Alichokisema Lissu juu ya kesi ya Wema

Alichokisema Lissu juu ya kesi ya Wema

Ameandika wakili msomi Tundu lissu

Sio msokoto wa bangi. Hati ya mashtaka dhidi yake inasema Wema amekutwa na gramu 1.08 za bangi. Gramu, sio kilogramu. Polisi waliokamata 'madawa hayo ya kulevya' walifanya sachi saa tatu usiku.

Sheria inayohusu sachi inasema sachi inatakiwa kufanyika kati ya saa moja asubuhi na saa 12 jioni ili, obviously, kupunguza uwezekano wa polisi kupandikiza ushahidi.

Tunamsubiri Paul Makonda mahakamani aje atoe ushahidi wa namna alivyojua Wema anatumia madawa ya kulevya mpaka akamtaja hadharani. Asipokuja basi kesi hakuna.
mtahangaika sana. kwa miaka mingi mmeaminishwa kwamba lissu ndio mwanasheria bora kuliko wote, kwamba hashindwi kesi, kwamba anajua sanaaaaaa kuliko wanasheria wengine. You are very wrong.
 
Mbele ya uCHADEMA na uCCM uongo hugeuka ukweli, na ukweli hugeuka uongo
 
wanasiasa wanatembea na akili za watu sana acha watuburuze na ujinga wetu yaani tanzania kilasiku muvi.
 
Lissu bana


Ila kina Lissu nao wana maswalii duuu

Lissu:Umesoma

Shahidi:Ndio

Lissu: Una uelewa wa kidogo wa mambo ya sheria?

Shahidi: Mi hayo mambo ya sheria za mahakamani sijui,maana nilisoma Physics

Lissu: Hata Newton's Law of Motion si sheria pia?Nayo huijui!?

Shahidi: Najua...Zipo kama tatu

Lissu :Ok ok...Sasa unaweza kutuambia why the last drop of urine doesn't obey
the law of gravity unless u shake it
well!!

Shahidi:Mimi hiyo sikuisoma

Lissu:Sasa kitu ulichosema unakifahamu,sasa unasema hujui,sasa huoni hata huo ushahidi unaosema ulikuwepo hapa unaweza kuwa unaongea kitu usichokijua?

Shahidi:Sijui

C n P
 
Haka kajamaa ni kaongo kupitiliza na kanawadanganta wajinga na wanamwamini kuwa anajua yaani hata polisi wakipata taarifa saa sita za usiku kuwa nyumba fulani kuna silaha watasubiri asubuhi eti!!!!? shame upon him
Mh???? In every general rule there is exeptions....! Lissu siyo mjinga anaelewa mambo ipasavyo.... Nahic hyo ulioisema ww ni exeption yke...Haihusiani na kesi hii
 
Kwa hiyo gram moja ni ndogo sana au? Mbona anasisitiza sana kuwa siyo kilogram?

Mkubwa jiongeze kidogo...hivi 1 gram ya bhange inaonekanaje? Pia nenda kwenye issue ya muda upekuzi ulipofanyika vs sheria inasemaje kuhusu muda wa upekuzi.....then connect the dots. Utapata nini TL anamaanisha na dhumuni la kumtaka Daudi Bashite (Makonda) atokee mahakamani kueleza chanzo cha taatifa ya Wema ni teja.
 
Huwezi kujivunia kushinda kesi kwa kutumia 'teknikalitizi' za kimahakama. Jivunie kesi kwa kumtetea mdai ama mdaiwa kulingana na hali halisi ya tukio zima. Usitumie mbinu ovu kuvuruga haki ya mdai. Stivu, kadhibitisha anavuta...wameenda usiku wamekuta 'msuba' wewe unasema ameonewa....!!! ndiyo maana mukulu kulu anataka nanyi mfungwe nao hao wahalifu!
Wa wapi wewe??? Lazma amtetee kwa kutumia technicality kwa sababu tunaamini aliyefanya kosa ni binadamu na anaweza kubadilika endapo akitoka nje... Vilevile hata akifungwa neno JELA lishapitwa na wakati tuamie kwenye CORRECTION HOUSE... Ova..
 
mtahangaika sana. kwa miaka mingi mmeaminishwa kwamba lissu ndio mwanasheria bora kuliko wote, kwamba hashindwi kesi, kwamba anajua sanaaaaaa kuliko wanasheria wengine. You are very wrong.
evidence to substantiate your statement! Lumumba Bwana!
 
evidence to substantiate your statement! Lumumba Bwana!
Kashindwa 'kumchomoa' Lema...mahabusu..!! Kumbuka ni mwanasheria mkuu wa Chama anawajibika kuwashughulikia wanachama wanaopatwa na maswahibu ya kimahakama. Kakimbilia sehemu anayodhani ni laini...ya mvuta 'msuba'!

---Leta hoja nyingine.
 
Oops! Tundu Lissu anatoa darasa la sheria mchana kweupe huku kesi ikiendelea. Hii ni dalili tosha ya kiuweledi kuwa hata nikiwapa "hints" mapema hawa wa upande wa mashitaka bado hawana uwezo wa kitaaluma kuwa na counter attack. Kudos mheshimiwa wakili msomi na aliyeelimika Mheshimiwa Lissu.
Yani jamaa kama anabutua kumbe anafinya, mwisho wa siku beki wanateleza na "kulaliana". Anabaki na kipa alafu anamuuliza unataka nikufunge je?
 
Back
Top Bottom