BAADA YA KUFIKA MKOA WA KUSINI MWA TANZANIA.

Rachel alikuwa na ndugu zake katika huo mkoa ila kwa upande wa Dan wala haikuwa hivyo yeye alikuwa mgeni tu aliyeamua kuja kuanza maisha. Wakitumia ile akiba yao walifungua duka dogo la bidhaa ambalo lilijaa kiasi chake.

Dan yeye alikuwa mchangamfu hivyo alifahamiana na watu wengi na mimi nikiwemo, baada yakuishi kwa pamoja kwa miezi miwili hatimaye Rachel alipata ujauzito wa Dan na wote walipata shauku yakuwa na mtoto, Rachel alimtaarifu dada yake ambaye alikuwa akiishi mkoa huo huo.

Dada mtu alimtaka Rachel amtembelee nyumbani kwake, Dan aliagwa na mchumba wake na hapo rasmi akaanza kuishi peke yake japo ilikuwa ahadi ya kuwa mkewe mchumbake angekaa kwa wiki moja siku zilisonga tu, Dan kila alipojaribu kumtafuta huyo Gf wake alikuwa akijibiwa majibu mepesi yaliyochangamana na madeko basi alikuwa akitulia.


Kwa bahati mbaya sijui ni mila za huko alikotoka au uvivu binafsi Dan hakuwa akipika bali alikuwa mtu wa kula kwa mama muuza, yaani pesa ile ile ambayo ingekuwa ya faida yeye aliingiza kwenye chakula, duka lilianza kuyumba na hapa hata kodi ikawa inamsumbua. Muda huu Dan aliamua kuanza kuzungusha barua kwenye baadhi ya shule binafsi ili kuomba kazi lakini mambo yalikuwa hola, mara nyingi alikuwa akiambulia maneno haya "tutakutafuta, kama namba yako hipo kwenye barua haina shida kijana".


Baada ya mwezi na ushee kupita Rachel alirejea kwa Dan lakini muda huu alikuwa amebadilika kabisa alikuja na demand mpya, Rachel alimtaka Dan amuoe tena kwa harusi kwani alidahi ndugu zake walimuona mtu wa ajabu kuishi na mwanaune kienyeji. Dan alijaribu kumuelezea Rachel kwamba ule haukuwa wakati muafaka lakini msimamo wa Rachel ulikuwa pale pale.

Rachel alitumia mwanya wa mama mwenye nyumba kidai kodi kupenyezea ajenda nyingine baada ya kumwambia Dan anamuonea huruma kwakuwa hana pesa hivyo anataka arudi kwa dada yake na angekuwa akimtembelea baada ya muda. Dan hakuona kama jambo lile lilikuwa likieleweka ila kila alipojaribu aliishia kishindwa kumshawishi Rachel, baada ya muda hata lile duka likaisha kwani lilibakiza bidhaa chache sana ambazo Dan aliziuza na kulifunga rasmi. Rachel aliondoka na kumfuata dada yake na muda huu Dan akaona kweli labda ukata unamkimbiza mchumba wake na yeye akaamua kusaka kazi kwa nguvu ili kuikimbia njaa.

Baada ya wiki moja Dan alipigiwa simu na dada wa Rachel na kuulizwa kama alikuwa tayari kumuoa Rachel, Dan hakuwa na jibu la haraka haraka ila alisema alikuwa tayari ila sio kwa muda huo.

Rachel alimfuata Dan na kumueleza kwamba hawezi kuwa nae tena kwani ndugu zake walikuwa wanataka wao waoane na sio kuishi ki-hunihuni, Rachel alikuwa akimwambia Dan basi ajichange apeleke hata laki tano kwao ili wazazi wake wajue kweli kuna ndoa na wala si kuchezeana. Dan hakuwa na pesa hivyo aliamua kufunguka ukweli kwamba hana pesa . Rachel kwa haraka alimwambia basi yeye ataolewa na mtu mwingine ambaye alifika kwao kuposa, Dan alihamaki na kuuliza kuhusu mtoto na alijibiwa kwamba mimba ilikwishatolewa.

Rachel aliondoka na kurudi kwa dada yake mazima hakuwa akipokea simu ya Dan na hiyo ikawa n'tolee mazima mdau wangu akawa ametemwa mazima.
 
MAISHA BILA YA RACHEL

Baada ya kukimbiwa na aliyekuwa mpenzi wake Dan alikimbilia kutafuta pesa ila baada ya kuona mambo yamemshinda aling'oa nanga na kurejea kwao huko Kaskazini akidahi alikuwa akienda kwenye machimbo kutafuta pesa.

Baada ya msoto alinicheki last time nakuniambia alipata ajira zile zilizotangazwa na Serikali na alipangiwa shule moja ya Sekondari ambayo sitaitaja ila inapatikana Kasulu Kigoma.
 
bado sijakupata kwani shida iko wapi?sijaona sehemu zaidi ya kumhonga,au kosa la recho liko wapi?nimeshindwa kuelewa kwa kweli au story haijaisha?
 
Vijana wengine wa hovyo sana,,,hela hana halafu anajiforce kumfanya demu wake awe happy,,,mbwaa kabisaa.
 
Mpenzi akinifanyia usaliti siwezi kumfanya chochote hata kama imenigharimu kiasi gani, ila mke wangu akinisaliti aisee mtasikilizia kwenye vyombo vya habari.
 
bado sijakupata kwani shida iko wapi?sijaona sehemu zaidi ya kumhonga,au kosa la recho liko wapi?nimeshindwa kuelewa kwa kweli au story haijaisha?
Ina muendelezo sehemu ya pili na ya tatu hapo hapo kwenye posti ya kwanza
 
Mwanamke hakua na mapenzi ya kweli kwa bwana dani. Huwezi toa mimba ya mwanaume unaempenda kwa kukusudia kabisa.
 
Matatizo mengne vijana tunajitafutia,.. unajua fika kuwa pesa huna af unang'ang'ania mapenzi, upuuzi wa hali ya juu sijui tuseme mara ngapi ila ivo ivo tutaendelea kukumbusha,
DATING ISN'T FOR BROKE MEN..
 
Matatizo mengne vijana tunajitafutia,.. unajua fika kuwa pesa huna af unang'ang'ania mapenzi, upuuzi wa hali ya juu sijui tuseme mara ngapi ila ivo ivo tutaendelea kukumbusha,
DATING ISN'T FOR BROKE MEN..
Sasa sisi tupige puchu tu ama!??
Tutabanana humo humo
 
Back
Top Bottom