Alikataa nisimuoe kisa ualimu

Alikataa nisimuoe kisa ualimu

Miaka kumi iliyopita yani 2009 niligraduate bachelor of Education in Arts UDSM nilikuwa na mpenzi wangu aliyekuwa anaitwa Rechael yeye alikuwa anasoma Bachelor of Tax .. IFM .
Hakika tulipendana na kuendana sana ila alikuwa sister duu sana hakupenda niseme kuwa mimi ni mwalimu by professional eti nitamtia aibu kwa marafiki zake.

Baada ya sisi wote kuhitimu sikumaliza hata mwezi nikapata kazi kufundisha St Anton mbagala na nilikuwa napata take home 700k kwa mwezi huku yeye akiwa bado anahaha kutafuta ajira but haikuwa issue nilimpa kila alichokitaka kadri ya uwezo wangu nikapanga nimuoe.

Kumwambia nimuoe akagoma eti hawezi kuolewa na mwalimu aina yeyote ni aibu kubwa sana kwake na familia yake sio siri niliumia sana but kwakuwa mimi sipendi fake love nikaamua bora tuachane.

Ktk pitapita zangu nikakutana na mtoto Glory ambaye alikuwa anasoma KCMC bachelor of Medicine akanipenda kweli na Inshaalah nilimuoa na mpaka sasa ni mke wangu na tumezaa watoto wawili.

Huwezi amini ile dharau ya Rechael ilinifanya nirudi shule kusoma zaidi na sasa Alhamdulillah nimefika sehemu nafanya kazi nzuri zaidi kwa maslahi zaidi huku nikiwa na miradi kibao hapa mjini ikiwemo uber, bodaboda, maduka etc.

Leo ktk pitapita zangu mitandaoni nikakutana na friend request kucomfirm kumbe ni Rechael akiniuliza maswali kibao na kunilaumu eti yeye ilikuwa ni ujana na ujinga tu tu hivyo haikuwa akili yake akaomba nimsamehe sana kwani bado ananipenda sana.

Nikamwambia siunajua kuwa nina mke sasa kajibu ndio ila yeye hajali na hawezi kubali kunitoa moyoni ni utoto tu hivyo yupo tayari nimuoe mke wa pili nikakumbuka wimbo wa "barua" ya Bushoke aliposema "kumpenda bado ninampenda msemakweli mpenzi wa Mungu" ila ninachofikiria ni mke wangu wa sasa.

Nimuoe mke wa pili au nimfanye outside chick hizo ni option nilizojipa coz bado ninampenda ukizingatia ni mtoto wa kiislamu full maadili bikra yenyewe kikombe nimekidondosha mimi kikavunjika!
Ila je ananipenda tu nikiwa na hadhi je nikiporomoka itakuwaje mana mshika mawili moja humponyoka au kukosa yote.

Nishaurini wadau ila naomba ushauri kutoka wanajf ambao atleast wana 30 yrs na kuendelea mana jf ya sikuhizi utoto mwingi
Maryme

Mzee sio dhana ya wewe kufuta dp akati jina umeliacha wazi.

maryme

Eti anaitwa Rachael ??????

Hahahaaaaaaa watu mnapenda majina matamu
 
Tulia na umuheshimu sana mke wako.kumbuka mlikotoka.
Hakuna mtu wa kumtahmin kama alietoka nawe mbali ukiwa chini wengine wakikuona takataka ye akauona dhahabu.
Nasema tena tulia ule wanao achana na hilo dubwasha..

Hivi mkeo akija kugundua huyo unataka kumuoa ndo ex wako nadhani atakudharau kabisa,pia utamshushia heshima.
All in all mtajua wenyewe,nimechoka kushupalia ya watu.
 
Glory sio jina la kiislam, Rachel Pia ila hapa unazungumzia ndoa ya.wake wawil
Anyways labda kama wote wmeshabadl dini
 
Ukimuoa huyo unaporomoka kiuchumi na laana unapata. Hii story yako kuna vitu umetunga though.
 
Watoto wa IFM bana, wanakula sana bata. Na mbaya zaidi wapo City center, wakware wote ndio wanaponea pale.
Lakini mtoa mada inawezekana wewe tu huna swagger, mbona mimi ni Dj na nilipata baby pale.
 
