Alichofanyiwa Mrisho Ngassa ni uhuni, TFF, TPLB mnawajibika

Kichuchunge

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
338
891
Nimeona mahali kwamba eti nyota wa zamani wa Yanga, Azam, Simba, Ndanda, Mbeya City na Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mrisho Khalfani Ngassa, juzi alizuiwa kuingia uwanjani kushuhudia mechi ya Ligi Kuu.

Ngassa alizuiwa na walinzi wa milangoni maarufu Steward, ambao walimfanyia kitendo cha udhalilishaji sana, jambo ambalo nadhani linapaswa kupigiwa kelele, vinginevyo, litatuletea matatizo makubwa hapo baadaye likiota mizizi.

Kibaya zaidi, wakati wa kumzuia haukutumika hata utu, uungwana wala ustaarabu. Ilikuwa ni nguvu zaidi, kukabwa, kusukumwa na naneno ya kashifa, huo ukiwa ni udhalilishaji wa hali ya juu sana.

Alizuiwa kuingia na walinzi wa getini, waliodai wameelekezwa kusimamia mapato, ambayo yamekuwa yakishuka siku hadi siku, hivyo eti ni lazima mapato hayo ya getini yasimamiwe kikamilifu ili hela ipatikane kwa wingi.

Hivyo, Ngassa ambaye amelitumikia taifa hili kwa moyo wake wote, akiwa ndiye mfungaji kinara wa muda wote kwenye kikosi cha Stars, aliambiwa ili aingie, anatakiwa awe na tiketi au kitambulisho maalumu cha kuingilia uwanjani.

Kwa kiasi fulani walikuwa sahihi madai yao, ila walikosa hekima, busara na utu, walitumia nguvu zaidi kuliko akili, kwani mbali na kumfahamu, hawakutaka japo sekunde moja kumsikiliza kwa nini yuko hapo, walichokifanya ni kumkaba, kumvuta, kumsukumiza na maneno kibao ya kashifa!

Kwa mwili wake kusukumizwa na wale jamaa, unadhani hali ilikuaje, piga picha upate uhalisia wake, ni hatari sana ilikuwa, asikwambie mtu! Kwa kawaida, Shirikisho la Soka nchini TFF au Bodi ya Ligi TPLB hutoa vitambulisho maalumu vya kuingilia uwanjani kwa wadau maalumu pamoja na viongozi wote wa klabu za Ligi Kuu.

Hao walinzi wa getini na viongozi wa timu husika kama walivyodai, wanalitambua hilo, ingawa ni mara chache vitambulisho hivyo vinatolewa kwa wachezaji wa zamani.

Kuna haja ya TFF, TPLB na Vilabu kuwa na utaratibu maalum kwa wachezaji wetu wa zamani. Mtu kama Mrisho hapaswi kuusotea mpira wetu akitaka kuja kiwanjani. Amewahi kutupa furaha na heshima kwa nyakati tofauti tofauti kupitia mpira huu huu, inakuwaje leo akija kiwanjani anapata shida kuingia?

Wako mastaa wengi wa zamani ambao wamekuwa wakikutana na adha hii ya kidhalilishaji.
Kuna wachezaji wengi wamecheza miaka ya nyuma kwenye klabu zao pamoja na timu zao za taifa. Nchi zetu zina wachezaji waliostaafu soka kwa sababu tofauti.

Kuna sabu nyingi mno za kibinafsi, majeraha, umri, kukosana na viongozi, ukosefu wa fedha za kujikimu kimaisha kutokana na fedha ambazo wanalipwa kuwa ndogo na kadhalika. Hata hivyo, wachezaji wakishastaafu tu huwa hawaheshimiwi na baadhi ya viongozi wa soka kwa sababu zisizoepukika.

Hii ndiyo sababu viongozi wengi wanaendesha soka wanavyotaka, kisa na maana ni kuwa wachezaji hawana nguvu za kifedha kupingana nao.
Wachezaji wanapojaribu kuingia katika uendeshaji wa soka wanafungiwa.