Huyu mtoa mada kwa kuwa ni muongo muongo ngoja na sisi tumtafute MD Glory, tuwe tunajipigia mdogomdogo ili kubalance mambo
 
Miaka kumi iliyopita yani 2009 niligraduate bachelor of Education in Arts UDSM nilikuwa na mpenzi wangu aliyekuwa anaitwa Rechael yeye alikuwa anasoma Bachelor of Tax .. IFM .
Hakika tulipendana na kuendana sana ila alikuwa sister duu sana hakupenda niseme kuwa mimi ni mwalimu by professional eti nitamtia aibu kwa marafiki zake.

Baada ya sisi wote kuhitimu sikumaliza hata mwezi nikapata kazi kufundisha St Anton mbagala na nilikuwa napata take home 700k kwa mwezi huku yeye akiwa bado anahaha kutafuta ajira but haikuwa issue nilimpa kila alichokitaka kadri ya uwezo wangu nikapanga nimuoe.

Kumwambia nimuoe akagoma eti hawezi kuolewa na mwalimu aina yeyote ni aibu kubwa sana kwake na familia yake sio siri niliumia sana but kwakuwa mimi sipendi fake love nikaamua bora tuachane.

Ktk pitapita zangu nikakutana na mtoto Glory ambaye alikuwa anasoma KCMC bachelor of Medicine akanipenda kweli na Inshaalah nilimuoa na mpaka sasa ni mke wangu na tumezaa watoto wawili.

Huwezi amini ile dharau ya Rechael ilinifanya nirudi shule kusoma zaidi na sasa Alhamdulillah nimefika sehemu nafanya kazi nzuri zaidi kwa maslahi zaidi huku nikiwa na miradi kibao hapa mjini ikiwemo uber, bodaboda, maduka etc.

Leo ktk pitapita zangu mitandaoni nikakutana na friend request kucomfirm kumbe ni Rechael akiniuliza maswali kibao na kunilaumu eti yeye ilikuwa ni ujana na ujinga tu tu hivyo haikuwa akili yake akaomba nimsamehe sana kwani bado ananipenda sana.

Nikamwambia siunajua kuwa nina mke sasa kajibu ndio ila yeye hajali na hawezi kubali kunitoa moyoni ni utoto tu hivyo yupo tayari nimuoe mke wa pili nikakumbuka wimbo wa "barua" ya Bushoke aliposema "kumpenda bado ninampenda msemakweli mpenzi wa Mungu" ila ninachofikiria ni mke wangu wa sasa.

Nimuoe mke wa pili au nimfanye outside chick hizo ni option nilizojipa coz bado ninampenda ukizingatia ni mtoto wa kiislamu full maadili bikra yenyewe kikombe nimekidondosha mimi kikavunjika!
Ila je ananipenda tu nikiwa na hadhi je nikiporomoka itakuwaje mana mshika mawili moja humponyoka au kukosa yote.

Nishaurini wadau ila naomba ushauri kutoka wanajf ambao atleast wana 30 yrs na kuendelea mana jf ya sikuhizi utoto mwingi
Tatizo liko kwako Chief
Kwanza nakunasihi
Uache utoto

Kisha
Angalia familia yako ikiwa una akili na msomi kama ulivyojinasibu.
 
Mkuu huyo atakuua mzee! Piga chini, songa mbele. Siku ukiyumba kiuchumi tuu kwisha habar yako.
 
Nilisikia wanaume wana balehe mbili eti
 
Endelea na mkeo achana na huyo, bila hivyo unachokitafuta utakipata
 
Watu wakiona umr unaenda wako tayar kufanya yasiyo tarajiwa jamani na kujibebsha kwing kumbe wiz mtupu
 
Akili za wanaume mnazijua wenyewe!

Huyo alokupenda ukiwa na uwalimu wako yeye unamuona sio kitu sababu ya mtu alokuacha sababu ya huo huo ualimu?!

Kila la kheri Mkuu, ila usidhani anakupenda wewe anapenda ulicho nacho!
 
Back
Top Bottom