Ni mapendekezo yangu kuwa, soka lingeachwa liendelezwe na wachezaji, hakuna siku mwanariadha ama mwanandondi atakuwa mkuu wa soka, ama mwanasoka awe mkuu wa masumbwi na kadhalika.

Shughuli hazitaweza kuendeshwa vizuri, atakuwa hana ufahamu wa kutosha wa mchezo huo unavyoendeshwa.
Hakuna siku rubani wa ndege atakuwa nahodha wa meli, daktari wa kutibu binadamu hawezi kuwa sawia na daktari wa kutibu mifugo.

Ni mengi sana ambayo mchezaji hupitia, ikifika wakati soka letu likaanza kuendeshwa na waliobobea ndipo tutaanza kuona mabadiliko halisi.
Ni aibu mchezaji unasukumwa na walinzi wa milangoni bila kuwa na heshima.

Hawa ni mastaa wa hapo awali, bila wao soka letu lisingefika lilipo sasa.
 

Attachments

  • NGASSA 4.JPG
    NGASSA 4.JPG
    141.2 KB · Views: 10
Inasikitisha ila wa kulaumiwa ni Yanga na Ngasa,

Yanga walimficha Ngasa hotelini Ili asiende kucheza nje ya nchi!
Na yeye Kwa upoyoyo wake akakubali..

Baadae Yanga wakamdap akaenda Ndanda..

Tuwalaumu Yanga
Umefuka moshi wa kuni mbichi. Kinachokusikitisha ni kipi? Kuzuiliwa kuingia au yeye kutoduata taratibu zilizowekwa? Halafu Yanga anahusikaje kwenye kumzuia kuingia au yeye kwenye kutofuata taratibu? UMAARUFU HAUONDOI TARATIBU ZILIZOPO, BALI HUWA NA UTARATIBU WAKE..!! Mfano, unasafiri ndege moja na mtu VIP lakini yeye anafutwa na gari maalumu hadi jirani na ndege na wewe kama si kutembea kuelekea ilipo mizigo basi utatumia basi
 
Kuna wanakumbana na hii Kadhia hasa kwa wachezaji wa zamani Lakini ni vema ukifuata utaratibu kunakuepusha kupata Kadhia kama hii..!

Kwasababu si walinzi wote wa Steward wenye kumtambua kwamba huyu ni Legendari wa Simba SC na Yanga SC na Azam FC.
 
Wakat ngassa anacheza mpira wale walinzi wote walikuwa wanasoma primary so hawamjui kama jamaa alikuwa fundi enzi hozo alienda mpaka ulaya kufanya majaribio hvyo wasamehen
 
Inasikitisha ila wa kulaumiwa ni Yanga na Ngasa,

Yanga walimficha Ngasa hotelini Ili asiende kucheza nje ya nchi!
Na yeye Kwa upoyoyo wake akakubali..

Baadae Yanga wakamdap akaenda Ndanda..

Tuwalaumu Yanga
Mtu mzima anafichwa?
 
Inasikitisha ila wa kulaumiwa ni Yanga na Ngasa,

Yanga walimficha Ngasa hotelini Ili asiende kucheza nje ya nchi!
Na yeye Kwa upoyoyo wake akakubali..

Baadae Yanga wakamdap akaenda Ndanda..

Tuwalaumu Yanga
Naona tayari Ngada FC mshabwia miunga yenu, mnaongea ujinga tu. Mada inahusu Ngasa kuzuiwa kuingia uwanjani, wewe unasema tuwalaumu Yanga. Yanga ndio wamemzuia na kumtolea maneno ya kashfa?

Mpira bila madawa inawezekana!
 
Inasikitisha ila wa kulaumiwa ni Yanga na Ngasa,

Yanga walimficha Ngasa hotelini Ili asiende kucheza nje ya nchi!
Na yeye Kwa upoyoyo wake akakubali..

Baadae Yanga wakamdap akaenda Ndanda..

Tuwalaumu Yanga
kwamba ngasa hakwenda south afrika na akakiputa kule
 
Back
Top Bottom